Messi ndie most overrated Player ever

Messi ndie most overrated Player ever

Hawa fifa wamejaribu sana kumbeba messi ila jamaa jana hakustaili!!! Mbappe jana ndo alikuwa man of the match

Man of the Match kivipi?? Ukiachana na goli 3 ambazo 2 za penalty kafanya nini kingine?? Mbappe kaja kuoneka dk70 wakati anafunga goli la penalty. Tutoe magoli yao tuangalie Performance nani anastahili?? Mpira sio magoli is more than that vinaangaliwa vitu vingi
 
Wewe utakua unavuta bangi sio bure au wewe mchawi mtu wa husda, Messi unaweza ukamlinganisha na mchezaji gani kama sio nguvu za bangi?
Tukiangalia career za mbappe na messi so far kwa kweli ni sawa na kulinganisha mbingu na ardhi lakini tukiangazia kwa mechi ya fainali peke ake ni mbappe ndie alitakiwa kuwa man of the match
 
Ila mbappe Jana alikuwa serious kweli na maisha🙉
 
Mkuu naomba usiihusishe bangi na mambo ya kipuuzi ...huyo ana matatizo yake mwenyewe
Ila nyie waongo mbape alikuja ibuka kipindi cha pili, man of the match ni yule alocheza vizuri mwanzo mwisho.
Mimi sina mahaba na messi kiviile ila alicheza vizuri mwanzo mwisho.

Out of topic, dah watoto wa france baadhi watamu kweli, ngozi nyeusi ina mvuto wake.

Argentina walistahili kombe hawakubebwa.
 
Mzee unakua sio kama mtu wa soka? Hizo web/App hazina uhalisia hawa ni Goal angalia rate yao
IMG_8074.jpg

IMG_8075.jpg

Mbappe ana 7.0 according to goal na Messi ana 8.1 acha mpira wa livescore
 
Shida sio kipaji mzee wangu! Game ya jana umeona lakini dogo mbappe mzigo aliyopiga???? Kafunga goli 4 jana tu kwann usiseme yeye ndo mchezaji bora wa world cup..... messi kabebwa sanaaaaa yani sanaa hata ile penalt wamepewa jana ni mchongo hamna penalt pale boss

Messi kafunga 3 na kachukua kombe kabisa
 
Ni kweli mkuu world cup kamaliza akiwa na goli 5 za penati na penati moja alikosa ilibidi ziwe 6

Messi kafunga penalty dhidi ya Saudia, Netherlands, Croatia na France jumla 4, kafunga goli dhidi ya Mexico, Australia na France jumla 3 ukijumlisha unapata goli 7. Hizo penalty zako 5 kafunga tim gani??. Mzee mpaka sasa mpira hujui maana unakuja na stats za uongo
 
Muache uchawi,,,ni ngumu kutoona Messi alichofanya jana labda kama ulikua unaangalia game Kwa makasiriko

1.Mbape hakuonekana mda wote wa mchezo mpaka ilipofika dk ya 70 ,,,kabla ya dk 70 alikua kama Peter Banda

2.Di Maria alikua na mchezo mzuri na Kocha alifanya makosa kumtoa,,, Messi alirekebisha makosa ya scallon

3.Martinez ni mwanaume dk ya 120 alifanya save bora katika maisha yake yote ya soka na kwa Wa Argentina na aliokoa penalty mbili kongole kwake

4 .Messi alifunga goli la Kwanza kumbuka penalty hua wanakosa, alichokifanya mpaka goli la pili linapatikana mungu tu ndo anaejua, Goli la tatu Kama ulikua france sawa ila kwa Argentina that was a Beautiful moment ever, penalty ya Kwanza alienda kupiga hakusubiri mambo yaharibike au ubishoo wa kupiga penalty ya mwisho, alitengeneza nafasi nyingi za kufunga kuliko mchezaji yoyote kwenye pitch kwenye ile fainal, Lautaro Kama angetulia au angekua mchezoni angebadilisha kazi alizofanya Messi kuwa magoli,,, yule mwanaume wa miaka 36 kafanya kazi ya vijana wa miaka 22

5.Acha uchawi na makasiriko Messi alistahili kuwa man of the match, Alikua akirekebisha mambo kila yalipokua yanaharibika,
Mkuu umemaliza kazi,,kwa dakika zote hizo si mbappe wala ufaransa walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wao.Watazamaji tunajisahau sana.
 
