Pele ni kumchukua messi mguu wake wa kushoto uuweke kulia, kisha jumlisha na cr7 ndio unampata pele huyo mmoja.
Mimi ni shabiki wa Messi, nazungumza haya baada ya kipindi fulani nilikuwa najarobu kutengeneza documentary ya pele nikakwama kwenye mambo ya hakimiliki,
Pele tumsikie tu mzee alikuwa anajua mpira na kacheza kipindi kigumu saana, faulo za ajabu ajabu mechi aliyokuwa anatafuta kufunga goli la buku, alikula viatu si mchezo, world cup 66 kina Eusebio walipiga viatu vya hatari kiasi alisema hatocheza teena worldcup.. Ile game walimuumiza mguu wa kulia akawa anatumia wa kushoto.
Pele aheshimiwe.
Siku zoote messi alikuwa hashindanishwi na pele ni baada ya kuchukua world cup, kama ishu ni world cup pele anazo 3(2 katika hizo mchango wake ni 100%,58,70) Katika game 14 za world cup ana goli 12, assist 10.