Niimeamini TISS wanatumia akili za hali yajuu sana. Ukiangalia huu uzi utadhani umeletwa kama taarifa ya kuonyesha "daring spirit" ya bwana Membe lakini ni uzi wa "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya"
Kwa uzi huu inaonyesha huku JF kuna waajiriwa wengi wa "kitengo" na wanachofanya ni kum expose Membe hata kwa kumsingizia ili kwanza kumtisha yeye mwenyewe lakini pia waungaji mkono wa awamu ya tano wapate muda wa kutosha wa kupanga namna ya kumshughulikia
Hivi ikifanyika move ya kumvua Bernard uanachama kabda hata ya kipindi cha kuchukua form za ugombea ndani ya chama nini tena anaweza kufanya?
Kwenye bandiko hili kuna akili ya ki TISS. Kwa mfano, ukitaka watu wautukane usabato au uislamu au ukatoliki wee andika uzi kuusifia humu ndani ambapo wàtatokeza wa kukuunga mkono lakini watakuwepo wengi wa kutukana, kuchambua, kuonyesha madhaifu ya imani husika na utajua misimamo, hisia na akili za watu kuhusiana na jambo hilo