Meneja KNCU asafiri kwa pikipiki toka Moshi hadi Shinyanga na kupata ajali

Meneja KNCU asafiri kwa pikipiki toka Moshi hadi Shinyanga na kupata ajali

Mkuu mikutano inapelekwa mbali na siku zinakua nyingi ili PerDiem iwe kubwa kubwa.
Tatizo ni hiyo njia ndio inawachanganya watu, mtu atoke moshi kwenda shinyanga, inakuwaje apitie tabora?wakati ni sehemu mbili zilizo kaa kushoto(haziingiliani)?
 
Sasa hiro route mbona ngumu kumeza sana. Alikatiza Serengeti au vipi na kwa nini hakupita hakupita ya babati kondoa dodoma au babati hydom Singida then aitafute tabora au mimi sielewi urefu wa hizi route.
Kuna njia ya kupitia Arusha, Ngorongoro, Meatu, Mhunze(Kishapu), Kolandoto na kufika Shinyanga.

Ila madhumuni ya safari ya Tabora yamepotoshwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nampongeza kwa uamuzi wake wa kubana matumizi.

Kilichomtokea ni ajari, ajari kama ajari imetokea si kwasababu amesafiria kwa pikipiki. Karibu vyombo vyote vya usafiri hupata ajari, hata meli na treni hutoke kupata ajari,- maneno yanayoashiria kumdhihaki kwasababu alitumia pikipiki ni maneno ya watu wabivu na malimbukeni.

Pole kwa familia ilyopoteza kijana wao, pole kwake maenyewe kwasababu ya hiyo ajari.

Kijana marehemu apumzike kwa amani.[emoji120][emoji120]
 
Kama Mungu alipanga Ajali hataingekuwaje angepatatu

Kama Mungu alipanga ajali kutokea ingetokea hata bila ya iyo pikipiki mh! Lakini jamaa anamoyo km 700 na ushehee kwa pikpik kweli Mangi kazidi
Ukiwa na protection gears unasepa kilometer kibao tu mkuu.

Ni kweli ajari haiangalii unatumia usafiri gani.
 
Aisee! Wachaga mmetisha kwa mara nyingine tena! Nadhani hii itakuwa ya kufungia mwaka!
 
Inaelezwa kisa cha kugoma kutumia gari hilo ni kubana matumizi ikiwamo mafuta,posho ya dereva na wajumbe ambao angeamabatana nao katika safari hiyo kitendo ambacho kinaelezwa ni cha kibinafsi kuliko maslahi ya chama.[emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Hii inaitwa roho mbaya na ubinafsi aliona angetumia gari wangekwenda wengi na wangepata posho kitu ambacho yeye asinge kifurahia, nawapa pole wanaofanya naye kazi. Pia hili liwe fundisho kwa wenye tabia kama ya huyu jamaa
 
Alitaka kuona maeneo yapi mengine ukiacha Kilimanjaro, Arusha, Serengeti na Mara yatafaa kulima kahawa.
 
Ukiwa na protection gears unasepa kilometer kibao tu mkuu.

Ni kweli ajari haiangalii unatumia usafiri gani.
Kuendesha piki piki masafa marefu huchosha sana mwili.

Makalio huuma kama umepigwa fimbo, kiuno ndiyo usiseme.

Pikipiki kwa safari ya km200 halisumbui, zaidi ya hapo labda upumzike ili kesho uendelee na safari yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanapopewa riziki na Mungu halafu ukizuia lazima upate shida.
 
Unatoka Moshi una fika Singida unapaa kuiruka Tabora adi Shinyanga una fia hapo seriously?
 
Inaelezwa kisa cha kugoma kutumia gari hilo ni kubana matumizi ikiwamo mafuta,posho ya dereva na wajumbe ambao angeamabatana nao katika safari hiyo kitendo ambacho kinaelezwa ni cha kibinafsi kuliko maslahi ya chama.[emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Mshana hii ajali atakuwa katengenezewa tu... maana si kwa roho mbaya hiyo. Tunguli zako zinasemaje😂😂
 
Tatizo makalio mkuu, yanakuwa ndembwe ndebwe kama umeyaazima.

Enzi hizo mi nilikuwa ninasonga hadi km300, lakini nafika nikiwa hoi kweli, nilikuwa natumia masaa6 safari hizo kwa rough road.

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani mkuu, makalio yamesharudi kwenye hali yake ya kawaida?. Au bado yako ndembe ndembwe kama ulivyoshuhudia?.
 
Back
Top Bottom