Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Hatua ya CCM kumwondoa ndani ya chama hicho, Bernard Membe sasa inakumbusha hadithi ya orodha ndefu ya makada wengine waliowahi kukumbwa na kadhia kama hiyo.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1985 CCM iliwatimua Maalim Seif Sharif Hamad, Hamad Rashid Mohamed, Juma Duni Haji kwa tuhuma za kukihujumu chama hicho katika uchaguzi huo baada ya kutoridhika na uamuzi wa CCM kumpitisha Abdul Wakili, kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Makada hao wote baadaye walijiunga na chama cha upinzani cha CUF na kutikisa chaguzi kuu zote visiwani humo tangu mwaka 1995 baada ya kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Maalim Seif ameongoza harakati za upinzani akiwa na vigogo wenzake hao kupitia CUF kabla ya kuzuka kwa mgogoro wa kiuongozi ndani ya chama hicho ulichowalazimisha kukihama na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.

Mbali na vigogo hao, mwaka 2017 chama hicho kilimtimua aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba kwa kukihujumu chama katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Hata hivyo Sophia alirejeshwa ndani ya CCM baada ya kuomba msamaha na tangu wakati huo amekuwa kimya.

Pia chama hicho kiliwatimua wenyeviti wa mikoa mbalimbali akiwamo Ramadhan Madabida (Dar es Salaam), Jesca Msambatavangu (Iringa), Erasto Kwilasa (Shinyanga) na Christopher Sanya (Mara) na wajumbe wa NEC, Ali Sumaye, Mathias Manga (Arumeru).

Wengine waliong’olewa katika sekeseke hilo ni pamoja na wenyeviti wa chama wilaya Madenge (Kinondoni), Assa Simba (Ilala), Leiza (Longido), Saileli Mollel (Arusha Mjini) Omary Hawadhi (Gairo) wenyeviti wa wilaya za Muleba, Babati na Bunda.
 
Umewasahau wabunge saba was bunge letu la Kwanza miaka ya 60 wakiwemo akina choga, kibuga, anangisye na wengineo
 
Membe kamwe hawezi kuwa Rais wa nchi hii,mchezo walomfanyia Lowassa na yeye kafanyiwa. Yeye kakatwa jina kwa kufukuzwa kwenye chama. Magufuli ndo CCM kwa sasa.
Ile kukatwa kwa Lowassa kiliniuma kama vile nilikuwa na undugu na huyo mzee!
 
Watu wana mafaili yake. Aangalie asije akashtukia ana kesi ya money takatisha. Uchunguzi wa kesi utaendelea mpaka November.
Sidhani kama magu anaweza mfanyia membe zaga la money laundering, imo.

Sent using Rocket Propelled Grenade
 
Naona kwenye social media ndiyo anazungumziwa zaidi, lakini mitaani hana impact yoyote.

Wacha aende huko anakoenda kutimiza ndoto yake but this time noo. Tunaenda na Magufuli
 
Alipoulizwa ni nani aliyempa taarifa kuhusu kuwapo kwa mpango huo alisema: “Sikiliza, mimi nina watu wangu serikalini, nina watu ndani ya chama na nina watu ndani ya usalama”.

Hit direct to the Ntonku
 
The goal ni kupata fursa ya kugombea. Na fursa hiyo ipo kama anaitaka.
Utakaporudia tena kusoma utaelewa.
Hapana.

Goal si kupata fursa ya kugombea tu.

Sasa mtu kama mimi ambaye sioni chama chochote Tanzania kinachonifaa, utanilazimisha niingie chama nisichokipenda?

Na nikiingia chama nisichokioenda nikaomba kugombea urais wakakataa?

Huoni hapo kwamba ujinga wa kulazimisha vyama unaninyima haki yangu ya kikatiba ya kugimbea uongozi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe anajipanga kua rais wa milele. Subiri muone show, hii miaka mitano constitution itabadilishwa na jiwe atatumia watu wengine akijifanya hataki awamu ya tatu, watanzania walivyo majority vilaza watasifia, jiwe anajua watanzania wengi ni vilaza na anatumia hiyo nafasi vizuri kabisa kuwachezea akili, akishindwa anahitaji kusema tu “niombee, maendeleo hayana chama” washika dini wote watamuunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…