Messi Vs Pele

Wewe ni shabiki wa ronaldo acha ubishi...mtu akisoma between the lines hata hufichi huo ushabiki wako.

Ronaldo anamzidi messi magoli ya vichwa lakini pace na ufungaji hamfikii messi maana messi ana pace kubwa na ana ratio kubwa ya magoli kwa mechi alizocheza.
Mwakani tu hapa Messi anamzidi Ronaldo idadi ya magoli.

Em wewe tuambie sasa...Huyo Pele anamzidi nini Messi???
 
Kwa maana hiyo hata hawa wavuta shisha waliochukua hii kombe wangeweza kukosa ingetumika system ya kipindi kile na yule dwarf angekosa hiyo sifa mnayompa hapa jukwaani
Amna anayevuta shisha apa....Enzi za Kina pele mabeki walikuwa wanatoka Uwanjani wanaenda kulima
Kidogo maforward walikuwa wana kamshahara ka kusastain life, ila mabeki ndo walikiwa wengi wafanyakazi wa viwandani, wakulima, + walikuwa heavy smokers...kipindi kile kuvuta ilikuwa ndio fasheni sasa
 
Enzi zenu za wapi wewe ? Kama tunaona matukio yaliyotokea kwenye ww2 , tushindwe kuona script za Pele , et Enzi zetu , yote aliyoyafanya Pele nasema yote clip zipo hakuna haja ya kudanganya watu...!!
Duh kwahio wewe una karai la bibi yako ambalo unaweza kuona hata mechi ambazo hazikuwa televised ?!!!!

Hivi unajua hata Game za mwanzo kuwa showed in Color ilikuwa 1966 England ambapo waingereza walihakikisha waandishi wa habari kutoka nchi nyingine ni wasizidi wawili na kila footage inachujwa na waandishi wao ?, Hivi unajua hata footage wakati timu za South America akiwemo na Pele wanafanyiwa Umafia nyingine zilikuwa hazionyeshwi....
Kwamba world Cup Messi kamzidi Pele ?, Kwamba Umri miaka chini ya 18 Messi alishachukua Kombe la Dunia ? Mtu anachukua kombe 1958; (akiwa kijana mdogo ever kwa kufunga bao) 1962 anacheza mechi ya kwanza anafunga bao ya pili anapigwa kiatu na kushindwa kuendelea na mechi nyingine lakini anachukua ndoo; 1966 anapigwa kiatu hadi kupelekea kujiuzulu (team zote za South America zinafanyiwa figisu na kutolewa ili Europe ichukue Kombe) anarudi tena 1970 anachukua ndoo tukija Messi kacheza Mechi za world cup nyingi kuliko wengi wengine kacheza Finals Mbili ila kachukua ndoo moja na hapo ni baada ya kukosa Penalty katika hayo mashindano na wakati mwingien akiwa captain kushuhudia team inapoteza a leading scoreline.....
magori kazidiwa , average stats za game ,
Unajua kitu kinaitwa ratio..., twende Spain anapojisifia kwa kufanya trade yake alafu niambia hata huko kama anaongoza kwa ratio ya magoli ?, Messi anafunga bali Messi is far from clinical....
goal and assist ndo mnajifichia hapo ,
Kwanza goal assists huenda Pele anazo nyingi kuliko hizo kipindi kile hazikuwa documented kwenye kila Mechi mpaka sasa labda ni kutafuta tafuta kwenye videos.... kwahio assists za Messi ni accurate za pele huenda nyingi zaidi
Kwa vile Messi anaendelea kucheza tutazifunika na hzo zotee....!!
Ngoja uone Messi kule PSG itakavyokuwa Messi inabidi utengeneze Timu kumzunguka unless otherwise anakuwa mzigo..., Messi sio Grafter.... Messi anatumia muda mwingi kwenye mpira anatembea tembea ukimba mpira ndio anafanya mambo
Kwamba Messi ana World Cup ngapi ? Kwa mchezaji ambaye ni mmoja kati ya watu wanaoongoza kucheza World Cup return on investment hairidhishi ni kama unainvest gunia kumi za mbegu unapata nusu gunia
 
