Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Wakati dalali wa Mahakama kampuni ya Yono (vijana wa kazi) ikihesabu siku zilizobaki katika 14 (siku za kazi) alizolewa mtukanaji Cyprian Majura Musiba kumlipa fidia Kachero Bernard Membe jumla ya shilingi 9.2 Bilioni, Bwana Musiba amewaangukia viongozi wa dini Askofu Alex Malasusa (KKKT Diyosisi ya Pwani) na Kardinali Porlycarp Pengo kumwombea msamaha kwa Membe asipige mnada mali zake.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Membe nyumbani kwake Mikocheni zinaeleza kwamba Jumatatu ya tarehe 24/4/2023 majira ya saa 10 alasiri mjumbe kutoka kwa Pengo alifika kwa Membe kumpa ujumbe wa Pengo kumsihi amsamehe Musiba.

"Alikuja hapa padre wa moja ya makanisa yetu kuleta ujumbe huo lakini naona Mzee alimkatalia na kumwambia 'namheshimu sana baba Askofu Pengo lakini kwenye hili anisamehe yeye (Pengo) huyu kijana lazima alipe gharama ya matusi yake' " anasema mwanafamilia aliyetajwa kwa jina la Colleta na kuongeza:

"Lakini jioni yake ya saa moja Askofu Malasusa naye alimpigia simu Mzee kuongelea suala hilo hilo lakini naye Mzee alimpa majibu yale yale aliyompa mjumbe wa Pengo." Hata hivyo kwa maelezo ya Colleta ni kwamba si tu ni msimamo wa Mwanadiplomasia huyo Bali ni msimamo pia wa familia.

Hii inakuja baada ya jitihada za Askofu Mwamakula pia kugonga mwamba baada ya kumwandikia barua Membe ya msamaha kwa Musiba.

Wakati hayo yakijiri hapa Mikocheni, tayari kampuni ya Yono imeshatua jijini Dodoma itakapoanzia kazi ya mnada kwa kuanza na apartments za Musiba zilizoko Ihumwa, nyumba yake ya Chamwino, guest house yake ya Msalato na shamba la hekari 10 njia ya Singida.

Baada ya hapo Yono atatimba apartment ya Kigamboni, shamba la hekari 5 Bagamoyo kabla ya kugeukia mitambo yake ya uchapaji iliyoko jengo la Exim ghorofa ya 8 jirani na Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba huko nyuma Musiba alichapa magazeti yake kampuni ya Malindi Printing huko Mbweni ambayo ni mali ya TISS. Jambo hili lilileta ukakasi wa kisheria kwani sheria ya vyombo vya habari (2016) inamtaka mlalamikaji kumshitaki Mwandishi, mhariri, mchapaji na msambazaji. Kwa mantiki hiyo DG wa TISS angetakiwa kusimama kortini. Ili kuokoa jahazi Musiba "alinunuliwa" mitambo mingine Mpya kutoka Ujerumani na kwa "huruma" mwana TISS Membe aliridhia. Nayo itanadiwa baada ya siku 14 kutamatika pamoja na nyumba na mashamba yake ya kijijini nakadhalika.

My take: Vijana tujifunze kitu katika sakata hili la Musiba na Membe kwamba tuwe na akiba ya maneno. Lakini pia akili ya kupewa changanya na zako. Waliokuwa wakimpa akili karibia wote wamemkimbia tena ndio wamekuwa jirani na Membe. Amtegemeae mwanadamu mwisho huwa kama hivi. Musiba kwishney!
Namuombea kila baya Musiba.
Ahenyeshwe na ikibidi hata yeye mwenyewe apigwe mnada
 
Lakini ni vyema Musiba asitake kuuzunguka mbuyu, atoke hadharani tu na kumuomba msamaha Membe na wengine wote aliowakosea, tena kwa namna ile aliyoifanya kupitia vyombo vyake vya habari.
Naunga mkono hoja.
 
Kama alitegemea kutoboa kupitia hiyo njia Naona atakwama tu huyo musiba hana kitu.

Kufulia uzeeni kubaya sana kunamfanya mtu afanye mambo ya kumshushia hadhi kabisa.

Sasa kweli waziri wa mambo ya nje mstaafu ni mtu wa kungangania kuuza mali za Musiba??

Anajiabisha kuliko hata vile anavyodai kuaibishwa na musiba.


Unajitisha , wauze Mpaka Kuku wake iwe fundisho kwa wengine
 
Mkuu

Kitengo cha propaganda. Hicho mkuu!!

Kina kazi maalum !!

NADHANI. TISS watatafuta namna ya kumsaidia!kuna picha itachezwa tu halafu itamuokoa musiba kwenye hio ishu!!!

Kama alitumika bas ni KWA manufaa ya umma yasiyooonekana tena yenye faida KWA Membe!! Yeye mwenyewe tena kwa kazi yake ya kikachero!!!
Yaani wewe akili yako bana... yaani TISS wamsaidie Musiba halaf wamtelekeze mwenzao Membe?!
 
Ku-deal na mtu kariba ya Membe ujipange hasa. Huyu ni jasusi si wa kitoto. Ni diplomat maarufu sana huko duniani. Bila Membe Jakaya asingepata Urais na hata baada ya kupata Kuna baadhi ya viongozi duniani asingewafikia. Huyo ni mwandamizi wa Jesuits mbali na kuwa Mwalimu wa ukachero wa M16 ya Uingereza. Niishie hapo maana kwanza ujue Membe anawakilisha wangapi kwenye kesi hiyo?
Sasa Jasusi mkubwa analilia malipo kutoka kwa kapuku Musiba!
 
Hahaaa..... wapambe mmeshindwa kumchangua shujaa wenu msiba?

Yuko mwingine alisingizia watu madawa ya kulevya.

Kesi zake zitafunguliwa hata baada ya miak 30 mbele. Ajiandae tu.
Yule DAB ni zaidi ya sheitwan yupo kitaa anatingisha msambwanda
 
Kuna watu wanalalamika wana maisha magumu na hawana raha kwa vitu vya kipumbavu, pata picha upo kwenye kiatu cha Musiba
 
Back
Top Bottom