Messi aitunishia misuli Serikali ya Israel, Serikali yafyata

Messi aitunishia misuli Serikali ya Israel, Serikali yafyata

Kwanini Messi akatae halafu aseme atarudisha gharama za mechi? au Messi akikataa ndiyo Argentina imekataa? By the way huo mji wa Jerusalem kwa sasa si unatumiwa na wote wayahudi na wapalestina? Ina maana Messi anawaondolea hao waisrael haki ya kutumia sehemu ya mji wanayoimiliki?
Let us see, maana hao jamaa hawakawii kuanza kumshughulikia ili kumshusha na kumuondolea udhamini kupitia makampuni yao yanayomdhamini Messi. Nadhani hakujua ukubwa wa vita anayoiingia na kama angeijua sidhani kama angethubutu.
Mchezo wa soka umebeba hisia kali sana kwa mashabiki na kwa wanasoka wenyewe!!!!.....

Kila mwenye akili timamu anajua jinsi gani suala la Jerusalem lilivyo kwenye tension kubwa sana kihisia kwa kila mpenda amani na ubinaadamu....!!!!

Messi ni miongoni mwa wanasoka wenye mashabiki wengi sana ulimwengu kutoka kila pembe ya dunia....hivyo muungwana huwa anajali hisia za wengine na sio kujijali yeye binafsi!!!!.....

Messi hakukataa kushiriki mechi hiyo amekataa kucheza mchezo huo kwenye ardhi ya Jerusalem kinyume na makubaliano yaliyopangwa mwanzo!!!!
 
Samahani mkuu unafikiri nani anasababisha Israel wanapendelewa hivyo? Unataka kuniambia America wanapata nini kutoka Israel kwa huo upendeleo?
Anayesababisha ni Marekani mwenyewe kwa faida yake...

Kwa mfano, mkataba niliogusia ulikuwa unaitaka Israel kutumia 75% ya msaada kununua vifaa vya kijeshi toka USA! Kwa maana nyingine, kiwango kikubwa cha misaada ya US kwa Israel kinarudi US kwenyewe!

Sasa umeshapata kujiuliza mataifa mengine yasiyojisikia salama dhidi ya Israel na yenyewe yatakavyolazimika kutumia billions kununua vifaa vya kijeshi toka US ili kujilinda dhidi ya Israeli?

In other way round, kadri Israel inapojiimarisha kijeshi kupitia US, nchi kama Iran unaipa pressure na hivyo na wao kuamua kujiimarisha kutokea Russia!

Iran ikinunua vifaa vya kijeshi toka Russia or elsewhere; lazima amtie pressure Saudi Arabia ambae nae ataamua kujiimarisha kwa kununua vifaa vya kijeshi toka US!

Ni kutokana na hiyo triangulation ndio maana haishangazi kuona Saudi Arabia wanatumia pesa nyingi sana kununua vifaa vya kijeshi toka USA!

Huo upande mmoja. Kingine: je umewahi kusikia kitu kinaitwa WRSA-I; yaani War Reserve Stockpile Ammunition-Israel?

Kama hujawahi kusikia, hiyo ni kama ghala la Kijeshi la Marekani lililopo Israel na lina kila kitu kinachohitajika kwa vita!

Hii maana yake nini? Leo hii US au Mshirika wake wa kijeshi akitaka kumshambulia Iran; hana haja ya kwenda US kukusanya mzigo kwa ajili ya kuingia vitani kwa sababu tayari wana stock ya kutosha waliyoiweka Israel!

That having said, msaada ni mkubwa kv Israeli inatumika pia kama ghala la US!

Aidha kuna siku niliwahi kuelezea hapa; ukiacha simulizi za kutaka mafuta, ni kwanini US wanang'ang'ania Middle East!

Nikasema kwamba, Middle East ni makutano ya world's military superpowers... yaani Russia & US!

Ukisoma jinsi Soviet ilivyokuwa inajitanua enzi hizo, ilikuwa tayari imeshaimeza West Asia na ilikuwa inakuja Middle East. Ni kutokana na hilo ndio maana yapo mataifa ya Kiislamu kutoka West Asia ambayo yalikuwa sehemu ya Soviet Union!

So, ili US kui-block Soviet isijitanue zaidi; wakalazimika kupiga kambi Middle East na kudumisha uhusiano na washirika wake!

Inafahamika, ni Israel na Saudi Arabia ndio washirika wakubwa eneo hilo!

Bila shaka hata kama wewe ungekuwa ndie mwenye maamuzi ndani ya US halafu unatakiwa uwekeze wapi mabilioni ya US kati ya Israel na Saudi Arabia ili kuendeleza ushawishi wako ndani ya Middle East; bila shaka ungeamua kuwekeza Israel badala ya Saudi Arabia!

Lakini pia usisahau what's so called War in Terror. Kwa miaka nenda rudi; CIA wamekuwa wakiitumia sana Pakistan's Inter-Intelligence Service; yaani ISI!

