Jf ni tofauti kiasi na hio mitandao mingine.
Jf watu wanamwaga taarifa ndefu na zenye kuhitaji utulivu wakati wa kuzisoma ili uelewe.
Sasa basi, kama ni hivyo maeneo pia ya kusoma,kudurusu,kudalizi,kudadisi,kuchambua na kuyaelewa hayo maandiko na mabandiko ya jf yanahitaji sifa zake kama
*Ukimya
*Utulivu na utayari..
Sasa sifa za haya maeneo mara nyingi hazipo kwenye madaladala,bar au sehem km hizo.
Ndio maana ni ngumu kuwaona watu wakitumia jf hadharani...sababu huko kwenye kadamnasi kunakosa zile sifa.