Linapokuja suala la mchezaji bora, ni vigezo vingi vinaangaliwa, sio idadi ya magoli peke yake. Ndio maana wakaweka tuzo ya mfungaji bora, na tuzo ya mchezaji bora.
Wanaosema Messi hakustahili tuzo ya mchezaji bora, ni watu wachache ambao wameumizwa na ushindi wa Argentina hapo jana.
Angalia hizi takwimu za Messi, alafu ulete takwimu za mchezaji wako unaedhani alitakiwa kupewa tuzo ya mchezaji bora ili tulinganishe!
Leonel Andres Messi "Cuccittini"
- Goals 7 : second
- Assists 3 : first
- Total shots 32 : first
- Shots on target 18 : first
- Chances created 21 : second
- Dribbles completed 15 : third
- Duels won 44 : third
- Touches in opposition box 45 : second
- Passes played into the box 39: second
Ukiwa sio mtu wa mpira, hauwezi kujua mchango wa mchezaji tofauti na magoli anayofunga. Ila watu wa mpira wanajua, kuna mengi yanafanyika uwanjani yanayoweza kuamua ubora wa mchezaji, na sio magoli pekee!
Namba hazidanganyi. Leta takwimu za mchezaji wako unaedhani alitakiwa kupewa tuzo ya mchezaji bora ili tulinganishe!