Membe: Nasubiri kwa hamu barua ya wito CCM. Hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa

Membe: Nasubiri kwa hamu barua ya wito CCM. Hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa

NDUGU YANGU MEMBE!!!wakati unasubiri barua kumbuka kuna Polonium,novichok!!!kuwa makini huko ulipo!!!pia wakati unaenda dodoma utatumia usafiri gani?pia uwe makini na kiti utakachopewa wakati unahojiwa je maiki,kalamu,mionzi!!!vaa kabisa bulleti proof!!!kama utatumia gari mkumbuke sokoine,kolimba, na wengine!!!pia wakati unaenda uwaage wanao,ndugu,jamaa na marafiki kwasababu unamwendea chatu halafu huna hata kisu cha kumuulia!!!!
 
f76fe03d31b910db4b075bb0a6541376

Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
WAZIRI wa zamani wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa nchini Tanzania, Benard Membe amesema, anasubiri kwa hamu, barua ya wito ya kumtaka kufika kwenye Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Anasema, “kutokana na wingi wa meseji, nashindwa kumjibu kila mtu aliyeniandikia ujumbe kuhusu tangazo la kuitwa kwangu. Niseme tu kwamba, nasubiri kwa hamu barua ya wito.”

Katika taarifa yake ya kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, tarehe 13 Desemba 2019 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, CCM kimeeeleza kuwa viongozi wake watatu wandamizi, “watahojiwa” na kamati yake ya maadili na usalama.

Polepole amewataja viongozi wanaopaswa kuhojiwa na kamati hiyo, kuwa ni Membe, Kanal Abdulrahaman Kinana na Luteni Yusuf Makamba.

Kinana na Makamba, waliwahi kwa nyakati tofauti, kushikilia wadhifa wa ukatibu mkuu ndani ya chama hicho, huku Membe akiwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Alisema, viongozi hao wandamizi, wataitwa mbele ya kamati hiyo, kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili.
Membe, Kinana na Makamba, wamenukuliwa wakiutuhumu uongozi wa juu wa chama chao, kumkumbatia

Katika kinachoitwa, “kuvuja kwa mazungumzo yao waliyofanya kwa njia ya simu,” Membe, Makamba, Kinana, Nape Nnauye na January Makamba, kwa nyakati mbalimbali, walisikika wakimtuhumu Rais John Magufuli, kumkumbatia Cyprian Musiba, anayetukuna na kusingizia watu kadhaa mambo mbalimbali.

Kinana na Makamba, waliamua kufikisha malalamiko yao kwa Pius Msekwa, katibu wa kamati ya wazee ya chama hicho.

Katika barua yao kwa Msekwa, Makamba na Kinana wanasema, “vitendo vya Musiba, anayeonekana ametumwa na anayetumia mwamvuli wa CCM na Ikulu, kushambulia kila mtu, vinakidhalilisha chama chetu.”

Akiandika kwa kujiamini, kujibu madai hayo ya Polepole yanayomtaka kufika kwenye kamati ya maadili, Membe anasema, “…nasubiri kwa hamu sana barua ya wito. Nitakwenda; hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa.”

Jina la Membe – mwanadipromasia mashuhuri nchini aliyepata kuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka takribani nane ya utawala wa Jakaya Kikwete – limepata umaarufu mkubwa katika siku za karibuni, kufuatia kuhusishwa na mbio za urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 kupitia CC.

