Menejimenti ya AUWSA yakaidi agizo la Waziri Mkuu, Wametumia Milioni 216 kwenda kutalii Mwanza

Rujomba alisababidha kifo cha Driver Aseri Munisi ( Mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi Munisi)

Huyu Kijana wa Mzee Munisi alisoma na Rujomba Chuo kimoja wakagombania Mwanamke na Rujomba ,Alipoteuliwa tuu kuwa MD wa AUWSA akambambikizia Munisi
Kesi ya Wizi wa Mafuta na Kumsimamisha kazi.

Munisi alifariki kutokana na Msongo wa mawazo baada ya Kusimamishwa kazi kwa muda Mrefu

Rujomba ni Fisadi na Muhuaji.
 
Ofisi ya Rais, Waziri Mkuu , PCCB , CAG , PPRA chunguzeni maeneo haya.

1.Management kutumia kiasi cha Shilingi 216 kwenye kutembelea Mbuga ya Wanyama na Mwanza ni Sahii wakati AUWSA upotevu wa Maji ( NRW) ni 64%, Ni sahii management kutumia kiasi hiki cha pesa wakati watumishi wa AUWSA wanadai 100,000/= Posho ya Mwezi awajapokea hadi leo, Na kwanini wamekaidi maelekezo ya waziri mkuu yq kutosafiri.

2.Ni Sahii Rujomba kutumia Tzs 10 milion kuunda kamati kwenda Dar kukagua Furniture, alitumia Criteria gani kuhunda hii kamati? Na Je wajumbe wa hii kamati kuna ambaye ana taaluma na useremala? Na Je Value For money hipo ?

3. Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya uhondoaji Maji taka A to Z wa TZs 2.5 bilion Uchunguzwe, Kwanini Mkandarasi Tumaini Engineer alipewa mkataba bila zabuni kutangazwa, Baada ya Mchunguzi huru Moshi town kuandika sana Juhuu ya huu mradi mkataba ukavunjwa , Je waliousika katika huu Mkataba wa Kifisadi wamechukuliwa hatua gani? Na Je Kampuni ya Tumaini engineer Imechukuliwa hatua gani? Wahusika wapo mtaani wanatamba wameshatoa Mshiko awawezi kufanywa chochote.

4.Ichunguzwe kwanini Eng Rujomba kanunuliwa Simu yenye Thamani ya Tzs 5,560,000.00 wakati Mkataba wa hali bora unasema MD atanunuliwa simu ya Tzs 1,000,000.00 Baada ya kipindi cha miaka 3. Kwanini ametumia pesa kinyume na mkataba wa hali bora?

5.Watumishi Kutishiwa na Rujomba kuwa atatoa pesa kwa Waziri Wa
maji Awewo awafukuze kazi kama
Alivyofanya kwa Eng Mwiyombela, Edes
mushi , Mwajabu na Kitigwa ,kunyanyaswa, Kutukanwa, kudhalilishwa na Eng Rujomba na wengi wameshushwa vyeo kinyume na Sheria za Utumishi.. Ushaidi ya watumishi walionewa hipo hapo Juhu.Watumishi zaidi ya 25 wameshushwa vyeo bila sababu , Mkurugenzi wa Jiji la Arusha aliamisha watumishi 48 Waziri Mkuu akasema siyo Jambo la kawaida watumishi 48 kuamishwa Eng Rujomba siyo jambo la kawaida achunguzwe,

6. Mradi wa Visima 5 vyenye thamani ya TZs 15 bilion vinavyochimbwa Arumeru Uchunguzwe, Visima hivi vinachimbwa maeneo yenye Fluoride zaidi ya 25% , Maji ayatafaa kwa Matumizi ya Binadamu,

7.kamati ya Uchunguzi ipitie Busines Plan iliyotumika kuomba Mkopo wa Tzs 530 bilion bank ya Africa na ichunguze Je mradi umekuwa na tija au hasara?

