Kama hatukuwahi kumshuhudia, inakuaje tuseme ni bora kumzidi Messi ambae tumemshuhudia? Kwamba tutumie clips za YouTube kujiaminisha kua Pele ni bora zaidi ya Messi tunaemuona day in day out?
Ni uongo!
Hoja kuu ya mashabiki wa Pele ni kwamba Pele alishinda world cup tatu. Tumewaambia, kushinda world cup sio kazi ya mtu mmoja. Ni kazi ya team nzima. Sote tumeona ambavyo Mbappe amekiwasha kwenye hii world cup japo France hawakubeba kombe. Je ni sahihi kusema Dybala ni mkali kuliko Mbappe, eti kwakua Dybala ameshinda world cup mwaka huu ambao Mbappe hajashinda?
Ndio maana wengi wetu tunaamini Messi angeendelea kua GOAT hata bila kushinda world cup.
Huyu Pele hata rekodi zake hazieleweki. Vijana wa sasa wakizifikia, anasogeza tena ili tu aonekane kua yeye ni bora zaidi. Ndio maana sisi ambao hatukumshuhudia akicheza, tunashindwa kuamini hizo takwimu zake. Hawa akina Messi na Ronaldo, kila kitu chao kipo recorded na tunashuhudia.
Anaanza Messi, then Ronaldo, alafu ndio hao wazee wanafuatia. Mimi sioni Pele anamzidi vipi Cristiano Ronaldo!