Mexico: Mahakama Kuu yasema ni kosa kumshtaki au kumzuia Mwanamke kutoa Mimba

Mexico: Mahakama Kuu yasema ni kosa kumshtaki au kumzuia Mwanamke kutoa Mimba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mahakama Kuu ya Mexico imeamua kuwa uhalifu wa utoaji mimba ni kinyume cha Katiba, kwa kura ya pamoja Jumanne, uamuzi ambao utawawezesha wanawake wa Mexico kote nchini kutoa mimba bila kizuizi.

vigezo vya mahakama na Katiba, kumshtaki mwanamke anayetoa mimba katika kesi zilizoidhinishwa na mahakama hii", ameeleza Arturo Zaldívar.

Mahakama hii ilikutana kwa siku mbili ili kujadili uhalali wa Ibara za kanuni za jukumu la jinai za jimbo la Coahuila, kaskazini mwa Mexico, ambazo zinawaadhibu wanawake wanaotoa mimba, hadi kifungo cha miaka mitatu jela.

Ibara hizi zilipitishwa kwa kauli moja kuwa ni kinyume cha katiba na majaji kumi walioshiriki kikao hiki.

Chanzo cha kimahakama kimeeleza kwamba uamuzi huu kwa kweli una upeo wa kitaifa kwa sababu utawaruhusu wanawake ambao wanaishi katika majimbo ambayo utoaji wa mimba ni uhalifu kutoa mimba kwa uamuzi wa jaji.

RFI Swahili
 
Back
Top Bottom