Meya Kinondoni: Kuna mapungufu yaliyofanyika; Serikali iliwapa CCM Uwanja wa Biafra kwa ajili ya kuendeleza michezo

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, amesema kuwa kuna makosa yaliyofanyika katika matumizi ya eneo la wazi la Biafra, Kinondoni, ambalo limeanza kutumika kwa shughuli tofauti na makubaliano yaliyokuwepo wakati eneo hilo lilipokabidhiwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza kupitia Wasafi FM leo June 25, 2026, amesema:

"Mimi nakiri kwamba yapo mapungufu na madhaifu yaliyofanyika kwa yule tuliyemkabidhi kiwanja kile, ilhali masharti yake yalitaka kitumike kwa manufaa ya umma."

Hata hivyo, amefafanua kuwa eneo hilo la wazi halipo chini ya usimamizi wa Manispaa ya Kinondoni kwa sasa, kwani takribani miaka 20 iliyopita lilikabidhiwa kwa CCM baada ya chama hicho kuomba kumiliki eneo hilo na kulitumia kwa maendeleo ya michezo nchini.

Aidha, amesema kuwa kwa mujibu wa ramani ya mipango miji, eneo hilo limetengwa kwa ajili ya shughuli za michezo. Ameeleza kuwa hata wakati CCM walipokabidhiwa eneo hilo, makubaliano yalikuwa litumike kwa shughuli hizo. Amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi, kupitia msemaji wake, kinaweza kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu zilizofanya matumizi ya eneo hilo kuwa tofauti na makusudio ya awali.

Gulio Biafra lisitishwe

Wakati huo huo, katika taarifa iliyotolewa jana, Juni 24, 2026, Songoro Mnyonge alitoa maelekezo ya kusitisha gulio unaofanyika katika eneo la Biafra, akieleza kuwa unachangia msongamano usio wa lazima kandokando ya barabara.

Itakumbukwa gulio hilo limekuwa likifanyika kila Jumamosi, ambapo wafanyabiashara kutokana maeneo mbalimbali ufika kuuza bidhaa zao, hata hivyo baada ya eneo ambalo walikuwa wakitumia awali kuwekewa ofisi za kuuza magari walilazimika kusogea zaidi eneo la pembezoni mwa barabara.

Pia soma
~
Bado siamini CCM imetoa eneo la Biafra kwa mfanyabiashara wa showroom wakati lilikuwa tija zaidi kijamii
~ Nani ameruhusu uwanja wa Biafra-Kinondoni uliokuwa unatumika kwa shughuli za umma umegwe kwa mfanyabiashara?
 
Uwanja ule haukuwa wa ccm,anyway sawa
Kwanini wameondoa waliokuwa wanautumia kwa michezo nk na kuwapangisha wauza magari nk
Hivi huyu meya anajuwa watoto/vijana kinondoni hawana mahali pa kwenda kucheza,kufanya mazoezi na shuguli zingine
Mitoto inaishia kucheza vichochoroni kwenye mazingira hatarishi
Hebu nyie viongozi acheni ubinafsi,tamaaaaa
Mtauzaaa mtagawa maeneo yote ya wazi au kwa sababu mitoto yenu mnawapeleka kucheza sehemu maalum zile za kulipia kwa masaa
Tuna watu selfish na war ohooo

Ova
Dkt. Gwajima D
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, amesema kuwa kuna makosa yaliyofanyika katika matumizi ya eneo la wazi la eo ambalo walikuwa wakitumia awali kuwekewa ofisi za kuuza magari walilazimika kusogea zaidi eneo la pembezoni mwa barabara.
Jiji la JOTO lisilo hata na BUSTANI wala CITY PARK.

Ni upumbavu IN and OUT.

BARS na KELELE tu
 
Safi sana watanganyika awajitambui nimwendo w kuwapelekesha tu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Uwanja ule haukuwa wa ccm,anyway sawa
Kwanini wameondoa waliokuwa wanautumia kwa michezo nk na kuwapangisha wauza magari nk
Hivi huyu meya anajuwa watoto/vijana kinondoni hawana mahali pa kwenda kucheza,kufanya mazoezi na shuguli zingine
Mitoto inaishia kucheza vichochoroni kwenye mazingira hatarishi
Hebu nyie viongozi acheni ubinafsi,tamaaaaa
Mtauzaaa mtagawa maeneo yote ya wazi au kwa sababu mitoto yenu mnawapeleka kucheza sehemu maalum zile za kulipia kwa masaa
Tuna watu selfish na war ohooo

