Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Niimeamini TISS wanatumia akili za hali yajuu sana. Ukiangalia huu uzi utadhani umeletwa kama taarifa ya kuonyesha "daring spirit" ya bwana Membe lakini ni uzi wa "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya"

Kwa uzi huu inaonyesha huku JF kuna waajiriwa wengi wa "kitengo" na wanachofanya ni kum expose Membe hata kwa kumsingizia ili kwanza kumtisha yeye mwenyewe lakini pia waungaji mkono wa awamu ya tano wapate muda wa kutosha wa kupanga namna ya kumshughulikia

Hivi ikifanyika move ya kumvua Bernard uanachama kabda hata ya kipindi cha kuchukua form za ugombea ndani ya chama nini tena anaweza kufanya?

Kwenye bandiko hili kuna akili ya ki TISS. Kwa mfano, ukitaka watu wautukane usabato au uislamu au ukatoliki wee andika uzi kuusifia humu ndani ambapo wàtatokeza wa kukuunga mkono lakini watakuwepo wengi wa kutukana, kuchambua, kuonyesha madhaifu ya imani husika na utajua misimamo, hisia na akili za watu kuhusiana na jambo hilo
hakuna kitu hapo labda wewe ndiyo TISS
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
Nyie si mnasema kila siku kuwa Jiwe anakubalika ,sasa atajuaje kuwa anakubalika sasa si ashindane na membe aonekane anavyokubalika ,mbona anaogopa hivyo ushindani .Halafu upinzani ndani ya chama sio uhaini ,tatizo la Jiwe wenu hajui siasa yeye ni ubabe ,matokea yake hana sapoti kabisa ndani ya chama labda wachumia tumbo kina Bashiru ,polepole ,musukuma ,lusinde ambao ni empty head ,membe akigombea Jiwe byebye .
 
Wagombanapo mafahali wawili ziumiazo ni nyasi, kicheeeko wasimamizi wa uchaguzi huyo Musiba na Makonda naona watu wakishinda kwa 100%
 
Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
Jamani wakati wa Kikwete si mlitaka rais dikteta? Hivi nyie watu mnataka nini hasa
 
Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.

"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.

Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.

Hongera Bernard Membe. Hata hivyo kwa kuwa najua ukipata Urais tutapata taabu zaidi kuliko wakati wo wote wa Uhuru WA Taifa letu siku ukichukua fomu nami pia nitachukua kwa sababu najua wazi kuwa naweza kuwa Kiongozi bora kuliko wewe. Tunavyokujua ulivyo na visasi visivyoisha!! Pisha ibilisi wewe
 
Ninachokiona ni Membe kupewa sifa ambazo hana. Hata hivyo sishangai kwa sababu wapinzani wa Rais Magufuli wana ombwe la mtu ambaye atapambana naye katika kiti cha Urais.

Kinachofanyika kwa sasa ni kumshabikia mtu yeyote anayesema au kuonekana atapambana na Rais Magufuli hata kama hana sifa ili tu kujaza ombwe.
Screenshot_2019-08-04_085110.jpg
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
Screenshot_2019-08-04_085110.jpg
 
Aliyekuwepo huko nyuma alijenga miundo mbinu IPI?? Huyo hawezi kuwa rais hata kwa mtutu was bunduki!!

Sio aliyekuwepo, sema waliokuwepo kuanzia wakoloni, kila mmoja aliweka miundo mbinu kulingana na mipango yake, labda kama hujui unaloongea.
 
Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.

"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.

Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.

Hahahaha yaani hakuna anayeongelea kina Mbowe, yaani ni CCM tu. 2020 twende na Magufuli ndiyo mpango mzima!
 
Matumbo yangu yote yamepata joto la ghafla... na amesema atashinda! !!!!!!! Oh my gosh
🤣🤣🤣🤣🤣😅😅😅😅😅 njaaaaaaaaaa hizi, hana uwezo wa kushinda labda asubirie chakula chake kiishe tumboni
 
Back
Top Bottom