Hata hivyo, Membe mwenyewe hajaweka wazi jambo hilo, ingawa watu waliokaribu naye wanasema, “ni lazima atajitosa kwenye kinyanganyiro hicho.”
Niguse ninuke
 
NDUGU YANGU MEMBE!!!wakati unasubiri barua kumbuka kuna Polonium,novichok!!!kuwa makini huko ulipo!!!pia wakati unaenda dodoma utatumia usafiri gani?pia uwe makini na kiti utakachopewa wakati unahojiwa je maiki,kalamu,mionzi!!!vaa kabisa bulleti proof!!!kama utatumia gari mkumbuke sokoine,kolimba, na wengine!!!pia wakati unaenda uwaage wanao,ndugu,jamaa na marafiki kwasababu unamwendea chatu halafu huna hata kisu cha kumuulia!!!!
kumbuka alikuwa nani huyo huko miaka ya nyuma na alikuwa na nafasi ipi na kwenye taasisi gani yaani mamba unamfundisha kuogelea
 
Kanali Kinana na Luteni Makamba......Once a Soldier, always one. CC ya CCM wawe makini sana. Afterall Kinana anajua siri zote za uporaji wa kura waliofanya 2015. Hicho kikao kitakuwa cha kishkaji tuu. Watagonga zao mvinyo na kutoka na matamko yasiyo na kichwa wala miguu
na huo ndiyo ukweli kikao chenyewe eti anaongoza jiwe wanamchezea kinana hawa ana roho ya kisomali yule wanafikiri ni mlugagaluga
 
Nawashauri wassiende kikao hicho kwani kitawapaata cha kuwapata, watajutia wamewasahau kina kolimba
Hao siyo dagaa ndani ya chama,Ni sawa na sangara ndani ya ziwa Victoria.
Akitokea wa kutaka kuwameza taarifa wataipata mapeeema Sana na huwenda wakawapa mgongo au microphone na maji yao wasiyatumie.
 
Hao siyo dagaa ndani ya chama,Ni sawa na sangara ndani ya ziwa Victoria.
Akitokea wa kutaka kuwameza taarifa wataipata mapeeema Sana na huwenda wakawapa mgongo au microphone na maji yao wasiyatumie.
mkuu shida watu wanafikiri hao ni kama akina nape vile, halafu dunia ishabadilika na hao level zao jiwe hagusi mtu ka kinana yupo kwenye tasnia ya politiki kitambo sana huyo jiwe alikuwa zake tocha hukoo hana ramani.......na ndiyo maana haishi kumshukuru ben maana anajua alivyookotwa jalalani
 
Kinana +Makamba hao watu Ni hatari.
Si watu wakuvuliwa nguo ndani ya chama.
Madhara yao wakiamua M/kiti Hana kiti.
Ninakifahamu chama,asichezee wale wazee.
Hata Eddo Hilo analijua na pia anawaheshimu balaa ila ameamua kupga kimya.
Subiri ujionee movie,nahisi nyuma ya kachero Kuna kundi kubwa Sana la wazee na wengine watakuwa kwenye kale ka kamati ka nidhamu.
 
Nahisi h

Nahisi hata ule msamaha walienda kumpa faraja ya moyo tu ,Sina uhakika Kama ilotoka mioyoni mwao
 
Kinana +Makamba hao watu Ni hatari.
Si watu wakuvuliwa nguo ndani ya chama.
Madhara yao wakiamua M/kiti Hana kiti.
Ninakifahamu chama,asichezee wale wazee.
Hata Eddo Hilo analijua na pia anawaheshimu balaa ila ameamua kupga kimya.
Subiri ujionee movie,nahisi nyuma ya kachero Kuna kundi kubwa Sana la wazee na wengine watakuwa kwenye kale ka kamati ka nidhamu.
ccm hii ambayo bashiru na polepole wanabwekabweka kijibwa koko eti ndiyo itamtisha kinana.....
 
safari hii anaguswa na mpaka anuke na atueleze moshi wa zwani na vimondo vya uvira atueleze kwa nini anawafungia vijana kwenye appartment kumuujumu jiwe kwenye mmitandao atueleze kule zimbabwe aliwepeleka kuwafunza nje ya system .... mh raisi mfukuze kazi yule dc wa iringa ....... na pangani na nkasi ...... na mkuu wa mkoa wa mara
Mkuu wamefanyeje hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom