Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Muacheni Membe apate tumaini la Kuishi.

Maumivu aliyo nayo ni makali sana. Anajua hadi 2025 upepo utakuwa umebadilika kabisa na hakuna mtanzania atamkumbuka maana enzi hizo vijana watataka watu wanaofahamu uchapa kazi wao. 2025 wapiga kura wa Membe wengi watakuwa wazee.

Akiwa anajua 2020 hawezi fanya lolote ndani ya ccm, kwa sasa anajaribu kuchonganisha Rais na Mwenyekiti wa ccm na wana ccm na wananchi kuonekana amefukuzwa ccm ili apate kura za huruma.

Naamini ccm wata mpuuza na kushughulika nae kimfumo ndani ya chama.

2020 hata akienda upinzani itakuwa too late.
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
Wacha upumbavu
 
Ninachokiona ni Membe kupewa sifa ambazo hana. Hata hivyo sishangai kwa sababu wapinzani wa Rais Magufuli wana ombwe la mtu ambaye atapambana naye katika kiti cha Urais.

Kinachofanyika kwa sasa ni kumshabikia mtu yeyote anayesema au kuonekana atapambana na Rais Magufuli hata kama hana sifa ili tu kujaza ombwe.
Kwa nini mnatumia bunduki kujibu hoja?
 
Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.

"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.

Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.

Watu bhaaaaana ati uraisi,labda urahisi
 
Miundombinu inajengwa kwa kodi za wananchi na sio hisani au mshahara wa rais. Hivyo miundombinu itajengwa na yoyote hata kama nchi itakuwa haina rais kwani mipango ya nchi ipo tayari.
Aliyekuwepo huko nyuma alijenga miundo mbinu IPI?? Huyo hawezi kuwa rais hata kwa mtutu was bunduki!!
 
CCM Taifa ikiridhia kufanya ambacho haikuwa Utamaduni wake huenda likawa jaribio la bei ghali lenye kutikisa mizizi yake ya asili. Hivyo kwa wanaokitegemea chama watajua si kipindi kizuri kugusa mizizi, kwani kiangazi kimeshaanza. Je wako tayari kufanya hivo ili mtu anayeotea zaidi apate?
Jibu jepesi lenye maslahi kwa familia za wenye chama itakuwa ni bora kuuza tena kwa bei ya 5years.
 
Ni haki yake kikatiba kuna tatizo gani akiitumia? Maadam JPM anafanya kazi natumai kazi zake zitakuwa kigezo cha yeye kuchaguliwa tena ndani ya chama hivyo natamani kuona uchaguzi huru na haki ndani ya chama atakayeshinda ashinde!
Pia utarajie watanzania wenzako kadha wakadha watakao kuwa upande wa Membe watapoteza maisha, Magu anamiliki wasio julikana!.
 
Kwa nini hamtaki Magufuli "mtu maarufu sana" apambanishwe na asiye maarufu?
Duh!
JF ya siku hizi hata kujibu comment za wachangiaji inahitaji moyo sana!

Wewe kwa uzoefu wako hapa ulipaswa angalau ujitofautishe na kundi la instagram lililovamia JF lakini umeshindwa!

Samahani kama nimekukwaza!
 
Huyu wa sasa hawezi kubadilika
Membe kuwa Rais!! Hapana kwa kweli. Heri ya Magufuli wetu. Tumwombee Magu,aache hofu ajiamini;awe na hekima na busara,aache kiburi.
 
Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
hahahahaha jomba unezungumza nini..hivi wewe hapo ulipo.unahitaji uhuru gani labda utujuze..hii ya kuandika msg bila kuhojiwa nayo pia ni uhuru tosha kabisa..au unahitaji uhuru wa kuoa wanawake wengi bila kuulizwa..sielewi uhuru upi unaouzungumzia zaidi ya uhuru wa nchi wa mwaka 1961
 
Niimeamini TISS wanatumia akili za hali yajuu sana. Ukiangalia huu uzi utadhani umeletwa kama taarifa ya kuonyesha "daring spirit" ya bwana Membe lakini ni uzi wa "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya"

Kwa uzi huu inaonyesha huku JF kuna waajiriwa wengi wa "kitengo" na wanachofanya ni kum expose Membe hata kwa kumsingizia ili kwanza kumtisha yeye mwenyewe lakini pia waungaji mkono wa awamu ya tano wapate muda wa kutosha wa kupanga namna ya kumshughulikia

Hivi ikifanyika move ya kumvua Bernard uanachama kabda hata ya kipindi cha kuchukua form za ugombea ndani ya chama nini tena anaweza kufanya?

Kwenye bandiko hili kuna akili ya ki TISS. Kwa mfano, ukitaka watu wautukane usabato au uislamu au ukatoliki wee andika uzi kuusifia humu ndani ambapo wàtatokeza wa kukuunga mkono lakini watakuwepo wengi wa kutukana, kuchambua, kuonyesha madhaifu ya imani husika na utajua misimamo, hisia na akili za watu kuhusiana na jambo hilo
 
Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
Tindo una maoni mazuri,una hoja fikirishi
 
Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.

"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.

Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.

Its on!

Jiwe’s shitting on himself now!
 
Back
Top Bottom