Messi apiga mbili Barcelona ikiizamisha madrid 3-2 bernabeu,

Royal Warrior

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
1,166
Reaction score
2,143

========


LIONEL Messi akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Barcelona katika ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Real Madrid katika mchezo mkali wa ligi ya La Liga uliochezwa usiku huu huko Santiago Bernabeu.

Real Madrid ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya kiungo wako Casemiro kufunga bao akimalizia mpira na Sergio Ramos uliogonga mwamba na kumkuta mfungaji.

Lionel Messi aliisawazishia bao hilo Barcelona dakika chache baadae baada ya kuwalamba chenga walinzi wawili wa Real Madrid na kufyatua mkwaju uliopita chini ya mikono ya kipa,Keylor Navas na kutinga wavuni.
Ivan Rakitic aliifungia Barcelona bao la pili kwa mkwaju wa mbali kabla ya mtokea benchi James Rodriguez kuifungia Real Madrid bao la kusawazisha.

Mchezo ukiwa unaelekea ukingoni Lionel Messi aliifungia Barcelona bao la tatu na la ushindi akiunganisha pasi ya mlinzi Jordi Alba aliyekuwa amegongeana vyema na kiungo Mreno,Andre Gomes.

Ushindi huo umeipeleka Barcelona kileleni baada ya kufikisha pointi 75 sawa na Real Madrid yenye mchezo mmoja.Barcelona ina mabao mengi ya kufunga.

Aidha katika mchezo huo Real Madrid ililazimika kumaliza ikiwa na wachezaji kumi (10) baada ya nahodha wake Sergio Ramos kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kosa la kumkwatua Lionel Messi aliyekuwa mwiba mkali.
 
ukizingatia Neymar hatacheza leo, maana yule ndo mpandisha timu..
hvyo Carvajal atapanda sana juu kuishambulia barca so leo R. madrid anaweza akashinda zaidi ya goal 3
 
yaaan ngoja nkawahi siti ya mbele kabsaa maana madrid navyomjua akishapgwa goli huwa anapata hasira ndo utamjua yaan inakua kama umefungulia nyuki so leo barca ajipange
 
Subiri elclassic ijayo labda mkuu
 
Mpira unadunda lakn mesi anadundisha! Mpira ni mchezo wa wazi lakn sio kwa style hii! [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Ahhahahahaahahahaha
Laliga mess
Uefa C.R
 
Huwezi mfananisha na mchezaji mwingine kwa dunia ya sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…