Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Haujasafiri na pikipiki masafa marefu, usingeuliza hilo swali.Samahani mkuu, makalio yajo yamesharudi kwenye hali yake ya kawaida?. Au bado yako ndembe ndembwe kama ulivyoshuhudia?.
Ni uongo , huwezi kutoka Moshi ukafika shinyanga kabla ya Tabora,, labda uzungukie NairobiSasa hiro route mbona ngumu kumeza sana. Alikatiza Serengeti au vipi na kwa nini hakupita hakupita ya babati kondoa dodoma au babati hydom Singida then aitafute tabora au mimi sielewi urefu wa hizi route.
Hata mm nimeshangaa kwakwel tabora ipo nyuma na shinyanga ipo mbrele ZaidAlikuwa anatokea Moshi kwenda Tabora na ajali akapatia Shinyanga?
Asante kwa taarifa.
Mkuu soma kwa makini ulichoandika utaona umejichanganya sehemuTatizo ni hiyo njia ndio inawachanganya watu, mtu atoke moshi kwenda shinyanga, inakuwaje apitie tabora?wakati ni sehemu mbili zilizo kaa kushoto(haziingiliani)?
Aliyekufa sio masaweUna kipaji sana aisee yani unaongea na Marehemu?
au ndio ile kwenye kila watanzania wanne mmoja ni chizi maarifa?
MchepukoMbona sijaelewa hapo. Yan anatoka moshi kwenda tabora alaf ajari kapatia shinyanga? Alifata nn shinyanga?
Tusimsingizie MunguKama Mungu alipanga Ajali hataingekuwaje angepatatu
Kama Mungu alipanga ajali kutokea ingetokea hata bila ya iyo pikipiki mh! Lakini jamaa anamoyo km 700 na ushehee kwa pikpik kweli Mangi kazidi
Ajengwe mnara kabisaHuyu ni kichaa
Yawezekana mkuuHiyo route ya kupita shinyanga ukiwa unatoka Moshi kwenda Tabora alizungukia mbuga ya Serengeti akapitia mwanza..??
Na usikute kwenye begi alikuwa na miraa ya biashara!Ila we masawe ni noma sasa c ungepanda basi tu au ulikua na mambo yako tu.
We muongo sana..hiyo route haipooUnaweza ukashangaa lakini huo ndiyo ukweli wenyewe.
Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro, Godfrey Massawe,hivi karibuni alisafiri kutoka Mjini Moshi kwenda Mkoani Tabora kwa shughuli za kichama akitumia usafiri wa pikipiki lengo likiwa ni kubana matumizi lakini kilichomtokea anajua mwenywe na Mungu wake.
Massawe alikuwa anakwenda kukiwakilisha chama chake kwenye mkutano wa wakulima wa kahawa lakini aliishia njiani baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga na kuumia vibaya lakini alisababisha kifo cha mtoto mdogo ambaye ni mwanafunzi baada ya kumgonga na kumsabaishia damu nyingi kuvuja na hatimaye kifo chake.
Taarfia kutoka ndani ya KNCU zinatonya kuwa,meneja huyo aligoma kutumia gari la chama aina ya Toyota LandCruser ambalo hutumiwa na viongozi wa chama hicho katika shughuli za kichama ikiwamo kusafiri.
Inaelezwa kisa cha kugoma kutumia gari hilo ni kubana matumizi ikiwamo mafuta,posho ya dereva na wajumbe ambao angeamabatana nao katika safari hiyo kitendo ambacho kinaelezwa ni cha kibinafsi kuliko maslahi ya chama.
Lakini matokeo ya kubana matumizi ndo hayo, Massawe hakufika mwisho wa safari yake na hata uwakilishi wa chama chake katika mkutano huo ukayeyuka .
Kazi mwenu mnaobana matumizi kwa mauala yenye tija kwa Taasisi zenu,lakini Mungu anawaona.
😊😊😊Ukifika unakaa kama mtu mwenye vidonda kwenye makalio.Tatizo makalio mkuu, yanakuwa ndembwe ndebwe kama umeyaazima.
Enzi hizo mi nilikuwa ninasonga hadi km300, lakini nafika nikiwa hoi kweli, nilikuwa natumia masaa6 safari hizo kwa rough road.
Sent using Jamii Forums mobile app
Dah! Pole sana mkuu.[emoji4][emoji4][emoji4]Ukifika unakaa kama mtu mwenye vidonda kwenye makalio.
Siku moja nimepita njia yenye mbung'o, na nilikuwa sijaa gloves. Mara nasikia maumivu makali kwenye kiganja, tena kiganja chenyewe cha mkono wa kulia kwenye accelerator. Nikajikaza nikashindwa kuvumilia halafu nilikuwa bado sijakuwa mzoefu kuendesha pikipiki. Nikaachia mkono ili nimwadhibu nduli ndorobo aliyekuwa ameanza kufyonza damu ya bure. Yale maumivu yalinifanya nisahau kuwa huu mkono ninaoachia ndio wenye mafuta. Aisee nilikosa balance, chombo kikazima na kupoteza mwelekeo, nikapiga mweleka na ndorobo kasepa zake alipoona nataka kutoa uhai wake. Bahati nzuri sikuwa kwenye mwendo kasi hatarishi. Nilianguka lakini sikuumia.