Menejimenti ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha Chini ya Engineer Justin Rujomba imetumia Milioni Mia Mbili na Kumi na Sita ( 216 Milion) kwenda Mwanza kwenye Semina na Kutalii kwenye Mbuga ya Wanyama Serengeti kinyume na maagizo ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasim Majaliwa aliyoyatoa wakati akifunga Bunge la Bajeti 2022/2023.
Mheshimiwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa alipiga marufuku Taasisi za Umma kutumia Fedha za walipa kodi katika Semina , Warsha na Utalii na badala yake akatoa agizo semina na Warsha Zifanyike kwa Njia ya mitandao ili kuongeza kasi ya maendeleo.
Ziara hii imefanya Shuguli za Mamlaka ( Maunganisho Mapya , Makusanyo na Uzibaji wa Mivujo ) kusimama kutokana na Usafiri wa Mafundi kwa maana ya Magari 8 yameenda katika Ziara hiyo hivyo Kufanya Mafundi kushindwa kwenda sites kuhudumia Wakazi wa Jiji la Arusha.
Kaimu Mkurugenzi AUWSA ameachiwa Junior staff Arnord Kipanju ( Ambaye ni Mpwa wake MD Rujomba) kutokana na Menejiment yote ( MD, Wakuu wa Idara , Wakuu wa Sehemu na units) wote 28 wamesafiri .
Ziara hii inafanyika wakati Upotevu wa Maji AUWSA ukiwa ni 63% kwa Lugha Raisi ni kwamba AUWSA inauza Maji asilimia 37% tuu Asilimia 63 ya Maji yanapotea
Pamoja na Serikali kuu Kuvunja mkataba wa AUWSA na Mkandarasi wa Mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Uhondoaji majitaka wa A to Z Kampuni ya Tumaini Engineer wahusika waliousika katika kuingia Mkataba huu wa kifisadi wapo huru na wanajisifu hakuna wa kuwakamata kwa maana wameiweka Wizara ya Maji, na TAKUKURU Arusha Mfukoni .
Haya yanatendeka ikiwa Tayari Serikali Imetoa Tzs 530 bilion kusambaza maji Jiji la Arusha lakini Maji ayaonekani yakiongezeka katika Jiji la Arusha Mgao wa Maji umeongezeka maradufu.