Messi apiga mbili Barcelona ikiizamisha madrid 3-2 bernabeu,

Messi apiga mbili Barcelona ikiizamisha madrid 3-2 bernabeu,

Mchezaji bora duniani ni C Ronaldo kwa kuwa Messi si wa Sayari hii
 
Nlishakata tamaa nikaenda kulala nikiamini bao ni 2-2 messi ananikumbusha zaman kwenye gazeti moja alikuwepo mchezaji mmoja anaitwa CHONKA. alikuwa balaa sana. Yule alikuwa akicheza mpira wa kudaiwa huko majuu. Na huyu messi wamchunguze vizuri anaweza kuwa ni ALIEN. si kwa aina hii ya mpira na kutokata tamaa. Jamaa hachezi mpira. ANAUCHEZEA MPIRA
 
Mechi zijazo inasemekana kuna uwezekano Mkubwa Real Madrid wakakataa L. Messi acheze. Wanasema huyu asiwe anacheza mechi zao maana alianza kucheza mpira toka siku amezaliwa
 
Vp goli la kwanza la R.Madrid? Haikuwa offside jaman? Wenye ujuz plz!!
Haikuwa offside. Ramos ambaye ndiye aliyeupata mpira alokuwa line moja na beki wa Barca. Wengine watatu wa madrid walikuwa mbele lakini hawakuupata.
 
ukizingatia Neymar hatacheza leo, maana yule ndo mpandisha timu..
hvyo Carvajal atapanda sana juu kuishambulia barca so leo R. madrid anaweza akashinda zaidi ya goal 3
[emoji12]
 
Ligi tunachukua na uefa pia tunachukua!! Nyie si mlipigwa tatu bila uefa mkatolewa??
Hata ninyi mwaweza tolewa na ubingwa wa laliga msiupate hakuna timu inayoenda na matokeo uwanjani
 
Niliichukia Real Madrid baada ya kuwatoa Bayern Munich kwa kubebwa hapo Bernabeu,na kiukweli nimefurahi kufungwa kwao na Barca ingawa sio mpenzi wa Barca.

Lakini kuna tofauti katika hivi vikosi,Madrid Wengi wa wachezaji wake ni Wazee na wameshachoka baada ya kufikia kilele cha mafanikio,Ronaldo hana njaa tena na ameridhika na mataji na mataji binafsi na record alizoweka au kuvunja na umri pia umeshamtupa mkono kimpira,mara nyingi wanashinda kutoka na Ujuzi binafsi na Uzoefu,hawana Mpira wa kutisha kama tulivyoizoea Real Madrid kwa misimu miwili mitatu iliyopita walipokuwa kwenye peak,then bado Zidane ana mbinu za kizamani katika ufundishaji wake,mifumo ya miaka ya 2000's ya Uingereza,Timu yake haina radha ya Mpira magoli mengi ni ya either kuvizia or counter attack,ndio mana Perezi pamoja na kushinda Kombe la UEFA bado hajaridhishwa na kiwango cha Zizou katika ufundishaji,Zidane sio muumini wa wachezaji Wenye Vipaji ndio mana unaona Mtu kama Hames Rodriguez akiwa banch au Morrata huku Benzema akipata nafasi kwenye kikosi chake.

Kwa Upande wa Barcelona,nayo now wanajijenga upya baada ya kuanguka katika msimu ya hivi karibuni,baada ya kuondoka Pep Gurdiola Barcelona ilipoteza ufalme wake bara ni Ulaya,wachezaji wengi waliokuzwa pale wameuzwa au kumfata Pep mfano Pedro,Alcantra n.k,so timu imekosa warithi wa Xavi,Iniesta,Mess,hivyo sasa kutegemea Zaidi Miujiza ya Mesi kama alivyofanya jana.

Hawa Watu watatu Xavi,Iniesta na Mess peke yao walikuwa na uwezo wa kupiga pasi si chini ya 600 per game.

Game na Man united pale Wembley walipiga pasi Zaidi ya 1000 huku Xav peke yake akipiga pasi si chini ya 400,utaona hiyo kasi,nguvu na skills hadi Fegurson akatetemeka, hakuamini kilichokuwa kinafanyika uwanjani utafikiri Play station.

Mess akienda ukingoni mzigo mkubwa unahamia kwa Neymar,na ndio mana nao sasa wanaingia sokoni kutafuta wachezaji badala la kutegemea la Masia kuziba nafasi za wakongwe na kurudisha soka lao la pasi nyingi.

Kiwango cha jana cha Mess ni hasira baada ya kushindwa kuperform kwenye game ya Juve na alijuwa udhaifu wa timu yake na Mzigo alioubeba.

Sitoshangaa kuja kwa Coutihno pale Barca,Griezman au hata Hazard kama watakuwa na mfuko mrefu.
 
Hata ninyi mwaweza tolewa na ubingwa wa laliga msiupate hakuna timu inayoenda na matokeo uwanjani
La liga ubingwa ni wetu! Uefa bado tupo na nyie mmetolewa kwa kupigwa tatu bila! Hiyo ni fact mkuu!!
 
La liga ubingwa ni wetu! Uefa bado tupo na nyie mmetolewa kwa kupigwa tatu bila! Hiyo ni fact mkuu!!
Haya na jana mmeshinda, hiyo la liga wenzio tushaizoea maana inataka kuhamia kwetu kabisa ndio maana nyinyi mnahangaika nayo mna miaka kibao haja chukua!!! Lkn pia kutoka kwetu uefa haipunguzi machungu ya kuwafunga jana tena kwenu
 
Haya na jana mmeshinda, hiyo la liga wenzio tushaizoea maana inataka kuhamia kwetu kabisa ndio maana nyinyi mnahangaika nayo mna miaka kibao haja chukua!!! Lkn pia kutoka kwetu uefa haipunguzi machungu ya kuwafunga jana tena kwenu
Kwekwekwekwekwee hahahaahaaaa jipe moyo!! Uefa tunabeba na laliga tuna inyakua!! Infact mmezoea kubebwa!!

Ivi ni timu gani imebeba uefa mara nyingi zaidi??
 
Back
Top Bottom