Member's mlioweka private profile zenu mnatukosesha nondo zetu...😔

Member's mlioweka private profile zenu mnatukosesha nondo zetu...😔

AmKATRINA

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
882
Reaction score
2,044
Habarini za muda huu wanajukwaa wenzangu.
Nawasalimu kwa nia njema kabisa.

Naomba niongee kidogo juu ya hili suala la mwana Jf KUTORUHUSU KU-VIEW PROFILE LAKE.
Hili suala kwa kweli linaumiza sana,najua si kwangu tu, hata kwa mwingine na mwingine.
Najua ni haki ya kila member kufanya atakalo kwenye profile yake, ila kiukweli hili suala wakati mwingine linanipa changamoto ya kupata baadhi ya nondo nilizokuwa napata hapo awali kabla Jf hawajaanza huu utaratibu.

Ipo mifano mingi sana ya wana Jf walioanzisha nyuzi zenye mafunzo, visa, elimu, maendeleo, mikasa na vingine vingi...lakini leo hii ukijaribu ku-view profile yake ili angalau ujikumbushe mada zake, unakutana na bango hili.
Screenshot_20240627-182357.jpg

Kiukweli bora niwe mkweli tu kuwa sasa hv tunakosa vingi sana.
Ni member's wachache sana wenye nondo wameturuhusu tu-view profile zao na kwenda kuangalia mada walizoanzisha, ila wengi sana mmetukatili.

Unatamani uende kwenye profile ya mtu fulani ili ukaview usome mada yake nzuri na yenye kuelimisha, ila unakutana na bango kubwa sana.
Please member's msitutese hivo.
Kila member ana ujuzi wa aina yake, tukajifunze wapi sasa🤧🤧🤧

Pm/conservation fungeni, ila achieni huko kwingine ili tupate maarifa zaidi.
Big up kwa wale wote wasioweka private,tunaendelea kujifunza mada kutoka kwao.
Tunaumia sana,ni vile tu hatuna pa kusemea.

Ndimi,
Katrina.
 
Attachments

  • Screenshot_20240627-182357.jpg
    Screenshot_20240627-182357.jpg
    151.4 KB · Views: 4
Katrina,

Pole kwa kadhia hiyo.

Lakini, member awaye yeyote hawezi kuzuia ufikaji wa post zake. Anaweza kulimit mtu kumuandikia private message (PM), mtu kuona picha yake kwa ukubwa, kuona taarifa za alipo na namna anavyo-interact humu.

Ila swala la posts zake hawezi abadani kuzuia zisionekane. Ili uweze kuona post za mhusika fanya yafuatayo;
1. Tafuta comment yeyote ya mhusika.
2. Bonyeza jina lake kwenye comment hiyo.
3. Itakuletea profile yake alafu kwa chini kuna posts, reaction score na points.

Wewe usidili na kisichokuhusu. Bonyeza hapo kwenye namba za posts. Utaona posts zake zote na comments.

Hangaika na unayotaka.
 
Mimi nilikua nimefunga ila nikiview za watu nakuta pia wamefunga nasikia hasira nikaona maumivu wanayopata wengine wakiview ya kwangu
Nikaamua niache yangu wazi
Yaani mimi ni leo nmegundua ndo nkakorokochoaa nkaweza na ni kabla ya hii mada sema kuangalia ya mtu nlijaribu member mmoja wa pili hvyohvyo ikaandika kama mtoa mada alivyosema na sijawahi jaribu tena😅😅
 
Katrina,

Pole kwa kadhia hiyo.

Lakini, member awaye yeyote hawezi kuzuia ufikaji wa post zake. Anaweza kulimit mtu kumuandikia private message (PM), mtu kuona picha yake kwa ukubwa, kuona taarifa za alipo na namna anavyo-interact humu.

Ila swala la posts zake hawezi abadani kuzuia zisionekane. Ili uweze kuona post za mhusika fanya yafuatayo;
1. Tafuta comment yeyote ya mhusika.
2. Bonyeza jina lake kwenye comment hiyo.
3. Itakuletea profile yake alafu kwa chini kuna posts, reaction score na points.

Wewe usidili na kisichokuhusu. Bonyeza hapo kwenye namba za posts. Utaona posts zake zote na comments.

Hangaika na unayotaka.
HAKUNA KITU KAMA HIKO.
HUONI MADA ZAKE HATA MOJA ....
Elewa ninachomaanisha.

Posts zake sio mada,
Post za hapa ni zile aidha alizochangia kwake au kwa wengine.
Nataka Mada yake...mada zake alizoanzisha.
NIELEWE
 
Afanye mambo mengine ya muhimu zaidi😂
Huwezi jua mtu kapatwa na tatizo na anataka solution, je...atapata wapi ufumbuzi?
Kusema nifanye mambo mengine ya muhimu, si wajibu wako huo na ndio maana nikaweka mada.
Kama unaona inakukera, an sorry acha ambao wanaielewa waendelee kuchangia ephen_ 🙏
 
Let's say nataka uzi wako unaozungumzia suala la athari za teknolojia ambao uliuanzisha mwezi Jan, nataka mada yako na si post yako ....mbona wavivu kunielewa?
Hiyo ni nyepesi zaidi.

Hapo juu, kuna kitufe cha search. Kibonyeze.

Kikifunguka kuna sehemu utaweka kichwa cha uzi ama neno lolote unalolikumbuka. Kama heading unaikumbuka vema weka.

Kisha kwa kuwa unamkumbuka muandishi basi pachika ID yake sehemu penye 'By member'.

Itakupeleka sehemu husika.
 
Mada zake zote kuja ni kitu hakiwezekani ephen_ .....never
JARIBU KISHA LETA MREJESHo
Mimi huwa ninafanya hivyo na ninapata mada za watu hadi za mwaka 2006
Cha muhimu jua hiyo mada inapatikana jukwaa gani

Nenda hilo jukwaa sehemu ya kusearch andika jina la member utaona posts zake zote
Huwezi jua mtu kapatwa na tatizo na anataka solution, je...atapata wapi ufumbuzi?
Kusema nifanye mambo mengine ya muhimu, si wajibu wako huo na ndio maana nikaweka mada.
Kama unaona inakukera, an sorry acha ambao wanaielewa waendelee kuchangia ephen_ 🙏
Naomba unisamehe! Nilifanya utani bila kujua utakasirika
 
Back
Top Bottom