Meneja Ahmed Ally afafanua Simba kufanya majaribio

Meneja Ahmed Ally afafanua Simba kufanya majaribio

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Anaandika Msemaji Mstaarabu Ahmed Ally katika kurasa ya Instagram

Ni kweli tuna wachezaji watatu tunawafanyia majaribio

Mashabiki wa Simba wamepata hofu kwanini timu yao na ukubwa wao wanafanya majaribio??

Kwanza kabla ya yote niwaambie tuu Wachezaji ambao sisi tunawafanyia majaribio wakienda timu yoyote ya hapa Africa Mashariki watapewa hadi unahodha

Au ingekua wale wengine wangelala Airport kuwasubiri lakini kwa ukubwa wa Simba tukasema hapana njoeni tujiridhishe kiufundi

Sisi hatusajili mtu kwa sababu tuu alifunga goli la Tiktaka

Majaribio ni aina ya mfumo wa Usajili unaokubalika duniani kote na yanampa fursa Mwalimu kumuangalia mchezaji kwa jicho lake mwenyewe (Naked Eye)

Kupitia majaribio Mwalimu anamfanyia tathimini mchezaji kwa kuangalia vitu muhimu kama vile Akili ya mchezaji (Mental health) , Ufundi (Technical) , mbinu ( Tactical) Presha ( Temperament) nguvu (Physic) nini anafanya akiwa na mpira na nini anafanya akiwa hana mpira (With or without a ball)

Vyote hivi huwezi kuvipata kwa kuangalia YouTube au kuhadithiwa na Wakala

Lakini kama haitoshi Majaribio pia yanampa fursa mchezaji mwenyewe kusoma mazingira ya klabu husika Ili aone kama anaweza kufanya kazi hapo au la

Wapo wachezaji wanaosajiliwa moja kwa moja na bado wamefeli hivyo kumnunua mchezaji hai gurentee atafanya vizur na unaemchukua kwa majaribio haina maana hajui Boli

Wana Simba tusiwe na presha na katika hawa ambao wapo kwenye Majaribio hakuna ambae atasajiliwa bila maagizo ya Mwalimu na kwa utaalamu wa Mwalimu wetu akipendekeza mchezaji basi anajua kweli

Tayar tumemuona Sharaf Shibob na Tenena Cheik na leo insha Allah tutamuona Etop David Udoh

Ingekua kusajili mchezaji moja kwa moja ni uhakika Sarpong angekua na top scorer

Tukutane Amaan Stadium tukaishudie timu yetu inatinga Nusu Fainali Inshallah🙏🙏
 
Majaribio ni utaratibu mzuri lakini ni wa kiridhaa zaidi, ni mzuri kama unataka kumleta mchezaji kwenye timu za vijana au shule za michezo...

Kwenye pro football watu hutumia zaidi scouting, mchezaji anafuatiliwa hata miaka 3 kimyakimya...

Mtazamo wangu
 
Tukija kwenye ukweli hamna club yenye scouting kama yanga bongo Anza kwa job,fei, yassin, chibada hadi kina kagere
 
ongezea akina sarpong, sibomana, bigirimana, yikpe, kindoki, bila kumsahau fiston abdulrazak
Bila kusahau hawa lukosa, nyoni,ilamfya,gut,ndemla, na mchezaji alieweka rekodi ya kutokugusa mpira tangu asajiliwe jeremia kisubi
 
Msimu ule kwenye mapinduzi hii hii tuliwafanyia Simba majaribio wachezaji wawili na hatukuwasajili, baadae Wakasajiliwa na Utopolo na Mmoja wao akapewa unaodha
Simba wakimwacha Maukolo lazima Yanga Yangu Wamsajiri.
 
Tatizo Mpalange FC wepesi sana kusahau,leo nimewasikia wale chawa wa GSM pale Efm muda wote wa kipindi ilikuwa madongo kwa Simba kwa kuwaacha baadhi ya wachezaji na wengine kuwapeleka kwa mkopo timu zingine wakati na Utopolo nao wamefanya hayo hayo. Hawa dawa yao View attachment 2071794

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Jamani mwenzenu niko nje ya dunia.

Hii Mirinda nyeusi imefanya Nini?
 
With vivid example.
FB_IMG_16415407339541529.jpg
 
Back
Top Bottom