Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe amesema wao wamepata wadhamini katika mikoa kumi.

Amesema ACT-Wazalenda waliamua kutafuta wadhamini kimyakimya ili kuepuka kuteleza.

Majina wa wateule wa kugombea Urais yanatarajia kutolewa na Tume ya Uchaguzi, NEC Agosti 25, na kampeni zitaanza Agosti 26

Chanzo: ITV
 
Wasalaam wana jamvi!

Mgombea wa ACT Wazalendo jana alikwenda mahakama kuuu kula kiapo kwa judge ... alipoulizwa na waandishi kuhusu njia yake ya kutafuta wadhamini aliweka wazi kabisa yeye alikuwa mtulivu kusoma kanuni na sheria hivyo ndio maana alitumia njia ya kutafuta wadhamini kimya kimya ili asivunje kanuni alizo zisoma na kuzielewa!

Alisema wazi kabisa hakutaka kuingia kwenye mtego wa kuanza kampeni kabla ya muda maana muda ya kujinadi bado haujafika mpaka hapo watakapo vuka kiunzi cha kuteuliwa na tume!

Ni wazi kuna mtu hapa alikuwa ana kumbushwa na kutumiwa salamu!

Wape salaaam.

Mswahilikavaasuti
 
Kwa hiyo Chadema waliotafuta wadhamini hadharani wameteleza.?

Kwa hii kauli haoni kama anawasaidia CCM na Tume ya Uchaguzi kufanya fitina.

Upepo wa Lissu unamtesa Sana huyu Membe kuliko nguvu ya CCM.

CCM inapenda watu waoga waoga kama Membe ili ipate kuwaburuza.

Halafu yeye Membe alivyoenda Zanzibar Yale maandamano na zile ahadi jukwaani alikuwa anafanya nini.

Inawezekana Membe ndio mchawi wa Lissu kuliko hata CCM wenyewe.
 
Wasalaam wana jamvi!

Mgombea wa ACT Wazalendo jana alikwenda mahakama kuuu kula kiapo kwa judge ... alipoulizwa na waandishi kuhusu njia yake ya kutafuta wadhamini aliweka wazi kabisa yeye alikuwa mtulivu kusoma kanuni na sheria hivyo ndio maana alitumia njia ya kutafuta wadhamini kimya kimya ili asivunje kanuni alizo zisoma na kuzielewa!

Alisema wazi kabisa hakutaka kuingia kwenye mtego wa kuanza kampeni kabla ya muda maana muda ya kujinadi bado haujafika mpaka hapo watakapo vuka kiunzi cha kuteuliwa na tume!

Ni wazi kuna mtu hapa alikuwa ana kumbushwa na kutumiwa salamu!

Wape salaaam....

Mswahilikavaasuti
 
Kule Zanzibar siyo kampeni. Kufanya mara mbili na aliyefanya zaidi wote kundi moja. Alishindwa kutambua hilo mapema na bora angeendelea tu. Hata Magufuli pale Chimwaga ni sawa na alifanya kampeni siku zote ingawa naye alifanya mara moja. Watu wasiojielewa wanaishi kwa tabu sana.
 
CCM naona sasa pumzi imewakata mnatafuta visingizio vya kitoto, nyie siku zote si mlikuwa mnajiamini na bombardier zenu mlizonunua? sasa twendeni uwanjani tukapige "game" acheni kulialia.
 
Kama ni kampeni basi kampeni huanza mara tu uchaguzi mmoja unapokamilika kwani wanasiasa kuahidi jambo fulani kwa wananchi huwa ni kitu kinachofanyika wakati wote wa miaka mitano.

Kwa kifupi, ndani ya miaka mitano huwa ni kipindi cha kampeni kisicho rasimi na hakuna kosa kisheria kufanya kampen zisizo raisimi
 
Membe keshaliwa
117803191_3129758130480435_9214425804489478799_o.jpg
 
Lissu ni mkongwe wa sheria ni wazi hajakurupuka,anajua alifanyalo,wajichanganye kumuengua uchaguzi UTASIMAMA.
Ni kweli. Nimemsikia Mkurugenzi wa NEC alipokuwa akihojiwa na Dr. Ryoba wa TBC akijibu swali hilo. Kuwa hadi sasa Tume haijateua mgombea yeyote,hivyo haina mgombea. Hadi itakapoteua tarehe 25.08.2020, ndo itakuwa na meno ya kushughulikia mtu. So, hata CCM wanapiga kampeni kidizaini kwa matamasha ya muziki, TVs, makongamano ya dini nk. Nafikiri kama ni kweli, sisi ccm ndo tumetangulia kuvunja,japo NEC haina meno kwa sasa.
 
Back
Top Bottom