Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Vita ni vita Mura.
Musiba atafute pisi kali iliyokuwa inafukiziwa na Membe aitumie kumuombea msamaha.
 
Duh..., kama mwandishi huyu, ambaye mimi nilimuona kama ni mwandishi kilaza, kanjanja na kichaa kabisa Kichaa mmoja, anaweweseka sana juu ya Zitto, kamtungia uongo, umebuma, Zitto tuko nae hapa Dodoma, anamiliki mali kama hizo!, then huyu jamaa ni kichwa sana!. Ametuheshimisha sana, hivyo najiunga na Maaskofu, Membe amsamehe tuu!.

Kitendo cha Membe kutowatii maaskofu kitamgharimu sana!. Kuna kiongozi fulani aliwahi kuwadharau maaskofu, najua ni nini kilikuja kumtokea, hivyo sitaki Membe yamkute ya kumkuta!. Amsamehe tuu Musiba!.

P.
 
Askofu Pengo Mtetezi wa wauaji
Huwezi kusikia hata siku Moja akitetea wanaoonewa
 
Yono auction wako site

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Maaskofu wametimiza wajibu wao kama watumishi wa kanisa. Inaelekea Musiba ameshalitambua na kujutia sana kosa lake, ijapokuwa amechelewa sana kuomba msamaha kwa Membe, na kwa wengine. Ameng'amua njia iliyobakia pekee kwake ni kuwatafuta viongozi wa kidini wenye ushawishi ili wapate kumuombea msamaha kwa Membe.

Sisi sote ni binadamu, na wote tunatenda makosa. Kama Mungu angalituhesabia makosa yetu tuyafanyayo kila iitwapo leo, hakika hakuna miongoni mwetu ambaye angestahili kuishi. Lakini ni vyema Musiba asitake kuuzunguka mbuyu, atoke hadharani tu na kumuomba msamaha Membe na wengine wote aliowakosea, tena kwa namna ile aliyoifanya kupitia vyombo vyake vya habari. Natambua Membe ni muumini mzuri, na tena ana kicho mbele ya Mungu wake. Anitambua amri kuwa anapaswa kumpenda jirani yake kama vile ambavyo anajipenda yeye mwenyewe. Ndiyo! Ni kweli alikosewa mno na Musiba, na dunia yote inatambua hivyo, na hata mahakama imethibitisha hivyo, lakini kama binadamu yeyote yule mwenye nafsi hai, anaweza kutafakari nukuu ifuatayo kutoka katika kipande cha Neno la Injili,

MATHAYO 18

15 “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwambie kosa lake mkiwa ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako.

16 Kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili kusudi wawepo mashahidi wawili au watatu wa kuthi bitisha jambo hilo.

17 Akikataa kuwasikiliza, liambie kanisa. Kama akikataa kulisikiliza kanisa, basi mhesabu yeye kama ni mpagani au mtoza ushuru.
 
Wajinga nyie

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Amefurahi kujiaibisha. Wewe unaumia nini? Tulia dawa iwaingie
 
Kuna maana gani kumdhalilisha mtu na kukimbilia kwa viongozi wa dini? Kumsamehe au kutomsamehe ni utashi wake Membe. Na tusisahau Musiba alivyomdhalilisha huyu mzee. Na laiti Magu angekuwepo sijui Membe angekuwa na hali gani muda huu? Yote kwa yote Membe alipwe fidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…