Menina aishtaki DSTV, adai shilingi za kitanzania bilioni 1.2

Tunaweza kabisa kujadiliana bila kutumia lugha za kuudhi utadhani huu ni UGONVI....... relax mkuu sio kila anayefikiri tofauti na wewe basi hana wala hatumii akili

Kama unaona maudhui ya taarifa ya habari na kipindi cha shilawadu(umbea) ni sawasawa basi hatuwezi kufikia muafaka

Nakupa tu dondoo kwamba kwenye tasnia ya habari kuna kuripoti habari na kutengeneza habari
Mayu akifa una RIPOTI kwamba amekufa
Lakini ukitaka amekufakufaje kwa undani zaidi inabidi utengeneze habari sasa kwa kuanza kukusanya taarifa...... iwapo hiyo taarifa yako ikitoka Mayu kafaje na wenye Mayu wao wakaona taarifa hiyo haina ukweli na inawachafua wanahaki ya kukushtaki mtengeneza taarifa

Huwezi kutengeneza li habari lako kwamba Mayu anakula nyama za watu kisha ukaenda kwa majirani na kuanza kuwahoji leading questions na wakasema ooh ndio tunamuonaga anapita na mifuko ina onekana ina nyama tena mida ya usiku kisha ukajustfy nakula nyama za watu

Kama umekiangalia kile kipindi majirani wenyewe hawajathibitisha kwamba menina kamuua mumewe isipikua ilikua ni mafununu ya kijinga kama “alikua anatoka asubuhi anarudi usiku kamtelekeza mgonjwa ndani”

Kuhusu youtube ukiupload ujinga unashtakiwa ulieupload kwenye chaneli yako sheria inakutaka kujisajili

Kama unadhani hii ni issue ndogo unajidanganya sana
Hadi sasa kipindi hakiendi tena hewani wanajitathmini upya

Kuna mamilioni ya kesi ambayo vyombo vya habari vilitengeneza habari ambazo hazikua za kweli na kuchafua watu wakalipa

Huwezi kutengeneza habari zako za kishenzi kisha ukatafuta washenzi wenzako ukawagoji kuchafua watu kisha ukajivua mzigo kisa umehoji wajinga wenzako
1.) Sijasema maudhui ya habari za ITV na maudhui ya habari za Shilawadu ni sawa, la hasha, bali nilichosema ni kwamba sioni connection ya ‘content’ za habari hizo na hoja hii, unless kama tayari una bias dhidi ya habari zinazoletwa kwa mtindo wa ‘kusherehesha’ hadhira, otherwise wote wanawasilisha taarifa kama wanavyozipokea toka kwenye vyanzo vyao, ila tu hawa Shilawadu wako artistic zaidi kwenye kuwasilisha taarifa zao, utangazaji ni sanaa, na ubunifu katika kuiteka hadhira ni muhimu, nikushauri uondoe kwanza bias uliyonayo dhidi ya wale wanaowasilisha habari kiubunifu zaidi (Kwa mtindo wa kusasambua).

2.) Hapo kwenye kutemgemeza habari ni kile tunachoita ‘investigative journalism’, na inaruhusiwa, kama tumepata taarifa kwamba Mayu amefariki, basi kwa mtimdo wa ‘investigative journalism’ tunalazimika kifanya uchunguzi na kukusanya taarifa toka kwa vyanzo vilivyopo, sasa tangu lini kufanya uchunguzi ikiwa kutengeneza tena habari? Yaani habari ipo tayari halafu useme tumeitengeneza? Kwa msingi upi udai hivyo? Chanzo kimoja wapo ni majirani, na hakuna ubaya kiwahoji maana wao ndio wapo karibu na eneo la tukio, ila kinachofanyika ni kukupigia simu ili kusikia upande wa pili wanasemaje, ila kwakuwa muhusika ni kiburi na hataki kuongea na waandishi wanaofanya utafiti na uchunguzi wa habari husika, then unawapa go ahead ya wao kurusha upande mmoja tu wa habari, halafu naadae wewe ndio utaamua ukanushenau otherwise, maana ulipewa chance kabla ila ukai-pass. Dstv wametimiza jukumu lao kwa wateja wao kwa kurusha taarifa ya majirani kama ilivyo, na hawawezi kuwajibika kwa yaliyosemwa na majirani, mnapoteza mida tu huko mahakamani. Kuuliza maswali ambayo wewe unahisi ni leading si kigezo cha wao kuitikia ndio wakati sivyo, ila mwandishi ni lazima utoe muelekeo wa mahojiano yako. Nasisitiza, DSTV hajatengeneza habari, na si kazi yake na haijawahi kuwa kazi yake, bali waliwasilisha habari kama ilivyokuwa na wakaichambua.

