Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Watz bana,"wanaaminishwa eti nguli wa UKACHERO mstaafu anaweza kwenda nje ya mstari" na wanaamini, Tz ina vihoja.
Chomoka kwenye box, acha kusujudia watu kwani hapo kosa liko wapi?utumwa wa fikra na ukoloni mambo leo unatutesa
 
Alipoulizwa ni nani aliyempa taarifa kuhusu kuwapo kwa mpango huo alisema: “Sikiliza, mimi nina watu wangu serikalini, nina watu ndani ya chama na nina watu ndani ya usalama”.

Kama maneno hayo hapo juu kayatamka "kachero" aliyebobea, nimejikuta nawaza hivi: Kumbe tulivyokuwa tukiambiwa tukiwa wadogo kuwa Tanzania ni ya pili nyuma ya Islael kwenye masuala ya upelelezi yalikuwa ni "joke" na kumbe hawa wasiojulikana wanaweza kuwa ni miongoni mwa akina M**nm** maana "operations' zao huwa ni za kijinga sana!
 
Kama anaamini ndoto haifi basi hii ISHAKUFA!!

Huyo kwa sasa hata rafiki zake wanaogopa kuwasiliana na kuonana naye hadharani!
 
Membe kumbe hana busara kabisa ya kuwa rais wa nchi kama principle yake ya kutumikia watanzania ni kwa yeye kuwa raisi tu. Kuitumikia Tanzania siyo lazima uwe raisi; ukaishasikia mtu analilia kwenda Ikulu basi mtu huyo ni wa kuogopa kama Ukoma!

Kitu Membe anasahahu ni kuwa lineup ya CCM ya mwaka 2014 siyo iliyopo leo, wale wajumbe waliokuwa wanampa nguvu ndani ya CCM mwaka 2014 hawapo madarakani tena. Zaidi ya kudanganywa na akina Nape, Membe huyu hata akiogombea leo, ndani ya halmashauri kuu na Kamati kuu hapiti; amebaki nawafuasi wachache sana ambao hata wote wakipimpa kura zao hawezi kufikisha 25%. Kamati kuu iliyomfukuza ndiyo pia inayopitishajina la mgombea wa CCM; sasa kama imeweza kumfukuza ni kweli ingepitisha yeye na kumwacha mwenyekiti wao? Kutokuona fact hiyo ni upungufu mkubwa sana wa busara; jambo linalomkosesha sifa ya kuwa rais. Sana sana yeye anonekana kama anataka kuivuruga CCM kwa filosofi ya "tukose wote", jambo la kiwehu kabisa

Makamba alipiga mahesabu akaona ili apalilie unga wa mtoto wake akaamua kuwa yaishe kusudi aache mwanya wa Januari kijaribu tena mwaka 2025.
 
Kina jamaa anapenda masifa ya kupita bila kupingwa hiyo!! Sasa kuona amejitokeza wakumpinga roho imemuuma akaona amtimue na hakika atamsakama mbaya kabisa. Mimi namuunga mkono Membe na asilani siwezi kukubaliana namtu anayefanya maisha kuwa magumu yalojawa vitisho
 
Yeye na washabiki wake wamejiaminisha kuwa eti anaogopwa.

Anaogopwa kwa lipi hasa?

Kujipa tu umuhimu ambao hana.
Yaani bora wangemuacha achukue form ili wamnyime kura ingekuwa vizuri sana maana hapo kweli watanzania wangeamini CCM hamuogopi kabisa.
 
Membe huyu hata akiogombea leo, ndani ya halmashauri kuu na Kamati kuu hapiti; amebaki nawafuasi wachache sana ambao hata wote wakipimpa kura zao hawezi kufikisha 25%.
Sasa kama ni hivyo woga wote huu unatoka wapi? Kwa nini asiachwe ajaribu bahati yake na akishindwa, si basi? Kwa nini afukuzwe hadi uanachama?

Kamati kuu iliyomfukuza ndiyo pia inayopitishajina la mgombea wa CCM; sasa kama imeweza kumfukuza ni kweli ingepitisha yeye na kumwacha mwenyekiti wao?
Tetesi zinasema wajumbe wengi hawakubariki hatua hiyo ila kama kawaida ya awamu hii udikteta ulitumika. Je tetesi hizo zina ukweli?

Huo upinzani wa kweli uko wapi
Kama huo upinzani haupo, haya matumizi ya polisi dhidi ya wananchi wasiounga mkono juhudi za nini? Fikiria mpaka inafikia Mwenyekiti wa Chama, Mbunge na Kiongozi Mkuu wa Upinzani Bungeni anawekewa mikwara asiweze kukutana na wananchi waliomchagua, je hapo tueleweje? Tatizo lako Kimbunga siku zote ni kwamba unaamini unajua kumbe hujui kitu na watu kama wewe ni hatari sana kwa afya ya taifa.
 
..CCM wangemuacha tu agombee.

..asingeweza kumshinda Magufuli ktk kura za wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM.

..CCM ina tabia ya kutumia mabavu hata ktk masuala yasiyohitaji mabavu.
Yule jamaa anaogopa upinzani kuliko ebola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…