Hata hivyo, hivi sasa US hawaiamini sana ISI kwa sababu baadhi ya maofisa wake ni ma-extremists!

Ni hawa maofisa ndio ambao pia walisababisha zoezi la kumsaka Osama bin Laden kuwa gumu kwa sababu walikuwa wanavujisha taarifa kwa Al Qaeda!

Kutokana na hilo, ni Mossad pekee ndio wanaoweza kuaminika na US/CIA kwenye ukanda wa Middle East katika kufanya intelligence sharing!!

That having said, ukipenda mtoto sharti upende na mamake na ili watimize majukumu yao ni lazima uwagharamie!
 
Suala la amani ya palestina [emoji1193] na Israel [emoji1134] ukiliangalia kiubinaadamu basi halina udini, haijaalishi uwe muislam, mkristo, myahudi, mhindu au mpagan, but ukiangalia wanaopinga messi kutokwenda Jerusalem unajua kabisa wanapinga kichuki, nani asiejua kuwa kunafanywa unyama na ukatili kila siku kwa kuuwawa watu, unafkiri kuna wakiristo hayaumi wanaofanyiwa wapalestina?? Unafkiri kuna watu ambao wako nje ya dini ya kiislam hayawaumi yanafanyika pale??? Ndio maana ata taifa la Venezuela [emoji1263] na mataifa mengine ambayo sio yakiislamu huwa yanapinga ukatili unaofanywa na izrail, hakuna asiejua uchafu unafanywa pale tuache unafiki. Wanatumia nguvu kubwa kwa kificha maovu, eti mpaka wanalazmisha miji kuwa mikuu,eti na mataifa mengine yafuate yasipofuata vikwazo tehhhh, yaani vichekesho tu.
 
img_20180606_153825_5802146045410.jpg


Inasemekana timu ya taifa ya Argentine imefutilia mbali mchezo wao wa kirafiki dhidi ya taifa la Israel. Taifa hilo lilipata ripoti kwamba Lionel Messi na mke wake walipokea vitisho kutoka kwa wapalestine wakiwataka kuahirisha mchezo huo mara moja.

Katibu mkuu wa chama cha soka cha Palestina Jibril Rajoub aliuomba uongozi wa chama soka cha argentine kufuta mchezo huo mara moja

Baadhi ya mashabiki wa Messi nchini Palestina walichoma jezi za nyota huyo mara baada ya kikosi hicho kuwasili Jerusalem kwa muda.

Rajoub amesema anafahamu wazi kuwa mchezo huo ulikuwa ni wa kusheherekea Miaka 70 ya shirikissho la soka nchini humo.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwasiliana na Rasi wa Argentine Mh Mauricio Macri. Netanyahu alimsihi Sana Macri kuwahimiza uongozi na wachezaji kutokufutilia mbali mchezo huo siku ya jumanne. Macri alimjibu waziri huyo kuwa yeye hawezi kuingilia maamuzi ya mwisho ya chama cha soka cha taifa hilo.

Raisi Macri aliwasiliana na uongozi wa chama cha soka kujua msimamo wao. Viongozi walimwambia kuwa kila mchezaji ana hofu na hakuna mchezaji ambaye yupo tayati kucheza pambano hilo. Macri alimpigia simu waziri wa Israel na kumuomba radhi kwamba hakuna mchezaji ambaye atakubali kucheza pambano hilo.

Macri mwenyewe alikuwa tayari kwenda katika mpambano baada ya kualikwa na matajiri wa kiyahudi wanaofanya kazi.

Mchezaji wao Gonzalo ” Nashukuru kwa maamuzi hayo Kwa ajili afya zetu na maisha yetu. Hakukua na haja ya kucheza na wayahudi.

Hata hivyo Uongozi wa chama cha soka cha Israel kimishtumu sana maamuzi ya Rajoub na kusema amevunja mipaka.

Waziri wa Ulinzi wa israel Avigdor Lieberman amelaani kitendo hicho na kudai kuwa Wapalestina wamejaa chuki na wivu.

Msemaji wa wizara ya ulinzi Gilad Erdan alionhelea suala hilo na kusema kwamba

wamekuza jambo hilo kwa makusudi ili kumtisha Messi. Amesema kitendo cha kuchoma jezi za nyota huyo ni mipango ya taifa hilo kutaka kuondoa amani.
 
Mkuu hebu rudia tena!! Who is nani!!??

Mie sitaki kujihusisha katika siasa za huko nikawa myahudi wa bongo, ila hapo kwenye who is messi nenda kamuulize ibrahimovic ama kamtafute icardi halafu ndio umuulize who is messi.
Tafakari kwanza nlchoandika,ibracadabra na icardi wanahusika vp na topic ya hapa?
 
Messi na Timu yake wamefanya jambo jema.
Ila wasiwe double standard kwa swala la watoto wengi wa Mataifa ya Kiarabu ambao wameuwawa kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Uhalifu ni uhalifu tu bila kujali umefanywa na baba au mama mzazi wa mtoto.
 
Back
Top Bottom