Pia nikuulize, hao majirani uliowaita WASHENZI kupitia JF, wakitaka kudai fidia kwa kuitwa WASHENZI, wataishtaki JAMIIFORUMS au watakutafuta wewe MAYU kwa msaada wa JF database ili ukajibu mashtaka mahakamani kwa kuwaita WASHENZ?
 
Mkuu umekazia hapohapo kuwashitaki majirani, hivi unaongea serious au unataka kuchekesha tu?
Sasa hapa nikujibu nini, maana sentensi yako haina hoja ndani yake, nachelea kusema unajaza server.
 
ngoja ashindwe kesi alafu atoe garama za kesi walioweka mawakili wao ndio atajua mahakama ni jehanamu.
DSTV wanaweza rightfully wakadai hizo bilioni 1.2 kwa kuharibiwa biashara kutokana na taswira yao kuchafuliwa, huyu lazima tumgeuzie kibao, we subiri tu. Maana DSTV TRA inaonekana wazi wanacholipa kinaendana na hayo mapato endapo yatapungua.
 
hapa ndo inakuja taaluma ya uandishi wa habari.. taarifa hua haichukuliwi tuu, hasa taarifa za kumtuhumu mtu, kosa si hao majirani tuu, ni media kusambaza habari ambazo pengine hazikuwa na uhakika!
.
.
kama kuna uhalisia kwenye hizo fedha alizopaswa kupewa, akipata mwanasheria mzuri hizi pesa anazichukua, swali linakuja Je kilichoenea kina ukweli?
Unaposema taarifa hua haichukuliwi tu una maana kwamba DSTV hiyo taarifa wameichukua tu? Au unamaanisha nini? Tangu lini mtu mwenye leseni kusambaza habari ikawa ni kosa? Kama habari ‘pengine’ si za kweli, aliyesema huo uongo si yupo na anafahamika?, shida iko wapi?
 
1.) Sijasema maudhui ya habari za ITV na maudhui ya habari za Shilawadu ni sawa, la hasha, bali nilichosema ni kwamba sioni connection ya ‘content’ za habari hizo na hoja hii, unless kama tayari una bias dhidi ya habari zinazoletwa kwa mtindo wa ‘kusherehesha’ hadhira, otherwise wote wanawasilisha taarifa kama wanavyozipokea toka kwenye vyanzo vyao, ila tu hawa Shilawadu wako artistic zaidi kwenye kuwasilisha taarifa zao, utangazaji ni sanaa, na ubunifu katika kuiteka hadhira ni muhimu, nikushauri uondoe kwanza bias uliyonayo dhidi ya wale wanaowasilisha habari kiubunifu zaidi (Kwa mtindo wa kusasambua).

2.) Hapo kwenye kutemgemeza habari ni kile tunachoita ‘investigative journalism’, na inaruhusiwa, kama tumepata taarifa kwamba Mayu amefariki, basi kwa mtimdo wa ‘investigative journalism’ tunalazimika kifanya uchunguzi na kukusanya taarifa toka kwa vyanzo vilivyopo, sasa tangu lini kufanya uchunguzi ikiwa kutengeneza tena habari? Yaani habari ipo tayari halafu useme tumeitengeneza? Kwa msingi upi udai hivyo? Chanzo kimoja wapo ni majirani, na hakuna ubaya kiwahoji maana wao ndio wapo karibu na eneo la tukio, ila kinachofanyika ni kukupigia simu ili kusikia upande wa pili wanasemaje, ila kwakuwa muhusika ni kiburi na hataki kuongea na waandishi wanaofanya utafiti na uchunguzi wa habari husika, then unawapa go ahead ya wao kurusha upande mmoja tu wa habari, halafu naadae wewe ndio utaamua ukanushenau otherwise, maana ulipewa chance kabla ila ukai-pass. Dstv wametimiza jukumu lao kwa wateja wao kwa kurusha taarifa ya majirani kama ilivyo, na hawawezi kuwajibika kwa yaliyosemwa na majirani, mnapoteza mida tu huko mahakamani. Kuuliza maswali ambayo wewe unahisi ni leading si kigezo cha wao kuitikia ndio wakati sivyo, ila mwandishi ni lazima utoe muelekeo wa mahojiano yako. Nasisitiza, DSTV hajatengeneza habari, na si kazi yake na haijawahi kuwa kazi yake, bali waliwasilisha habari kama ilivyokuwa na wakaichambua.

