Meneja KNCU asafiri kwa pikipiki toka Moshi hadi Shinyanga na kupata ajali

Meneja KNCU asafiri kwa pikipiki toka Moshi hadi Shinyanga na kupata ajali

Imani za kishirikina tu hizo vinginevyo ni roho mbaya iliyopitiliza
 
Huyo ½hayati masawwe msenge sana amebana posho ya dereva kisa hicho kiwani ten chake

Mpuuzi kabisa kaenda kutuulia msomi msukuma orijino wa Shinyanga ambae ndio bado alikuwa anaanza kufaidi matunda ya elimu bure kutoka kwa hayati kamili(mchato)
 
Tena bora alivyokataa kwenda na uwakilishi ili apunguze idadi ya ajali
 
Sasa hiro route mbona ngumu kumeza sana. Alikatiza Serengeti au vipi na kwa nini hakupita hakupita ya babati kondoa dodoma au babati hydom Singida then aitafute tabora au mimi sielewi urefu wa hizi route.
Ni uongo , huwezi kutoka Moshi ukafika shinyanga kabla ya Tabora,, labda uzungukie Nairobi
 
Tatizo ni hiyo njia ndio inawachanganya watu, mtu atoke moshi kwenda shinyanga, inakuwaje apitie tabora?wakati ni sehemu mbili zilizo kaa kushoto(haziingiliani)?
Mkuu soma kwa makini ulichoandika utaona umejichanganya sehemu
 
Mbona sijaelewa hapo. Yan anatoka moshi kwenda tabora alaf ajari kapatia shinyanga? Alifata nn shinyanga?
 
Habari Ina uwalakini hii shinyanga imeingiaje hapo
 
Kama Mungu alipanga Ajali hataingekuwaje angepatatu

Kama Mungu alipanga ajali kutokea ingetokea hata bila ya iyo pikipiki mh! Lakini jamaa anamoyo km 700 na ushehee kwa pikpik kweli Mangi kazidi
Tusimsingizie Mungu
 
Unaweza ukashangaa lakini huo ndiyo ukweli wenyewe.

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro, Godfrey Massawe,hivi karibuni alisafiri kutoka Mjini Moshi kwenda Mkoani Tabora kwa shughuli za kichama akitumia usafiri wa pikipiki lengo likiwa ni kubana matumizi lakini kilichomtokea anajua mwenywe na Mungu wake.

Massawe alikuwa anakwenda kukiwakilisha chama chake kwenye mkutano wa wakulima wa kahawa lakini aliishia njiani baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga na kuumia vibaya lakini alisababisha kifo cha mtoto mdogo ambaye ni mwanafunzi baada ya kumgonga na kumsabaishia damu nyingi kuvuja na hatimaye kifo chake.

Taarfia kutoka ndani ya KNCU zinatonya kuwa,meneja huyo aligoma kutumia gari la chama aina ya Toyota LandCruser ambalo hutumiwa na viongozi wa chama hicho katika shughuli za kichama ikiwamo kusafiri.

Inaelezwa kisa cha kugoma kutumia gari hilo ni kubana matumizi ikiwamo mafuta,posho ya dereva na wajumbe ambao angeamabatana nao katika safari hiyo kitendo ambacho kinaelezwa ni cha kibinafsi kuliko maslahi ya chama.

Lakini matokeo ya kubana matumizi ndo hayo, Massawe hakufika mwisho wa safari yake na hata uwakilishi wa chama chake katika mkutano huo ukayeyuka .

Kazi mwenu mnaobana matumizi kwa mauala yenye tija kwa Taasisi zenu,lakini Mungu anawaona.
We muongo sana..hiyo route haipoo
 
Pole sana kwa Masawe, ila hapa naona aliwaiga Watani zake wa kipare.
 
Tatizo makalio mkuu, yanakuwa ndembwe ndebwe kama umeyaazima.

Enzi hizo mi nilikuwa ninasonga hadi km300, lakini nafika nikiwa hoi kweli, nilikuwa natumia masaa6 safari hizo kwa rough road.

Sent using Jamii Forums mobile app
😊😊😊Ukifika unakaa kama mtu mwenye vidonda kwenye makalio.

Siku moja nimepita njia yenye mbung'o, na nilikuwa sijaa gloves. Mara nasikia maumivu makali kwenye kiganja, tena kiganja chenyewe cha mkono wa kulia kwenye accelerator. Nikajikaza nikashindwa kuvumilia halafu nilikuwa bado sijakuwa mzoefu kuendesha pikipiki. Nikaachia mkono ili nimwadhibu nduli ndorobo aliyekuwa ameanza kufyonza damu ya bure. Yale maumivu yalinifanya nisahau kuwa huu mkono ninaoachia ndio wenye mafuta. Aisee nilikosa balance, chombo kikazima na kupoteza mwelekeo, nikapiga mweleka na ndorobo kasepa zake alipoona nataka kutoa uhai wake. Bahati nzuri sikuwa kwenye mwendo kasi hatarishi. Nilianguka lakini sikuumia.
 
[emoji4][emoji4][emoji4]Ukifika unakaa kama mtu mwenye vidonda kwenye makalio.

Siku moja nimepita njia yenye mbung'o, na nilikuwa sijaa gloves. Mara nasikia maumivu makali kwenye kiganja, tena kiganja chenyewe cha mkono wa kulia kwenye accelerator. Nikajikaza nikashindwa kuvumilia halafu nilikuwa bado sijakuwa mzoefu kuendesha pikipiki. Nikaachia mkono ili nimwadhibu nduli ndorobo aliyekuwa ameanza kufyonza damu ya bure. Yale maumivu yalinifanya nisahau kuwa huu mkono ninaoachia ndio wenye mafuta. Aisee nilikosa balance, chombo kikazima na kupoteza mwelekeo, nikapiga mweleka na ndorobo kasepa zake alipoona nataka kutoa uhai wake. Bahati nzuri sikuwa kwenye mwendo kasi hatarishi. Nilianguka lakini sikuumia.
Dah! Pole sana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom