Mkuu vaa suti ikuvutie wewe, sio mwanamke. The rule of thumb: hata siku moja usinunue suti kwa ajili ya kumfurahisha mwanamke. Nilishawahi kuuliza wanawake wa hapa hapa JF kama walishawahi kutovutiwa na mwanaume aliyevaa suti iliyomkaa. Sikupata jibu. So, nunua na vaa suti inayokutosha kulingana na unapoenda.
Kumbuka kuvaa suti si lazima tuu kumvutia mwanamke. Otherwise, wanaume wote wanaovaa jeans wangekuwa hawawavutii wanawake. There is something more in a man which attract a woman than a suti. Pia suti inaweza kukufanya uonekane nadhifu na mwenye heshima ndani ya jamii kwa ujumla.
Tatizo ambalo huwa naliona ni kuvaa suti visivyo. That is the big big problem. Zipo sheria sheria ambazo zinatakiwa kuzifuatwa unapovaa suti. Kama hutafuata hizi sheria unaweza kujikuta upo matatani kwa kuvunja moja ya sheria hizo. Sheria zenyewe ambazo nimezinyakua mahali ni kama ifuatavyo. Unapovaa suti au tai hakikisha huvunji sheria hizi hapa chini:-
1. Ni marufuku kuvaa kandambili au malapa
2. Ni marufuku kuvaa soksi mbovu.
3. Ni marufuku kujisaidia uchochoroni.
4. Ni marufuku kupenga kamasi barabarani.
5. Ni marufuku kupanda daladala.
6. Ni marufuku kuendesha baiskeli au pikipiki.
7. Ni marufuku kucheka cheka hovyo.
8. Ni marufuku kuomba change dukani.
9. Ni marufuku kubeba mfuko wa plastiki maarufu kama rambo
10. Ni marufuku kuingia kwenye kibanda cha simu.
11. Ni marufuku kula magengeni.
12. Ni marufuku kuonekana unatafuna barabarani.
13. Ni marufuku kutembea na pesa za sarafu mifukoni mwako.
12. Ni marufuku kulia hata kama umeletewa taarifa ya msiba.
14. Ni marufuku kupiga miruzi.
15. Ni marufuku kuonekana unatoka mijasho kama unasukuma mkokoteni.
16. Ni marufuku kuongea kwa kelele.
17. Ni marufuku kunywa chai au kahawa kwa kutumia kikombe cha plastiki.
18. Ni marufuku kutembea kwa miguu.
19. Ni marufuku kukimbia.
20. Ni marufuku kunuka mdomo wala kikwapa hili kosa kubwa sana na hukumu yake mpaka mbinguni ipo.
21. Ni marufuku kusema uongo.
22. Ni marufuku kuonekana umekasirika unatakiwa uwe na uso uliokunjuka.
23. Ni marufuku kumchapa mtoto.
24. Ni marufuku kusababisha ubishi au mjadala usio na maana (hata hapa JF).
25. Ni marufuku kuvaa suti na lebal yake (hii nimeongezea)
Source:
HABARI NA MATUKIO: ZIJUE SHERIA ZA UVAAJI WA TAI NA SUTI
Kama huwezi kuzifuata hizo sheria, stick with the jeans, which is my favorite.