Pia nikuulize, hao majirani uliowaita WASHENZI kupitia JF, wakitaka kudai fidia kwa kuitwa WASHENZI, wataishtaki JAMIIFORUMS au watakutafuta wewe MAYU kwa msaada wa JF database ili ukajibu mashtaka mahakamani kwa kuwaita WASHENZ?
Nahakika hujakiona hicho kipindi ila umeamua KUBISHA tu
Tafuta uangalie halafu utajua naongea nini vinginevyo utakua una dhania tu kwamba wameripoti kama wanavyoripoti habari za haji manara akiita waandishi au Mama Samia akihutubia
Hakuna hata jirani mmoja alitoa fact ya alichoona kinafanyika ndani zaidi ya kudai alikua anachelewa kurudi nyumbani mara alikua anakula bata, sijui yupo bize na shooting yaani upuuzi mtupu

Kubalance stori pekee hakuhalalishi habari ya kumchafua mtu

Na kama ulikua hujui basi nakutaarifu ujinga wowote nitakao uandika humu jf basi jf wanawajibika nao kwa asilimia 100..... nchi hii ina sheria za kipuuzi sana za kubana media

Narudia tena huwezi kuja na habari ya kunichafua na kujikinga kwa mgongo wa watu utakao kwenda kuwahoji unapofanya habari zako za kiuchunguzi...... kama hawajajumuishwa kwenye kesi basi utawatumia kuja kuthibitisha kama kweli nakula nyama za watu au mlikua mnahojiana porojo
 
ICU na dstv kivipi

Wasafi ipo star times
Ipo azam
Ipo zuku
Ipo dstv
Ipo yaan

Why only dstv?

Mi nadhani angeshtki kipindi
 
Maudhui ni ‘Content’ kwa maneno mengine, sasa sijajua unamaana gani kuinkove concept ya maudhui katika hoja hii. Unaposema wametengeneza habari ni kwa msingi upi? Jambo limeibuka toka kwa majirani kwamba kuna moja, mbili, tatu, waandishi wa habari wakaingia kazini kufanya kazi yao, wakawapata hao majirani na kuwahoji, shida iko wapi? Sasa utasemaje wametengeneza, on what basis, kwa hisia na bias tu uliyonayo? Maoni / mtazamo/msimamo wa Magufuli kwamba chanjo ni hatari ndio tuhuma zenyewe hizo, sasa sijajua maoni/ mtazamo/ msimamo unatofauti gani na ‘tuhuma’ katika muktadha huo.

Analogy niliyokupa hivyo basi bado ni valid. Atakayeshtakiwa ni Rais Magufuli, na sio ITV. Maana siku nyingine hao wenye kipindi wataamua kukiupload Youtube baada ya mkataba wao na DSTV kuisha, mtawashtaki Youtube kwa kukirusha? Tumia akili unapotoa hoja, usitumie hisia wala mihemko, tumeelewana?
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahakika hujakiona hicho kipindi ila umeamua KUBISHA tu
Tafuta uangalie halafu utajua naongea nini vinginevyo utakua una dhania tu kwamba wameripoti kama wanavyoripoti habari za haji manara akiita waandishi au Mama Samia akihutubia
Hakuna hata jirani mmoja alitoa fact ya alichoona kinafanyika ndani zaidi ya kudai alikua anachelewa kurudi nyumbani mara alikua anakula bata, sijui yupo bize na shooting yaani upuuzi mtupu

Kubalance stori pekee hakuhalalishi habari ya kumchafua mtu

Na kama ulikua hujui basi nakutaarifu ujinga wowote nitakao uandika humu jf basi jf wanawajibika nao kwa asilimia 100..... nchi hii ina sheria za kipuuzi sana za kubana media

Narudia tena huwezi kuja na habari ya kunichafua na kujikinga kwa mgongo wa watu utakao kwenda kuwahoji unapofanya habari zako za kiuchunguzi...... kama hawajajumuishwa kwenye kesi basi utawatumia kuja kuthibitisha kama kweli nakula nyama za watu au mlikua mnahojiana porojo
Mi nadhani hadi hapa tumeshajadili kila kinachoweza kujadilika, tukiendelea itakuwa tunarudia rudia tu mambo yale yale.Tuishie hapa.
 
