Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Kapambana kipo wapi mzee???

Wote wewe mfanyakazi na wafanyabiashara tunajua kuna mianya yenu ya upigaji ridhikeni nayo msiende kwenye jinai mbaya kama hizi ona kijana fresh alitegemea afanye mengi kwenye maisha yake lakini sasa kazi hana na bangili amekula.
 
Aisee! Tuseme kwamba mshahara anaopata pamoja na marupurupu ya Cheo Cha Umeneja wa TRA havitoshelezi mahitaji yake ya msingi ya kiuchumi? Is it??

Ama kweli kwamba Ufisadi ni tabia, Wala siyo kwa sababu ya kipato kidogo kisichokidhi mahitaji.

Kwani huoni matozo yanavumbuliwa kila leo! Srkl haitosheki na ilichonacho

Kweli peponi wataingia wachache sana
 
Tamaa mbaya ...
 
alikuwa anatumia gari ya serikali au vipi? pia, hapo mbona rahisi tu, atauza nyumba, analipa kwa plea bargaining, imeisha hiyo. tembo nadhani gharama yake kama 30m, wakipiga mara tatu 90m anatoka fresh. ila kazi ndio hana tena. wao wanaita hizo ni bahati mbaya kazini. inawezekana kashakusanya nyingi zaidi ya hizo, na mawakili wa serikali walivyo wabaya watapora hata nyumba na magari aliyonayo.
 
Siku hizi TRA hakuna maokoto ya kutosha mpaka viongozi mnafanya biashara haramu?

top level manager kabisa, umezingua sana
TRA maokoto ya kawaida sana,, ishu ni chocho la kula pesa haramu kama wale wazee wa bandari tu ,labda wale wa vyeo vya juu maokoto yana maajabu kidogo, ila huku kwa wakina ofisa ni kawaida sema njia za kula nje ya mshahara ndo nyingi
 
Awaambie alikua anaenda kutengenezea tusker amwagilie moyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…