Ova
Dkt. Gwajima D
Ule uwanja Toka zamani tunacheza Mpira pale, Kumbukumbu Fc, Nyuki

CCM waharibifu sana, bado pale kwa mwalimu ule uwanja wanaulia timing tu
 
Huyu Meya uzuri namjuwa vzr,yy mwenyewe alienda kujenga bwawani eneo ambalo wkt wa mvua pana jaa maji
Hawa maeneo mengi ya wazi wameyamaliza
Jiji hata hakuna sehemu ya kupumua
Wamejaa tamaa,wabjnsfsi,war ohooo

Sawa sawa ,pale kwake napajua
 
Kuna maswali bado najiuliza.
1.Kama Uwanja ukikuwa ni serikali.
utaratibu gani ulitumika kuwapa CCM uwanja, waliuziwa?, au walipewa tuu?
Kama walipewa tuu, ni utaratibu upi?

2. Kama waliomba uwanja kwa ajili ya michezo, kubadirisha matumizi, si kosa? Si inatakiwa wanyang'anywe?
 
Uwanja ule haukuwa wa ccm,anyway sawa
Kwanini wameondoa waliokuwa wanautumia kwa michezo nk na kuwapangisha wauza magari nk
Hivi huyu meya anajuwa watoto/vijana kinondoni hawana mahali pa kwenda kucheza,kufanya mazoezi na shuguli zingine
Mitoto inaishia kucheza vichochoroni kwenye mazingira hatarishi
Hebu nyie viongozi acheni ubinafsi,tamaaaaa
Mtauzaaa mtagawa maeneo yote ya wazi au kwa sababu mitoto yenu mnawapeleka kucheza sehemu maalum zile za kulipia kwa masaa
Tuna watu selfish na war ohooo

Ova
Dkt. Gwajima D
Hii ndiyo sabavu vijana wengi wamekuwa mateja
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, amesema kuwa kuna makosa yaliyofanyika katika matumizi ya eneo la wazi la Biafra, Kinondoni, ambalo limeanza kutumika kwa shughuli tofauti na makubaliano yaliyokuwepo wakati eneo hilo lilipokabidhiwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza kupitia Wasafi FM leo June 25, 2026, amesema:

"Mimi nakiri kwamba yapo mapungufu na madhaifu yaliyofanyika kwa yule tuliyemkabidhi kiwanja kile, ilhali masharti yake yalitaka kitumike kwa manufaa ya umma."

Hata hivyo, amefafanua kuwa eneo hilo la wazi halipo chini ya usimamizi wa Manispaa ya Kinondoni kwa sasa, kwani takribani miaka 20 iliyopita lilikabidhiwa kwa CCM baada ya chama hicho kuomba kumiliki eneo hilo na kulitumia kwa maendeleo ya michezo nchini.

Aidha, amesema kuwa kwa mujibu wa ramani ya mipango miji, eneo hilo limetengwa kwa ajili ya shughuli za michezo. Ameeleza kuwa hata wakati CCM walipokabidhiwa eneo hilo, makubaliano yalikuwa litumike kwa shughuli hizo. Amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi, kupitia msemaji wake, kinaweza kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu zilizofanya matumizi ya eneo hilo kuwa tofauti na makusudio ya awali.

Gulio Biafra lisitishwe

Wakati huo huo, katika taarifa iliyotolewa jana, Juni 24, 2026, Songoro Mnyonge alitoa maelekezo ya kusitisha gulio unaofanyika katika eneo la Biafra, akieleza kuwa unachangia msongamano usio wa lazima kandokando ya barabara.

Itakumbukwa gulio hilo limekuwa likifanyika kila Jumamosi, ambapo wafanyabiashara kutokana maeneo mbalimbali ufika kuuza bidhaa zao, hata hivyo baada ya eneo ambalo walikuwa wakitumia awali kuwekewa ofisi za kuuza magari walilazimika kusogea zaidi eneo la pembezoni mwa barabara.
Barabara ya kawawa road ,shemful

USSR
 
Malizeni tu maeneo yote ya wazi.....urohooo umewazidi
Nyie

Ova
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, amesema kuwa kuna makosa yaliyofanyika katika matumizi ya eneo la wazi la Biafra, Kinondoni, ambalo limeanza kutumika kwa shughuli tofauti na makubaliano yaliyokuwepo wakati eneo hilo.
hahahahaa wamempa yule jamaa kajenga Yard ya Magari
 
Back
Top Bottom