Samahani mkuu unafikiri nani anasababisha Israel wanapendelewa hivyo? Unataka kuniambia America wanapata nini kutoka Israel kwa huo upendeleo?
Anayesababisha ni Marekani mwenyewe kwa faida yake...
Kwa mfano, mkataba niliogusia ulikuwa unaitaka Israel kutumia 75% ya msaada kununua vifaa vya kijeshi toka USA! Kwa maana nyingine, kiwango kikubwa cha misaada ya US kwa Israel kinarudi US kwenyewe!
Sasa umeshapata kujiuliza mataifa mengine yasiyojisikia salama dhidi ya Israel na yenyewe yatakavyolazimika kutumia billions kununua vifaa vya kijeshi toka US ili kujilinda dhidi ya Israeli?
In other way round, kadri Israel inapojiimarisha kijeshi kupitia US, nchi kama Iran unaipa pressure na hivyo na wao kuamua kujiimarisha kutokea Russia!
Iran ikinunua vifaa vya kijeshi toka Russia or elsewhere; lazima amtie pressure Saudi Arabia ambae nae ataamua kujiimarisha kwa kununua vifaa vya kijeshi toka US!
Ni kutokana na hiyo triangulation ndio maana haishangazi kuona Saudi Arabia wanatumia pesa nyingi sana kununua vifaa vya kijeshi toka USA!
Huo upande mmoja. Kingine: je umewahi kusikia kitu kinaitwa WRSA-I; yaani War Reserve Stockpile Ammunition-Israel?
Kama hujawahi kusikia, hiyo ni kama ghala la Kijeshi la Marekani lililopo Israel na lina kila kitu kinachohitajika kwa vita!
Hii maana yake nini? Leo hii US au Mshirika wake wa kijeshi akitaka kumshambulia Iran; hana haja ya kwenda US kukusanya mzigo kwa ajili ya kuingia vitani kwa sababu tayari wana stock ya kutosha waliyoiweka Israel!
That having said, msaada ni mkubwa kv Israeli inatumika pia kama ghala la US!
Aidha kuna siku niliwahi kuelezea hapa; ukiacha simulizi za kutaka mafuta, ni kwanini US wanang'ang'ania Middle East!
Nikasema kwamba, Middle East ni makutano ya world's military superpowers... yaani Russia & US!
Ukisoma jinsi Soviet ilivyokuwa inajitanua enzi hizo, ilikuwa tayari imeshaimeza West Asia na ilikuwa inakuja Middle East. Ni kutokana na hilo ndio maana yapo mataifa ya Kiislamu kutoka West Asia ambayo yalikuwa sehemu ya Soviet Union!
So, ili US kui-block Soviet isijitanue zaidi; wakalazimika kupiga kambi Middle East na kudumisha uhusiano na washirika wake!
Inafahamika, ni Israel na Saudi Arabia ndio washirika wakubwa eneo hilo!
Bila shaka hata kama wewe ungekuwa ndie mwenye maamuzi ndani ya US halafu unatakiwa uwekeze wapi mabilioni ya US kati ya Israel na Saudi Arabia ili kuendeleza ushawishi wako ndani ya Middle East; bila shaka ungeamua kuwekeza Israel badala ya Saudi Arabia!
Lakini pia usisahau what's so called War in Terror. Kwa miaka nenda rudi; CIA wamekuwa wakiitumia sana Pakistan's Inter-Intelligence Service; yaani ISI!
Hata hivyo, hivi sasa US hawaiamini sana ISI kwa sababu baadhi ya maofisa wake ni ma-extremists!
Ni hawa maofisa ndio ambao pia walisababisha zoezi la kumsaka Osama bin Laden kuwa gumu kwa sababu walikuwa wanavujisha taarifa kwa Al Qaeda!
Kutokana na hilo, ni Mossad pekee ndio wanaoweza kuaminika na US/CIA kwenye ukanda wa Middle East katika kufanya intelligence sharing!!
That having said, ukipenda mtoto sharti upende na mamake na ili watimize majukumu yao ni lazima uwagharamie!