Kwangu mimi katika kikosi cha Argentina, Di Maria alikuwa kwenye kiwango bora zaidi kuliko Messi

Mbappe huyu nilimzungumzia sana jana, huyu ni mchezaji wa kipekee sana ila kinacho mkosti hana fanbase ya kutosha
MacAllister
 
K
Muache uchawi,,,ni ngumu kutoona Messi alichofanya jana labda kama ulikua unaangalia game Kwa makasiriko

1.Mbape hakuonekana mda wote wa mchezo mpaka ilipofika dk ya 70 ,,,kabla ya dk 70 alikua kama Peter Banda

2.Di Maria alikua na mchezo mzuri na Kocha alifanya makosa kumtoa,,, Messi alirekebisha makosa ya scallon

3.Martinez ni mwanaume dk ya 120 alifanya save bora katika maisha yake yote ya soka na kwa Wa Argentina na aliokoa penalty mbili kongole kwake

4 .Messi alifunga goli la Kwanza kumbuka penalty hua wanakosa, alichokifanya mpaka goli la pili linapatikana mungu tu ndo anaejua, Goli la tatu Kama ulikua france sawa ila kwa Argentina that was a Beautiful moment ever, penalty ya Kwanza alienda kupiga hakusubiri mambo yaharibike au ubishoo wa kupiga penalty ya mwisho, alitengeneza nafasi nyingi za kufunga kuliko mchezaji yoyote kwenye pitch kwenye ile fainal, Lautaro Kama angetulia au angekua mchezoni angebadilisha kazi alizofanya Messi kuwa magoli,,, yule mwanaume wa miaka 36 kafanya kazi ya vijana wa miaka 22

5.Acha uchawi na makasiriko Messi alistahili kuwa man of the match, Alikua akirekebisha mambo kila yalipokua yanaharibika,
Mbappe alijitahidi kutaka kufulukuta tangu mwanzo wa mechi ila alikosa ushirikiano maana dembele, giroud na griezman game iliwakataa kabisa mbaya zaidi midfielders za ufaransa tchouamen na rabiot ni defensive oriented zaidi kwaiyo mbappe akajikuta yupo peke ake asingeweza kupambana na mabeki yeye mwenyewe ni mpaka alivyotoka giroud na dembele france akawa tishio kule mbele ikampa nafasi na mbappe kuweza kupata upenyo wa kufanya mambo yake alicheza mpira kuanzia second half na sio uko dakika ya 70 unayosema kwenye suala la penati kumbuka mbappe pia alipiga penati ya kufunga goli la kwanza ina presha ukozingatia timu inahitaji kuchomoa ile finishing ya goli la kusawazisha nadhani uliiona mwenyewe that was a miracle hata baada ya kwenda matuta mbappe alipiga penati ya kwanza tukiangalia game neutral ni wazi kati ya mbappe au yule kipa ya argentina mmoja wapo ndie alistahili man of the match.. tukija kwenye suala la kiufundi kocha wa argentina alikosea sana kumtoa di maria pili yule Alvarez mechi ilimshinda alitakiwa kumwingiza lautaro martinez mapema maana baada ya lautaro kuingia alipachangamsha pale mbele na pia baada ya france kuchangamka kocha alitakiwa kutafuta namna ya kumpeleka lisandro martinez uwanjani kuimalisha ulinzi hii game ilikua haiendi 120 ni uzembe tu wa kocha., upande wa france kocha alikua faster kufanya sub sahihi dembele game ilimshinda kuanzia mwanzo wa mchezo nafikiri kitendo cha kumwacha benzema kimemghalimu maana hizi ndo game za benzema kufanya miujiza hata kama majeruhi angebaki nae tu kuanzia semis angekua ashapona kuna mtu anaitwa camavinga bhana yule dogo ana touch fulani hivi za kimasiahala masihala tu ila mara zote akiingia uwanjani huwa anabadilisha mchezo mfatilie hata akiwa real madrid ila nilicheka muda fulani game ipo extra unaambiwa france walikua waafrika watupu mzungu kipa tu
 
Kwangu mimi katika kikosi cha Argentina, Di Maria alikuwa kwenye kiwango bora zaidi kuliko Messi

Mbappe huyu nilimzungumzia sana jana, huyu ni mchezaji wa kipekee sana ila kinacho mkosti hana fanbase ya kutosha
Nafikiri baada ya messi na ronaldo kutundika daluga basi mbappe atapewa heshima anayostahili kwa sasa anafunikwa na vivuli vya hawa magwiji wawili ingawa currently uwanjani yeye ndie yupo productive zaidi
 
Back
Top Bottom