TANZIA Member deo paul55 wa JamiiForums afariki dunia

TANZIA Member deo paul55 wa JamiiForums afariki dunia

fullcup

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
809
Reaction score
2,204
Huyu ni moja ya member tuliyekuwa naye humu kwa muda mrefu. Ni moja ya watu walionifanya niijue JF miaka ya 2013 huko ingawa yeye alichelewa kidogo kujiunga. Na kwa Mara ya mwisho kuonekana humu ni 28/11/2020

Anaitwa Deogratius Paul (30) mkazi wa Madibira Mbarali Mbeya, amefariki usiku wa kuamkia tarehe 08/12/2020 katika Hospitali ya Irembula kwa matatizo ya tumbo.

Kwa miaka mingi alikuwa anasumbuliwa na miguu kufa ganzi kitu kilichofanya ashinde home tu akichat kwenye mitandao ya kijamii. Baadae alipona miguu na ingawa hakuwa full recovered.

Tar 3/12/2020 alipelekwa Sanitarium moja baada ya kuona mwili unakosa nguvu, huko aliambiwa ana kisukari akapewa dawa lakini hali ikawa mbaya akakimbizwa Ilembula. Baada ya vipimo ikabainika utumbo umejifunga na anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka.

Wakati wanaanza mchakato yakatokea ya kutokea. Alifariki usiku wa saa saba na nusu usiku wa tar 8/22/2020

Amezikwa Leo Tarehe 09/12/2020 katika makaburi ya kanisa Catholic Mahango - Madibira.


R. I. P deo paul555

Baadhi ya michango ya wadau




 
Back
Top Bottom