FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
1.) Sijasema maudhui ya habari za ITV na maudhui ya habari za Shilawadu ni sawa, la hasha, bali nilichosema ni kwamba sioni connection ya ‘content’ za habari hizo na hoja hii, unless kama tayari una bias dhidi ya habari zinazoletwa kwa mtindo wa ‘kusherehesha’ hadhira, otherwise wote wanawasilisha taarifa kama wanavyozipokea toka kwenye vyanzo vyao, ila tu hawa Shilawadu wako artistic zaidi kwenye kuwasilisha taarifa zao, utangazaji ni sanaa, na ubunifu katika kuiteka hadhira ni muhimu, nikushauri uondoe kwanza bias uliyonayo dhidi ya wale wanaowasilisha habari kiubunifu zaidi (Kwa mtindo wa kusasambua).Tunaweza kabisa kujadiliana bila kutumia lugha za kuudhi utadhani huu ni UGONVI....... relax mkuu sio kila anayefikiri tofauti na wewe basi hana wala hatumii akili
Kama unaona maudhui ya taarifa ya habari na kipindi cha shilawadu(umbea) ni sawasawa basi hatuwezi kufikia muafaka
Nakupa tu dondoo kwamba kwenye tasnia ya habari kuna kuripoti habari na kutengeneza habari
Mayu akifa una RIPOTI kwamba amekufa
Lakini ukitaka amekufakufaje kwa undani zaidi inabidi utengeneze habari sasa kwa kuanza kukusanya taarifa...... iwapo hiyo taarifa yako ikitoka Mayu kafaje na wenye Mayu wao wakaona taarifa hiyo haina ukweli na inawachafua wanahaki ya kukushtaki mtengeneza taarifa
Huwezi kutengeneza li habari lako kwamba Mayu anakula nyama za watu kisha ukaenda kwa majirani na kuanza kuwahoji leading questions na wakasema ooh ndio tunamuonaga anapita na mifuko ina onekana ina nyama tena mida ya usiku kisha ukajustfy nakula nyama za watu
Kama umekiangalia kile kipindi majirani wenyewe hawajathibitisha kwamba menina kamuua mumewe isipikua ilikua ni mafununu ya kijinga kama “alikua anatoka asubuhi anarudi usiku kamtelekeza mgonjwa ndani”
Kuhusu youtube ukiupload ujinga unashtakiwa ulieupload kwenye chaneli yako sheria inakutaka kujisajili
Kama unadhani hii ni issue ndogo unajidanganya sana
Hadi sasa kipindi hakiendi tena hewani wanajitathmini upya
Kuna mamilioni ya kesi ambayo vyombo vya habari vilitengeneza habari ambazo hazikua za kweli na kuchafua watu wakalipa
Huwezi kutengeneza habari zako za kishenzi kisha ukatafuta washenzi wenzako ukawagoji kuchafua watu kisha ukajivua mzigo kisa umehoji wajinga wenzako
2.) Hapo kwenye kutemgemeza habari ni kile tunachoita ‘investigative journalism’, na inaruhusiwa, kama tumepata taarifa kwamba Mayu amefariki, basi kwa mtimdo wa ‘investigative journalism’ tunalazimika kifanya uchunguzi na kukusanya taarifa toka kwa vyanzo vilivyopo, sasa tangu lini kufanya uchunguzi ikiwa kutengeneza tena habari? Yaani habari ipo tayari halafu useme tumeitengeneza? Kwa msingi upi udai hivyo? Chanzo kimoja wapo ni majirani, na hakuna ubaya kiwahoji maana wao ndio wapo karibu na eneo la tukio, ila kinachofanyika ni kukupigia simu ili kusikia upande wa pili wanasemaje, ila kwakuwa muhusika ni kiburi na hataki kuongea na waandishi wanaofanya utafiti na uchunguzi wa habari husika, then unawapa go ahead ya wao kurusha upande mmoja tu wa habari, halafu naadae wewe ndio utaamua ukanushenau otherwise, maana ulipewa chance kabla ila ukai-pass. Dstv wametimiza jukumu lao kwa wateja wao kwa kurusha taarifa ya majirani kama ilivyo, na hawawezi kuwajibika kwa yaliyosemwa na majirani, mnapoteza mida tu huko mahakamani. Kuuliza maswali ambayo wewe unahisi ni leading si kigezo cha wao kuitikia ndio wakati sivyo, ila mwandishi ni lazima utoe muelekeo wa mahojiano yako. Nasisitiza, DSTV hajatengeneza habari, na si kazi yake na haijawahi kuwa kazi yake, bali waliwasilisha habari kama ilivyokuwa na wakaichambua.
Pia nikuulize, hao majirani uliowaita WASHENZI kupitia JF, wakitaka kudai fidia kwa kuitwa WASHENZI, wataishtaki JAMIIFORUMS au watakutafuta wewe MAYU kwa msaada wa JF database ili ukajibu mashtaka mahakamani kwa kuwaita WASHENZ?