Messi aumia kwenye mchezo wa ligi wiki chache kuelekea Kombe la Dunia, Waargentina wajawa na hofu

Messi aumia kwenye mchezo wa ligi wiki chache kuelekea Kombe la Dunia, Waargentina wajawa na hofu

Meja Jenerali Isamuhyo

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
3,709
Reaction score
10,896
Lionel Messi, nahodha wa Inter Miami na Argentina jana aliumia kwenye mchezo wa ligi ya MLS.

Messi alitolewa dakika ya 73 na kuelekea moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo huku akishika mguu wake.

Hii inatokea wiki chache kabla ya mashindano makubwa ya World Cup.

Jeraha la Messi limeibua hisia tofauti hasa nchini Argentina hofu imetanda kwa baadhi ya mashabiki wa taifa hilo kwa nahodha wao.

Klabu yake ya Inter Miami haijasema bado ukubwa wa jeraha la Messi na namna gani litamweka nje ya uwanja kwa muda gani.

Je, Messi atakosa kombe la dunia? Tusubiri na tuone…
 
Kazi na umri.
Umri ukisogea majeraha hayachezi mbali na wewe.
Apone haraka aje aburudishe Dunia kwa vyenga vyake
 
Jamaa akapumzike sasa.

Kwenye soka amemaliza kila kitu.

Hakuna anachodaiwa.

It's time to leave.
 
Back
Top Bottom