Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Kama bado ana ndoto..... Aanzishe movement ambayo akina Mbowe na Zitto imewashinda.
 
Hivi kweli Membe anaamini alikuwa tishio kwa JPM ndani ya CCM?

He can’t be serious.
Hilo pia linaweza angaliwa upande wa pili, je wamemuogopa wakimuacha humo ndani au au kufukuzwa kwake kutasaidia kulinda utamaduni uliowekwa maana impact ya kumuacha achallenge awamu ya pili ya JPM kutawaibua hata wenye mvuto zaidi Kama itakavyokua 2025. Binafsi naona kuna sababu 2;

° kumlinda mteule
° Kulinda utamaduni wa chama.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ndiyo sababu pekee.

Watafute wote waliomsumbua 2015 akigombea, wale front runners wote kawafukuza kwa kashfa.

Prof.Mwandosya, Prof.Muhongo, Mwigulu, January, na sasa Membe. Sijui atafuata nani lakini wote waliokuwa top 10 na top five kagalagaza katupa.

Hahahaha Eti yeye ndiye msafi, wakati kashfa zake hataki ziguswe, Meli kawapa wanajeshi, Nyumba za serikali hataki kusikia.
List ni ndefu.... Binti Makecela, Byarandu, January...... Naona wamebaki Kingwangalla na yule Mkulima tu. At least kwa sasa.
 
Kitu CCM mnajivika upofu ni kutojua tu..
Jinsi gani Watanzania wanahitaji mbadala wa hiyo dikteta uchwara..

Yani Membe akicheua tu... Tunalala nae.
Angecheua akiwa CCM hapo sawa. Ila nje ya CCM ni sawa na Nyoka bila Venom.
 
Ninaowakumbuka na walioumbuka kwa kuiasi CCM TOKA VYAMA VINGI VIANZE
1. KIGHOMA ALLY MALIMA (rip)
2. AUGUSTINO LYATONGA MREMA
3. EDWARD LOWASA
4. FREDRICK SUMAYE
5. KINGUNGE NGOMBALE MWIRU
Hawa wote walikuwa na nguvu kubwa kiuchumi na kisiasa kuliko Ben Membe waliondoka wakatukana CCM kwa nguvu zote lakini mpaka leo CCM ndiyo inayotawala Tanzania. Binafsi siioni kabisa impact ya huyu waziri wa zamani ni kama tone la maji baharini.
Tatizo watu wanajua siasa ni maneno ya jukwaani na mitandaoni ukiwa mwanasiasa mwenye nguvu lazima polosoo uwe nayo ya kutosha
Mfano lowasa polosoo ndo ilimfikisha hapo alipo na kuwa alikua ndani ya sistim kwenye chama na serikalini ilimfanya wengi wamfuate.Na Membe kama polosoo ya kutafunwa ipo sawa utapata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akagombee urais kupitia Chadema, akatimize hiyo ndoto yake. Makamanda tayari wameshajitayarisha kumpigia deki barabara.
Atagomea kupitia CCM imani,na siyo CCM maslahi waliomfukuza eti kwakuwa tu kasema atagombea urais.
 
Sioni tofauti ya Membe kuachia jimbo la Mtama, Emmanuel Nchimbi kuachia jimbo na Regina Lowassa baada ya uchaguzi CDM walipompa ubunge wa viti maalum alipowaambia hiyo nafasi anastahili mtu mwingine sio yeye. Kuna watu washashiba.

Kama ni uraisi huyo Lowassa wakati kama huu 2015 alishaanza na ziara rasmi za kuonyesha nia, alikuwa ni rich backers na wapambe kibao wa wazi kama Nchimbi wenye jukumu ku-mobilise support ya ndani tena hapo nafasi ilikuwa inaenda kuwa wazi maana raisi alikuwa anamaliza muda wake.

Sasa how on earth Membe ambae mpaka sasa udhani kama kuna jitihada zozote za kushawishi humo ndani angeweza msumbua Magu.

Kama ni mkakakati wa mtu mmoja basi ni sawa na upuuzi tu na kama ni mkakati wa wengi wako wapi watu wake na sidhani kama leo angekuwa anatimuliwa pekee.

Kuna watu washashiba Membe mwenyewe baada ya kustaafu anazungukia vogue toleo jipya kufukuzwa CCM ambayo aimlipi pension ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu tu.

The only motive behind this ni kwamba CCM is cooking something I don’t know what.
Wewe ndio kichwa! Ndio yale ya Chadema na EL huku kampeni meneja ni retired Spy Master! Inabidi uwe kichaa kidogo kusimama na wapinzani wetu! Bora hao CCM watawale hadi tutapokuwa tayari kufanya mabadiliko lakini si kizazi chetu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwani kuna ubaya gani?

Wanaosema kuna ubaya si nyie?

Membe na hata hao wengine wote mnaowadhalilisha, hata marais wastaafu, wakiwamo hata kina Sumaye, Lowassa, wote wanaojitambua na watakaojitambua wakati wowote wanakaribishwa katika jitihada za kuwaadabisha.

Makelele mnayopiga si kwa sababu ya buku 7.
 
Back
Top Bottom