Kumbe unamkumbuka, wale waarabu wa yemen wana balaa, ndio alikua mjomba wake, na leaky abdalah, ambao familia yao nyingine ni akina mahsein, sasa aliebakia ni mdogo wao mmoja anaitwa jamal tamim yuko palepale mabamba ndio alikua na leseni ya uwindaji kwenye yale mapori nadhani hadi leo bado anamiliki vile vitalu, hao ni family friend na mzee kinana na Kwa sasa jamal tamim ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa kigoma, lakini najaribu kuangalia dili za waarabu anzia akina shabiby, superdoll, ssf, aboud na hao akina sharif abdalah waliamua kukaa karibu na hifadhi za wanyama pori na ni matajri wa kutupwa, hata akina, waarabu wengi hukaa karibu na mapori ya hifadhi hata Baba yao gharib gsm nae alikua pale tunduru ilipo hifadhi ya selou sijui ni kilimo kinawatoa labda,
Hilo lisikutie wasiwasi, watu hufanya mengi ya halali na yasiyo ya halali.
Kitu cha kukumbuka ni kuwa mitaji ya uhakika ni mali za asili, na mali za asili ni ngumu sana kuzipata mijini. mijini wanakuja kuwekeza baada ya kupata mitaji. Matajiri kuwepo mbali na miji si lazima wawe wanafanya kazi za magendo.
Baba yao kina GSM si Tunduru tu, hata Tanga kaishi. Kumbuka hawa mawahara miaka ya 70s walikuwa wanakuja kwa wingi Tanzania baada ya nchini kwao Yemen kuwa ni wakomunisti, ile haswa sio ya usoshalisti kama Tanzania.
Hawa Wamahara ni wachapa kazi sana, nakumbuka kila anaekuja alikuwa anaanza kuuza nguo kwa kutembeza na kukopesha wakiitwa "guoguo", naamini na baba yao kina Ghalib ilikuwa ni hivyo hivyo. Kidogo kidogo wakawa wanatawanyika kuanzia mijini mpaka vijijini, huko of course walikuwa wanakutana na fursa zingine, kama hizi za kusfirisha pembe, miti, mbao, makaaa ambavzo zote kwao ni mali na huku wameona kama wanaziokota bure. Wakichuma walikuwa wanawekeza kwenye maduka na majumba mijini.
Uzuri wa hao Warabu hawana ubaguzi, wameowana na wenyeji na walikuwa si wazinzi.
Hao wa Morogoro wao kazi zao kubwa zilikuwa ni sukari guru m[paka wengine sasa ni wazalishaji wakubwa wa sukari kama wa Mtibwa.
Wamefanya biashara na wenyeji na wazawa na uzuri wao hao hawamdhulumu mtu kwenye biashara, lakini wenyeji ndiyo kama unavyotujuwa tukipata pesa tunataka kutanuwa, kulewa sana, ngoma na sherehe nyingi, tunaishia kuwa omba omba kwa wajomba zetu.
Sema hao Waarabu walikuwa na roho ngumu na mashujaa kwenda kuishi mbali na kwao maporini, wamekumbana na majanga mengi sana mpaka wao, watoto au wajukuu zao kupata mafanikio.
Uzuri wao, siyo wajinga kama wenyeji.