Membe: Nasubiri kwa hamu barua ya wito CCM. Hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa

Huyu Membe anajiona ana nguvu sana ndani ya ccm wakati aliingia tano bora akagaragazwa vibaya hadi na January Makamba tu..

Kama anajiamini aje chadema achukue fomu.

Sent using Jamii Forums mobile app
ningeshangaa kama usingeandika ujinga wako. na kuunganisha na chadema. mnajidai mnademokrasia wakati mtu akitangaza nia tu mnamhukumu? huyo musiba kawatukana na kuwazalilisha watu hajawahi kuitw ahata kwa mjumbee
 
f76fe03d31b910db4b075bb0a6541376

Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
WAZIRI wa zamani wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa nchini Tanzania, Benard Membe amesema, anasubiri kwa hamu, barua ya wito ya kumtaka kufika kwenye Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Anasema, “kutokana na wingi wa meseji, nashindwa kumjibu kila mtu aliyeniandikia ujumbe kuhusu tangazo la kuitwa kwangu. Niseme tu kwamba, nasubiri kwa hamu barua ya wito.”

Katika taarifa yake ya kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, tarehe 13 Desemba 2019 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, CCM kimeeeleza kuwa viongozi wake watatu wandamizi, “watahojiwa” na kamati yake ya maadili na usalama.

Polepole amewataja viongozi wanaopaswa kuhojiwa na kamati hiyo, kuwa ni Membe, Kanal Abdulrahaman Kinana na Luteni Yusuf Makamba.

Kinana na Makamba, waliwahi kwa nyakati tofauti, kushikilia wadhifa wa ukatibu mkuu ndani ya chama hicho, huku Membe akiwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Alisema, viongozi hao wandamizi, wataitwa mbele ya kamati hiyo, kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili.
Membe, Kinana na Makamba, wamenukuliwa wakiutuhumu uongozi wa juu wa chama chao, kumkumbatia

Katika kinachoitwa, “kuvuja kwa mazungumzo yao waliyofanya kwa njia ya simu,” Membe, Makamba, Kinana, Nape Nnauye na January Makamba, kwa nyakati mbalimbali, walisikika wakimtuhumu Rais John Magufuli, kumkumbatia Cyprian Musiba, anayetukuna na kusingizia watu kadhaa mambo mbalimbali.

Kinana na Makamba, waliamua kufikisha malalamiko yao kwa Pius Msekwa, katibu wa kamati ya wazee ya chama hicho.

Katika barua yao kwa Msekwa, Makamba na Kinana wanasema, “vitendo vya Musiba, anayeonekana ametumwa na anayetumia mwamvuli wa CCM na Ikulu, kushambulia kila mtu, vinakidhalilisha chama chetu.”

Akiandika kwa kujiamini, kujibu madai hayo ya Polepole yanayomtaka kufika kwenye kamati ya maadili, Membe anasema, “…nasubiri kwa hamu sana barua ya wito. Nitakwenda; hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa.”

Jina la Membe – mwanadipromasia mashuhuri nchini aliyepata kuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka takribani nane ya utawala wa Jakaya Kikwete – limepata umaarufu mkubwa katika siku za karibuni, kufuatia kuhusishwa na mbio za urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 kupitia CC.

Hata hivyo, Membe mwenyewe hajaweka wazi jambo hilo, ingawa watu waliokaribu naye wanasema, “ni lazima atajitosa kwenye kinyanganyiro hicho.”
Mwanadiplomasia yeyote mbobevu ni lazima awe na ujasiri mkubwa, vile ambavyo anafanya. Hivi ndiyo ambayo Mh. Membe siku zote alivyo, huyu mtu aliaminiwa na awamu zote nne zilizotangulia, aliaminiwa na Mw. Nyerere mwenyewe. Sijui awamu hii ina shida gani!

Badala ya kutumia vyema ushauri wa watu aina ya Mh. Membe, Makamba na Kinana yenyewe inatafuta tu fitna dhidi. Wasipoangalia na kuzicheza vyema kete zao, kwa hakika itakula kwao mazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Once upon a time there was a great politician in Tz namely Benard Membe, now lives in his remote village in Lindi region...
You just cant *** wth the system..that's the hym known to any intelligence agency worldwide and any retired TISS member should know this trick...
Politically, Membe is finished..
 
hivi kweli slowslow ,ndi wa kumuita kanali mstaafu kinana,luteni mstaafu makamba na kachero benard membe,da kweli dunia ina mambo hasa tanzania,nakumbuka wakati meja jenerali mstaafu marehemu muhidini mfaume kimario alipotaka kufikishwa mahakamani na aliekuwa spika wa bunge kipindi hicho,pius msekwa,
mabaka mabaka walisema nini kwa msekwa,muulizeni atawaambia.
 
Wanaend

WANAITWA ILI WAOMBWR MSAMAHA KWA MAKOSA WALIYOTE DEWA NA KUVUNJIWA HESHIMA
 
Nasikia Kolimba aliitwa pia. Baada ya hapo kilichomtokea wote tunakijua. Membe inatakiwa ufuate maadili ya Chama chako.
Ni kweli, Ma CCM haya yalimkolimba Horace mchana kweupe. So Bro. Bernard take care. Hayo makamati ni ya kimafia na yamejaa watu wenye roho chafu. Japo hoja unayo ya kwa nini Mwenyekiti na watu wake wanaingilia kwa udukuzi mazungumzo ya watu kinyume cha sheria!!!?
 
Niguse .............
safari hii anaguswa na mpaka anuke na atueleze moshi wa zwani na vimondo vya uvira atueleze kwa nini anawafungia vijana kwenye appartment kumuujumu jiwe kwenye mmitandao atueleze kule zimbabwe aliwepeleka kuwafunza nje ya system .... mh raisi mfukuze kazi yule dc wa iringa ....... na pangani na nkasi ...... na mkuu wa mkoa wa mara
 
Hawana la kumfanya zaidi ya kufurahishana tu kwenye vikao vyao

Back
Top Bottom