Hivi ndugu yangu umeshawi kupanda jukwaa hata moja huko vijijini na kujaribu kama sauti yako inatoka au mikwara tu ya cyberspace
🙂
Kama vyama vikubwa like CUF na CHADEMA vinapwaya unafikiri mgombea binafsi atatosha kwa local context ya siasa za Bongo?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Suala ninaloongelea si kutosha au kutotosha.
Suala ninaloongelea ni mtu kupata haki yake ya msingi ya kikatiba.
Kuna mahojiano fulani Nyerere alifanya mwaka 1959 na Mama Eleanor Roosevelt New York, akaulizwa, hivi nyie Watanganyika mnadai uhuru, mko tayari kujiongoza wenyewe mkipewa uhuru?
Nyerere akajibu, akalishangaa lile swali.
Akasema sisi tulikuwa tunajitawala kabla wazungu hamjaja, tutashindwaje kujitawala?
Na hata tukishindwa, tuachieni tushindwe wenyewe.
Umenikuta mtu nina jacket langu mwenyewe, umelichukua, nalidai, unaniambia hili jacket halikutoshi, kama linanitosha au halinitoshi hiyo si hoja.
Hoja ni kwamba hili ni jacket langu, niachie mwenyewe.
Kama watu wataweza kushinda au hawawezi hiyo si hoja.Hoja ni kwamba watu wana haki ya kikatiba ya kuwa na ugombea binafsi, na wananyimwa haki hiyo ya kikatiba.
Kipindi kilirekodiwa na kipo Youtube