Member wa JF huwa mnajificha wapi mnapo tumia JamiiForums.!??

Me nipo Cambodia ss nani atajua?Ila nilikuja huko kwa sizonje kuna siku nilimwotea mmoja akifungua jf
 
Kuna siku nipo brela nasubiri huduma kulikuwa na jamaa anacheka tu kila akisoma kitu kwenye simu yake (huku anakagua kagua fomu) uzuri walikuwa wawili hawa ma bro mwenzake akamuuliza vipi? Jamaa akamtaja 'Gudume' basi mimi fasta nikazama JF lahaulaa! nkakutana na Uzi wa Gudume nikakausha.

Nikamcheki jamaa bado anajichekesha tu!, ghafla akaanza ku type nikasubiri post mpya nimjue aka post utumbo kinoma tofauti na muonekano wake ata sikuamini na mimi nkamsapoti kwa kum-quote ghafla nkasikia kantaja huku anaongea na mwenzake

Asa kila nkifika ofisi yao nabaki namcheka tu huyu bro wa early 40s maan ana post za ajabu ajabu. Sema uzuri si mtu wa jukwaa la siasa.

[bro wa Brela habari yako?, Mgeni wa Jiji nakusalimu[emoji1538]]
 
Hahahaaaaa sasa hapa na yy atakujua
 
Mi npo hapa play master betting baada ya kuandika mikeka yangu npo natumia jf bila kumuhofia fala yoyote.
 
Njemba moja ilikuwa humu miaka ya nyuma. Na alikuwa mchangiaji mzuri sana. Siku moja wamekaa sitting room na mkewe kila mmoja yuko busy kwenye lap top yake.
Basi mke akaenda jikoni ndiyo mume mbio kwenye lap top ya mkewe kuona alikuwa anafanya nini mtandaoni maana haikufunga lap top yake. Mke alikuwa humu na hivyo mume kujua ID yake.

Mume akaanza kufuatilia michango ya mkewe humu ndiyo kugundua anafagilia sana mambo ya tigo na kudai ni bomba sana. Jamaa alikuja kuandika humu kwamba kachanganyikiwa maana hawajawahi kufanya hiyo kitu wala kuizungumzia hivyo kubaki akijiuliza mkewe hufanya na nani?

Jamaa baada ya wiki tu alipotea humu labda alibadili ID.

me waifu wangu anajua tu nikiwa bize na pc anajua tayari natupia mavitu JF,ila hajui hata ID yangu
 
Mie nipo kwenye bajaji za kushare za buku buku hadi Mbagala hapa natumia JF.
 
Hata mimi kwakweli huwa nipo huru na jf yangu
Bahati nzuri sijawahi fanya lolote baya la kuniogofya mpaka nijifiche na nina mpango siku za hivi karibuni nitatumia jina langu kamali
Maisha ni jinsi uvyoyafanya yawe
 
Udhuri wa JF wengi wao ni wathomi kama vile mimi ni profesional ktk mambo ya computer. alafu sipendagi2 m2 anione nipo jf kwani akiona hata usename sipendi2 kwa kifupi.
 
Jf ni ya wasomi/ wanaojitambua huko kwingine mmmmhh!!
 
Getto mkuu hadharani you can be tissilized
 
Kuna majukwaa mengine yanaweusha ukiwa hadharani wanaweza kukuwahisha milembe eg. Jf foto, love connect.

Mengine yanahitaji utulivu mkubwa eg. Grt thinkaz inabidi uwe sehem tulivu kwelikweli

Ukisurf jf kuna nyuzi zinabamba kiasi ukiwa road unaweza ukavamia bodaboda au ukagongana na bajaji
 
Natumia app....popote pale. JF watu hawaijui na wanaoijua hawaifuatilii
 
Wana jf wanakaa maeneo tofauti ndo maana huwaoni. Mimi ninatumia JF nikiwa home, kazini, kwenye burudani like soka na draft
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…