Membe: Nasubiri kwa hamu barua ya wito CCM. Hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa

Labda Maembe ila kama ni Membe hapana ccm wote wezi hakuna mwenye moral authority aanze kwanza yule aliyehonga nyumba ya umma kwa hawara.
lazima anuke na atueleze zile appartment za vijana wake kule dom na dar...... na usajili anaofanya vyuo vikuu .........
 
Kanali Kinana na Luteni Makamba......Once a Soldier, always one. CC ya CCM wawe makini sana. Afterall Kinana anajua siri zote za uporaji wa kura waliofanya 2015. Hicho kikao kitakuwa cha kishkaji tuu. Watagonga zao mvinyo na kutoka na matamko yasiyo na kichwa wala miguu
 
Siasa za CCM kweli ni za hali ya juu sana. Fikiri:
Membe ameitwa CC na hao hao ndo watakao ijadili fomu yake kama atachukua fomu kuomba agombee. Sasa, anasema ati; Hoja zitatolewa na hoja zitatatuliwa.
Hoja zipi?? Sisi CC tumeshasema; Hatuyumbishwi bali tutaendelea na ule utamaduni wetu wa mgombea kupewa vippindi viwili. Wewe Mbembe, utaipitishia wapi hiyo fomu yako?? Haya, si weye Mbembe tu, hata na mwengine aje atuletee hizo hela za kununua fomu tufanyie shughuli ya kampeni. Njooni 42 tena ka 2015. CC tumeamua ni huyo huyo hadi 2025.
Acheni kuwaghilibu waTZ na maneno yenu ya kanga. Hapo hakuna cha Membe wala mbembe. Huyo aliyeko ndiye tu
 
Atatoka akiwa mdogo tu
Kinachofanyika ni kumpa haki ya kujitetea tu bada ya hapo ni kumtimulia mbali
 
Watu wanaongea kana kwamba system ikitaka kukuondoa inashindwa.
Unaondolewa dakika moja tu, ukiona system haikuondoi inakutumia na huenda hata wewe unatumika na unajua au hujui ila Watu wa nnje wanaweza wasijue.
Na inawezekana unaonekana huna madhara Umemalizwa unawekwa kama mfano watu watakua wakikuangalia wanajua nguvu waliyonayo Watu wa system wanakaa kimya wasije kuwa kama wewe.
Mtu aliyekua tishio CCM ni Lowasa tu Na kama alishindwa kuiua CCM basi CCM haiwezi kumpigia Magoti yeyote nchi hii.
Membe anaweza kupewa adhabu ya kutoshiriki masuala ya siasa ya CCM kwa mwaka mmoja, hapo atakua hana chakufanya au akaambiwa rudisha kadi yetu atakua pia hanachakufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi kabisa,wana uwezo wakumchukulia kila kitu anajiharibia sana
 
Haya mavyama hatari, ukimkosoa mwenyekiti tayari unaitwa kwenye vikao..
Si akheri yao wanaitwa kwenye vikao?
Walala hoi wanawekwa ndani na kufunguliwa mashtaka, na wanafungwa, wakisubiri 'msamaha' wa waliemkosoa kwa ujira wa kumpa sifa nyingi kwa huruma aliyowafanyia.
 
f76fe03d31b910db4b075bb0a6541376

Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
WAZIRI wa zamani wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa nchini Tanzania, Benard Membe amesema, anasubiri kwa hamu, barua ya wito ya kumtaka kufika kwenye Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Anasema, “kutokana na wingi wa meseji, nashindwa kumjibu kila mtu aliyeniandikia ujumbe kuhusu tangazo la kuitwa kwangu. Niseme tu kwamba, nasubiri kwa hamu barua ya wito.”

Katika taarifa yake ya kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, tarehe 13 Desemba 2019 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, CCM kimeeeleza kuwa viongozi wake watatu wandamizi, “watahojiwa” na kamati yake ya maadili na usalama.

Polepole amewataja viongozi wanaopaswa kuhojiwa na kamati hiyo, kuwa ni Membe, Kanal Abdulrahaman Kinana na Luteni Yusuf Makamba.

Kinana na Makamba, waliwahi kwa nyakati tofauti, kushikilia wadhifa wa ukatibu mkuu ndani ya chama hicho, huku Membe akiwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Alisema, viongozi hao wandamizi, wataitwa mbele ya kamati hiyo, kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili.
Membe, Kinana na Makamba, wamenukuliwa wakiutuhumu uongozi wa juu wa chama chao, kumkumbatia

Katika kinachoitwa, “kuvuja kwa mazungumzo yao waliyofanya kwa njia ya simu,” Membe, Makamba, Kinana, Nape Nnauye na January Makamba, kwa nyakati mbalimbali, walisikika wakimtuhumu Rais John Magufuli, kumkumbatia Cyprian Musiba, anayetukuna na kusingizia watu kadhaa mambo mbalimbali.

Kinana na Makamba, waliamua kufikisha malalamiko yao kwa Pius Msekwa, katibu wa kamati ya wazee ya chama hicho.

Katika barua yao kwa Msekwa, Makamba na Kinana wanasema, “vitendo vya Musiba, anayeonekana ametumwa na anayetumia mwamvuli wa CCM na Ikulu, kushambulia kila mtu, vinakidhalilisha chama chetu.”

Akiandika kwa kujiamini, kujibu madai hayo ya Polepole yanayomtaka kufika kwenye kamati ya maadili, Membe anasema, “…nasubiri kwa hamu sana barua ya wito. Nitakwenda; hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa.”

Jina la Membe – mwanadipromasia mashuhuri nchini aliyepata kuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka takribani nane ya utawala wa Jakaya Kikwete – limepata umaarufu mkubwa katika siku za karibuni, kufuatia kuhusishwa na mbio za urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 kupitia CC.

Hata hivyo, Membe mwenyewe hajaweka wazi jambo hilo, ingawa watu waliokaribu naye wanasema, “ni lazima atajitosa kwenye kinyanganyiro hicho.”

Katika mambo ambayo sita

Kuna mambo ambayo siwezi kuyasahau na miongoni mwa hayo ni kile kilichotokea kwenye ukumbi wa White house pale Dodoma wakati Kamati Kuu ya CCM ikimhoji aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba , miaka kadhaa iliyopita...Kolimba naye ''akiwa nje' alionekana kama anatamba lakini siku ile ya kuhojiwa ilikuwa ni tofauti....Mungu amlaze mahali pema peponi....
 
Back
Top Bottom