8. Ununuzi wa Uniform 2022/2023 Uchunguzwe Eng Rujomba ametoa maagizo kampuni ya kupewa kazi, Alituma Picha ya Sample ya Uniform akiiwa Nje ya Nchi ( Nertheland) kwa HPMU ambaye aliitisha kikao cha Mangement na kuomba management ipitishe ununuzi wa mashati haya kwa sababu ni maelekezo ya MD, Maswali ya Msingi kwanini Eng Rujomba apendekeze uniform za Kununua na siyo evalution comitee? Na kwanini Sample ipelekwe management na siyo kwa wafanyakazi ?Jukumu la pCCB ni kupambana na kuzuhia Rushwa… Hii bado mna Fursa ya Kuzuhia Supplier bado ajaleta uniform.

9. Ichunguzwe kwanini AUWSA imetumia 41 Milion kukarimu kamati ya Bunge ya bajeti Tarehe 6 Julai 2022. Je ni Sahii AUWSA kuwalipa Wabunge posho kuwanyamazisha wasiseme Juhu ya Matumizi mabaya ya Fedha za Covid?

10. Ichunguzwe kwanini baadhi ya Member wa Management walikuwa likizo wiki ya Maji na Kukumbiza Mwenge
wamelipwa Posho

11: Ichunguzwe kwanini AUWSA ilimpatia zabuni Fundi Garage bubu John kutoka moshi kutengeneza magari wakati muongozo wa Serikali ni magari yatengenezwe Tamesa , Fundi Johon alipatikanaje ? Magari aliyotengeneza yote yamesimama nani atafidia hasara aliyolet fundi John?

12. Waziri na katibu mkuu waojiwe ni kweli wameagiza mabomba yanunuliwe Plasco au ni Janja janja ya Eng Rujomba? Week iliyopita Eng Rujomba amemuita HPMU na kumuagiza afanye namna kuwaondoa kampuni ya Lodhia na Simba Plastic zabuni ya Mabomba apatiwe Plasco kuwa ni maagizo ya Waziri wa Maji.. Na kama waziri anatoa maagizo haoni kama anapingana na Rais mama Samia ambaye antumia nguvu nyingi Kujenga sekta binafsi ( Private sector).. Tume ya Ushindani ( Fair Competition) ingilieni ili.

12. Ichunguzwe Malalamiko ya Upendeleo vyeo Je walipandishwa vyeo wana sifa kulingana na Scheme of Service iliyopo na iliyotolewa na Utumishi? Na Kama Scheme of Service aifuatwi kwanini ENg Rujomba asiwajibishwe?

13. Ichunguzwe kwanini Rujomba alimuachia Ofisi wakati wa Ziara ya management mbugani Serengeti na Mwanza Junior staff ( Mpwa wake) Arnord Kipanju akasafiri , Je ni Sahii MD
ana Mamlaka ya Kumuachia mtumishi yoyote ofisi hata akiwa ni Junior? Je AUWSA ina Succesion Plan ? Na Ichunguzwe kipindi amemuachia Mpwa wake kipanju ofisi kuna Loss yoyote imetokea?

14. Baada ya Mchunguzi huru moshi Town kutoa taarifa za Safari ya Management ya AUWSA Mbugani Serengeti na Mwanza Eng Rujomba alikatisha ziara akarudi Ofisini Ichunguzwe Je Baada ya kukatisha ziara amerudisha pesa alizopewa za siku 10? Amekaa ziara siku 2 anatakiwa kurudisha pesa za Siku 8 na mafuta maaana akukamilisha ziara.

15. Kwa taratibu MD anaposafiri / Kuwa Nje ya kituo cha kazi anapaswa kuandika barua ya kukabidhi ofisi na Nakala
Kwa RAS na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Je? Barua ya Kumkabidhi Ofisi Mpwa wake Arnord Kipanju alituma nakala kwa
Katibu mkuu na RAS? Na kama alituma Je? Baada ya kurudi kabla ya Siku kuisha ameandika Barua kwa katibu mkuu na RAS kuwataarifu ametengua mpwa wake Arnord Kipanju kukaimu Ukurugenzi? Au aliacha ofisi rejareja kama mtu anayetoka chooni na akarudi ofisini Rejareja kama mtu anayeingia chooni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…