Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Ninachokiona ni Membe kupewa sifa ambazo hana. Hata hivyo sishangai kwa sababu wapinzani wa Rais Magufuli wana ombwe la mtu ambaye atapambana naye katika kiti cha Urais.

Kinachofanyika kwa sasa ni kumshabikia mtu yeyote anayesema au kuonekana atapambana na Rais Magufuli hata kama hana sifa ili tu kujaza ombwe.
 
Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
Ni ajabu sana kuwa Wanaopiga kelele kusifia kuwa awamu ya tano haina mfano kwa jinsi inavyo Fanya vizuri katika uongozi ndio haohao wenye hofu kubwa ya uchaguzi kwa nini?
Kama umeongoza vyema una haja gani kuwa na wasiwasi na kutumia hila kutaka ubaki madarakani?
Mbona ulipaswa kukaa kimya kisha matendo yako ndio yakakubeba?
Na hofu kubwa mbona iko kwenye uteuzi ambao wapigakura ndani ya chama ni wastani wa 3,000 tuu na huku kwenye wapiga kura zaidi ya 15M hawaogopi sana?
Au kwa vile ndani ya Chama hawawezi kuiba kura kuliko uchaguzi mkuu?
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
Kamfukuze...
 
Mnaogopa nini hadi kufukuza wanaotaka kugombea? Katiba yenu haina kugombea?
 
Ninachokiona ni Membe kupewa sifa ambazo hana. Hata hivyo sishangai kwa sababu wapinzani wa Rais Magufuli wana ombwe la mtu ambaye atapambana naye katika kiti cha Urais.

Kinachofanyika kwa sasa ni kumshabikia mtu yeyote anayesema au kuonekana atapambana na Rais Magufuli hata kama hana sifa ili tu kujaza ombwe.

Kumbuka 2015 waligombea wangapi kwa tiketi ya CCM?
 
Ninachokiona ni Membe kupewa sifa ambazo hana. Hata hivyo sishangai kwa sababu wapinzani wa Rais Magufuli wana ombwe la mtu ambaye atapambana naye katika kiti cha Urais.

Kinachofanyika kwa sasa ni kumshabikia mtu yeyote anayesema au kuonekana atapambana na Rais Magufuli hata kama hana sifa ili tu kujaza ombwe.
Kwa nini hamtaki Magufuli "mtu maarufu sana" apambanishwe na asiye maarufu?
 
Napendekeza Jiwe akabadili katiba haraka bungeni aweke kipengele kuwa mtu haruhusiwi kuwania urais kama siyo Rais wa nchi.. Jiwe fanya chap chap jembe langu maana nakuaminia kwa kupendekeza sheria za matango pori.
Na itapita kwa kishindo cha Ndiyooo
 
Back
Top Bottom