Muache uchawi,,,ni ngumu kutoona Messi alichofanya jana labda kama ulikua unaangalia game Kwa makasiriko
1.Mbape hakuonekana mda wote wa mchezo mpaka ilipofika dk ya 70 ,,,kabla ya dk 70 alikua kama Peter Banda
2.Di Maria alikua na mchezo mzuri na Kocha alifanya makosa kumtoa,,, Messi alirekebisha makosa ya scallon
3.Martinez ni mwanaume dk ya 120 alifanya save bora katika maisha yake yote ya soka na kwa Wa Argentina na aliokoa penalty mbili kongole kwake
4 .Messi alifunga goli la Kwanza kumbuka penalty hua wanakosa, alichokifanya mpaka goli la pili linapatikana mungu tu ndo anaejua, Goli la tatu Kama ulikua france sawa ila kwa Argentina that was a Beautiful moment ever, penalty ya Kwanza alienda kupiga hakusubiri mambo yaharibike au ubishoo wa kupiga penalty ya mwisho, alitengeneza nafasi nyingi za kufunga kuliko mchezaji yoyote kwenye pitch kwenye ile fainal, Lautaro Kama angetulia au angekua mchezoni angebadilisha kazi alizofanya Messi kuwa magoli,,, yule mwanaume wa miaka 36 kafanya kazi ya vijana wa miaka 22
5.Acha uchawi na makasiriko Messi alistahili kuwa man of the match, Alikua akirekebisha mambo kila yalipokua yanaharibika,