chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Serikali ifanye uamuzi mgumu, hii ni biashara ya hasara, nadhani ATCL wajikumbushe sababu zilizofanya ATC ikafilisika, abiria sita ni sawa na milioni mbili laki nne kwa nauli ya laki nne, Dar-Chato direct flight, maana yake kama ni dreamliner siti nyingi hazikaliwi,inaenda tupu kwa asilimia 98
======
Kamati ya Barabara ya mkoa wa Geita imefanya ziara ya kukuagua barabara mkoani humo kikiwemo kiwanja cha ndege cha Geita kilichopo wilayani Chato na kuridhishwa na mwenendo ukamilishaji ujenzi wa kiwanja hicho sambamba na utoaji huduma ya usafirishaji
"Tumeshahudumia abiria – in-bound na out-bound – kama 3000. Yani kwa mwezi, on average, ni kama abiria 250 mpaka 300 ambao wanatumia kiwanja hiki" Amesema afisa wa Chato Airport
Naye Rosemary Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Geita, amesema:
"Tumeuona ni mradi ambao una viwango ambavyo ni vya juu na haujawahi kupata ufa, haujawahi kupata ajali yoyote. Ni uwanja ambao tangu umejengwa ni imara na umeendelea kutumika mpaka sasa...
… sanasana tuendelee kualika abiria. Tuna safari mbili kwa sasa lakini tunategemea kupata safari tatu kwa wiki. Tuendelee kuwakaribisha watu waendelee kuutumia uwanja huu kwani ni mzuri na wenzetu wa ATCL wametuletea ndege zinakuja. Tuendelee kuunga mkono juhudi kwa kuutumia uwanja huu kama ambavyo wengine wanaendelea kufanya.
Bado tunawakumbusha wenzetu wa ATCL waturudishie route tuwe na siku tatu kwasababu abiria ni wengi. Mnaosimamia hapa muendelee kutunza miundombinu hii… kama ambavyo serikali imewekeza fedha nyingi katika eneo hili
Tumeambiwa zaidi ya bilioni 59 zimetumika kuweza kukamilisha hizi hatua ambazo zipo…"
=====