Let be honest. Usichukie kubali kukosolewa. Umesema hv hujawahi kumshuhudia Pele. Yet unasema Messi ni zaidi sasa umewalinganisha vipi hapo!!???
Sina tabia ya kuchukia hovyo ila dharau ya kuita wengine hawajielewi huenda we ndiyo hujielewi
 
Imagine katika situation hiyo bado kibopa akaweza ku overcome hayo mazingira na ku score 1k goals bila kudrop kiwango

Ukimuweka modern player yeyote katika nafasi ya Pele hawezi kutusua
 
Imagine katika situation hiyo bado kibopa akaweza ku overcome hayo mazingira na ku score 1k goals bila kudrop kiwango

Ukimuweka modern player yeyote katika nafasi ya Pele hawezi kutusua
Pele hakuwahi kuvuta sigara...Imagine umuweke hata Mayele tu Vs wavuta sigara mapafu yameoza, si atakuwa anaondoka na Hattrick kila Mechi?
 
Umeuliza Messi na Pele

Mambo ya zizzou yametoka wapi.
Logic kama Ukiraka ndio ubora kuna Viraka kweli..., na nimekwambia sio ukiraka tu Pele hadi alikuwa Substitute Keeper na aliwasaidia Santos Game moja baada ya Kipa kupewa Kadi akarudi golini na akafanya yake golini baada ya huko mbele kuwa alishatupia Hat Trick (Talk about Man of the Match).....

 
Pele hakuwahi kuvuta sigara...Imagine umuweke hata Mayele tu Vs wavuta sigara mapafu yameoza, si atakuwa anaondoka na Hattrick kila Mechi?
Nitajie hiyo timu iliyokuwa na wavuta sigara ambayo Pele alikuwa akitumia advantage kuwafunga kwasababu yeye havuti
 
Amna anayevuta shisha apa....Enzi za Kina pele mabeki walikuwa wanatoka Uwanjani wanaenda kulima
Duh sasa huoni kwamba ukulima ni zoezi ?, Nani yupo fit mkulima au mcheza golf / playstation na msuka mikeka na muangalia Horse Racing ?
Kidogo maforward walikuwa wana kamshahara ka kusastain life, ila mabeki ndo walikiwa wengi wafanyakazi wa viwandani, wakulima, + walikuwa heavy smokers...kipindi kile kuvuta ilikuwa ndio fasheni sasa
Kuvuta sigara kunapunguza stamina na ku-hinder life span ya kucheza ila nimekuuliza kuvuta sigara kunafanya mguu usipige kiatu ?, wakati ule mabeki kazi yao ni kuzuia sio kupanda kusaidia attack kwahio ni kwamba ili kukupunguza makali unapigwa konzi za kutosha na kiatu cha kutosha.., kipindi kile beki unakuwa beki sababu ya nguvu yaani mtu akikupita kweli kafanya kazi...

Kuhusu kipato hivi unajua mpira ndio ilikuwa njia ya wananchi masikini angalau kutoka kwenye Poverty Cycle ? (ukiacha wachache kina The Doctor (Sio Doctor wa AKA bali Dokta MD wa kweli Socrates) wengi walikuwa wanatoka familia masikini.., na ukianza kucheza kama dogo kazi yako inakuwa kwanza kusafisha viatu vya mastaa wakubwa kwenye timu wanakupa posho za hapa na pale na baadae ukicheza posho zaidi kwahio mpira ulikuwa a means of getting extra / better income kuliko wengine...

Kwamba mtu anafanya kazi kiwandani alafu inakuja game ya kusafiri kucheza pengine unadhani kazini watamwambia nini chukua likizo ? (au unafananisha ndondo na ligi za zamani)?!!! Kipindi kile Vilabu vilikuwepo pia na Sponsor walikuwepo na hivyo viwanda n.k. vilikuwa na timu zao (na hili lilifanya ligi iwe na ushindani kutokana na kwamba gap in wealthy haikuwa kubwa)
 
Modern athletes wengi wana smoke na hakuna mtu mwenye shaka juu ya viwango vyao

 
Maelezo meengi halafu dah!!
Sidhani kama hata wewe unaamini unayoandika ila unaandika ili kubishana tu.

Kwahyo kuvuta sigara utakuwa na pumzi kama asiyevuta??
Yani points zako ni weak mpaka naona uvivu hata kuzijibu.

Anyways, Pele amemzidi nini Messi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…