Nahakika hujakiona hicho kipindi ila umeamua KUBISHA tu
Tafuta uangalie halafu utajua naongea nini vinginevyo utakua una dhania tu kwamba wameripoti kama wanavyoripoti habari za haji manara akiita waandishi au Mama Samia akihutubia
Hakuna hata jirani mmoja alitoa fact ya alichoona kinafanyika ndani zaidi ya kudai alikua anachelewa kurudi nyumbani mara alikua anakula bata, sijui yupo bize na shooting yaani upuuzi mtupu

Kubalance stori pekee hakuhalalishi habari ya kumchafua mtu

Na kama ulikua hujui basi nakutaarifu ujinga wowote nitakao uandika humu jf basi jf wanawajibika nao kwa asilimia 100..... nchi hii ina sheria za kipuuzi sana za kubana media

Narudia tena huwezi kuja na habari ya kunichafua na kujikinga kwa mgongo wa watu utakao kwenda kuwahoji unapofanya habari zako za kiuchunguzi...... kama hawajajumuishwa kwenye kesi basi utawatumia kuja kuthibitisha kama kweli nakula nyama za watu au mlikua mnahojiana porojo
tatizo unatumia hisia sana katika tukio hili, kiukweli kama ni kesi angepewa prince wa uingereza na mke wake pale walipoituhumu royal family. Lakini upande wa pili walijisafisha kwa kukanusha madai hayo hadharani kupitia vyombo vya habari. Kifupi hapo hakuna kesi ni kujisumbua tu na wanaweza kumgeuzia kesi yeye.
 
Hoja yangu na bwana Don haikuwa kama kuna kesi au hakuna, wala haikua kama atashinda au atashindwa

Hoja ilikua kupinga madai ya Don kwamba Menina ameshitaki watu wasio sahihi, eti alitakiwa kuwashitaki majirani walio hojiwa

Wewe unadai dstv inarusha Itv clouds wasafi nk
Lakini kumbuka kuna vipindi vipo chini ya Dstv na kuna vipindi vinarushwa via Dstv
 
Hii yote ni muendelezo comedy za bongo movie, nitamtumia mwanasheria wangu kumpeleka mahakamani, mara mwanasheria wangu sijui nini mwisho wa siku hakuna lolote. Hapo unakuta kuna mjanja mmoja anampiga hela dada wa watu akimpa matarajio lukuki. Dada akija kutahamaki kashapigwa kibunda cha kutosha na hakuna matokeo.
 
Mkuu kuna mambo mengi nyuma ya pazia zaidi ya haya tunayoyaona kwenye IG

Hapo inawezekana pia ni fursa kwa Menina, wajuaji wa sheria wanaweza kumpa ramani akashtaki kisha Dstv wakiona tusisumbuane wanamalizizana naye kimya kimya anapewa vimilioni vyake kadhaa anagawana na wakili wake ananunua Toyota crown used maisha yanaendelea

Watu tunamdharau Menina sababu ya CV yake mbovu lakini haya mambo wapo wanasheria wanaisimamia bure kwa makubaliano wakishinda wanakula asilimia zao........ wanachofanya ni kuhakikisha kesi ina ground nzuri za kushinda
 
siyo kwa kesi hii ndg yangu. Zipo kesi kama ile ya majani, Ay na FA lakini hii hapana hata kama sina utaalamu wa sheria sioni kesi mkuu.
 
Mkuu haya ni maoni yetu tusubiri yajayo

Lakini most likely Shelukindo atamuita Menina watayajenga kimya kimya yataisha
Hakuna kampuni inayopenda kuchafua cv yake kwa kushtakiwa shitakiwa

So far naona na kipindi chenyewe kimesimamishwa baada ya sakata hili
 
sawa ila hakuna pesa rahisi.
 
Hoja yangu na bwana Don haikuwa kama kuna kesi au hakuna, wala haikua kama atashinda au atashindwa

Hoja ilikua kupinga madai ya Don kwamba Menina ameshitaki watu wasio sahihi, eti alitakiwa kuwashitaki majirani walio hojiwa

Wewe unadai dstv inarusha Itv clouds wasafi nk
Lakini kumbuka kuna vipindi vipo chini ya Dstv na kuna vipindi vinarushwa via Dstv
Wewe unataka tuanze upya sasa, kama unasema amewashtaki watu walio sahihi iweje tena hoja isiwe kama kuna kesi au la? Unaweza ukashtaki watu walio sahihi halafu pasiwe na kesi? Anyway, ukijibu mtu mjibu kivyako, usinitaje, maana nimeshachoka sasa.
 
😂😂😂😂😂
Mkuu unapenda sana ligi wewe

Muheshimiwa alinukuu post yangu bila kujua msingi wa tofauti ya hoja zetu
 
Back
Top Bottom