Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amjibu Shigongo

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amjibu Shigongo

Shigongo anatafuta kiki kupitia Diamond. Kama vipi na yeye ajiite Diamondrapa tujue moja.
 
Shigongo amekuwa mpuuzi, yaani nilikuwa najiuliza sana kwa anayowaandikia wasanii ya ukweli...?
 
Huku mwaka ni mwaka wa wasukuma, wanatrend hao kuanza January makonda, mara gwajima tukapumzika kidogo Shigongo, sijui baadaye atakuwa nani. Ila nimekaa nimejiuliza Kuna msemo mmoja wa fid q anasema '' SIKU HIZI HAMNA UHURU WA HABARI, KUNA UHURU WA MWENYE MITAMBO NA MWENYE MALI '' sasa naliamini, sasa subiria reaction ya Shigongo na magazeti yake, atakavyomuandama diamond platnumz na management yake, ila kwa diamond platnumz nina uhakika atashindwa tuu, kwanza hata yeye mwenyewe na magazeti yake hali ni mbaya, instagram, Facebook, Twitter na whatsup zinampa stress na bado kama hana mpango mbadala wa kuiokoa kampuni yake yeye ndio atakuwa wa kwanza kudondoka.
 
"Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao.
Kumbe wazaramo asili yao ni waluguru? Maana haya maneno yalitakiwa yatolewe na watu wa Msangangongelo ama Kimanzinchana!!
 
Shigongo kaamua kuchapisha gazeti la ijumaa kama jarida halafu anauza kwa buku tu, sijui anapata faida gan
 
Sikuwahi wala sikutaka kuamini kama shigongo nyumbu kiasi hicho kweli magufuli kabana watu biashara zimebuma yani shigongo leo hii ndio unataka kutelezea kwa mondi kweli kua uyaone sio kwa kiki hii umejinyea bro
Umepuyangaaaaaa[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
 
Kwanza imebidi niende huko insta nikamtafute huyo bwana shigongo halafu ndo nirudi kusema kitu.

Huyu jamaa (shigongo), bashite na bwana yule wanawaangusha kweli kweli wasukuma wenzao. Wanawafanya wasukuma wazidi kuonekana watu wa ovyo ovyo.

Kushindwa kwake kumuafford mondi isiwe big issue, so anataka aweke dau dogo ili yeye afaidike mwenzake azame?

Aisee tale kasema vema mbona yeye hapangiwi gazeti lake auze bei gani?

Mbona mondi anapiga show za buku 30, wasafi beach part, na kule iringa.

Nàrudia tena huyu shigongo, bashite na bwana yule wanawaangusha wasukuma kweli kweli
 
Tale hajui kuandka vizr cjaelewa chochote itakuwa kaandkiwa na mke wake
 
Udaku hauuziki siku hizi watu wapo instagram, youtube na kucheki shilawadu.
Teh teh teh.
 
Shigongo maisha yashamuendea hovyo badala ya kumshauri domo kwanini asije kulipa wafanyakazi wake mishahara mara wanafedheheka na mishahara ya tarehe 40,mpaka leo tarehe31 dirishani kweupe, then me pia namshauri aache kuzaa zaa hovyo na wafanyakazi wake huku akiwaweka ofisi moja, awe na heshima na ndoa yake kwanza
 
Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya. Baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako.

Siku zote nimekuheshimu na sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali.... tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu.

Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond ila sie tumekaa kimya na kujifanya unazunga eti unatushauri. Kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?

Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? Na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa.

Hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na mashabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum'bomoa msanii kupitia magazeti yako.

Tafadhali heshimu heshima yetu kwako. "Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao.
Duuu [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Erick atulie, now hatusomi magazeti umbea tunaupata insta lazima apate stress!!

Huwa ana karoho kabaya sana yule baba
Halafu anajifanya mlokole, kuna watu wana maigizo dunia hii
 
Mbona hajaongelea dau la dola 55,000 .
Maana ndo ushauri alioutoa shigongo...nilitegemea angejibu ushauri huo kwa kusema kwa vipi haitowezekana kushusha dau...badala yake anaongelea vijembe na shutma za kike kike.
 
Back
Top Bottom