Messi Messi Messi

Wapi Messi leo coni matobo naona vitu adimu tu toka kwa le brazilian "Marcelo" hahahahaha.
Hahahahahah...
Marcelo kacheza kwa sababu alikua huru... Kiumbe wa AJABU MESSI alienda kati kupambana na kuzima mashambulizi ya kroos, modric na isco
 

Inamaana kaka ulishindwa kuona kwamba MESSI Jana alicheza katikati!? (Japo mwanzo alianza pembeni)

Alicheza kati ili apambane na kuzuia uanzishaji wa mashambulizi toka kwa Isco, Kroos na Modric... Siyo kwamba alikua mkabaji hapana Bali uwezo wake wa kukaa na mpira mguuni muda mrefu uliwazima vijana wa galacticos..

Messi alifanya kazi kubwa ya kuwazuia wale watu wasionekane, na ndio maana mashambulizi ya Madrid yalianzia/kupitia pembeni Mara nyingi...

Messi akiwa kama mchezaji wa kati(kiungo wa juu) aliwapa pasi nyingi sana Suarez na Neymar ila hawakua makini sana..

Mwisho... Messi ni kiumbe wa ajabu huyu kazaliwa hapa duniani lakini ana mpira wa baadae sana..

Hongera MESSI
 
Inamaana kaka ulishindwa kuona kwamba MESSI Jana alicheza katikati!? (Japo mwanzo alianza pembeni)
Kwanini acheze katikati wakati viungo wapo?
Alicheza kati ili apambane na kuzuia uanzishaji wa mashambulizi toka kwa Isco, Kroos na Modric... Siyo kwamba alikua mkabaji hapana Bali uwezo wake wa kukaa na mpira mguuni muda mrefu uliwazima vijana wa galacticos..
Kumbe mnawaogopa eeeh?
Mwisho... Messi ni kiumbe wa ajabu huyu kazaliwa hapa duniani lakini ana mpira wa baadae sana..
Hapa umetudanganya.

Hoja yangu ni kwamba kama messi ni bora kama wewe unavyosema mbona hakufurukuta? na kwanini acheze kama kiungo wakati yeye by nature ni forward? christiano alifunga goli je messi alifunga ngapi? huo ubora unaousemea wewe unaonekana kama akikutana na vitimu vidogo na si vinginevyo!!! messi ni mchezaji mzuri ila hamkuti cr7 kwa ubora!!
 

Wapi nimedanganya!???

Mpira siku hizi umebadilika sana.. Hakuna tena mambo ya Mimi ni namba sita/tano/Tisa... Tunaangalia majukumu ambayo kocha anakupangia(na hiki ndicho kilicho tokea kwa messi ktk hiyo mechi...) Na sio kwamba hao akina isco wanaogopwa Bali ule ni mpira na ushindi ni muhimu... Utapataje ushindi sasa, kwanza inabd uzuie vema wapinzani(KWA MADRID ILIBIDI KUWAZUIA AKINA KROOS... NA MESSI ALIWEZA) pili inabidi utengeneze nafasi ili upate ushindi(MESSI PIA ALISAIDIA.. ASSIST MOJA, NA PASI NYINGINE KIBAO AMBAZO NEYMAR HAKUWA MAKINI NAZO)

Wewe ulitaka kocha aache Rakitic apambane na isco, kroos na Modric!??? Ni wazi wangemzidi.. Kumbuka xavi hakuwepo so jukumu la kuwadhibiti hawa alipewa kiumbe wa ajabu MESSI.. NA ALIWEZA

Nimegundua ww ni RMA fan.. Ila mm sio wa Barca bali nazungumza mpira halisi

Assist ile ilikua kazi tosha kumfanya Messi aendelee kuwa mbabe kwa sasa
 
Huwezi kumpima kwa mechi moja tu. Kama kigezo ni magoli kuna siku walikutana na madrid na CR akiwemo mess akawapiga hatrick kitu ambacho cr mpaka leo hajakifanya. CR akiwa porto aliicheza mechi 25 akafunga magoli 3, akiwa utd alicheza mechi 196 akafunga magoli 84 akiwa madrid amecheza karibu mechi 190 na ana magoli 208 katika mechi zote hizo(411) amefunga magoli 295 wastani wa magoli kwa mechi ni 0.72. Messi mpaka sasa hivi amecheza mechi 304 na ana magoli 275 wastani wa magori kwa mechi ni 0.91. CR ni mzuri lakini hajamfikia mesi.
 
Si kweli.
 

Kaka, Shkamoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…