Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, amesema kuwa kuna makosa yaliyofanyika katika matumizi ya eneo la wazi la Biafra, Kinondoni, ambalo limeanza kutumika kwa shughuli tofauti na makubaliano yaliyokuwepo wakati eneo hilo lilipokabidhiwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza kupitia Wasafi FM leo June 25, 2026, amesema:
"Mimi nakiri kwamba yapo mapungufu na madhaifu yaliyofanyika kwa yule tuliyemkabidhi kiwanja kile, ilhali masharti yake yalitaka kitumike kwa manufaa ya umma."
Hata hivyo, amefafanua kuwa eneo hilo la wazi halipo chini ya usimamizi wa Manispaa ya Kinondoni kwa sasa, kwani takribani miaka 20 iliyopita lilikabidhiwa kwa CCM baada ya chama hicho kuomba kumiliki eneo hilo na kulitumia kwa maendeleo ya michezo nchini.
Aidha, amesema kuwa kwa mujibu wa ramani ya mipango miji, eneo hilo limetengwa kwa ajili ya shughuli za michezo. Ameeleza kuwa hata wakati CCM walipokabidhiwa eneo hilo, makubaliano yalikuwa litumike kwa shughuli hizo. Amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi, kupitia msemaji wake, kinaweza kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu zilizofanya matumizi ya eneo hilo kuwa tofauti na makusudio ya awali.
Gulio Biafra lisitishwe
Wakati huo huo, katika taarifa iliyotolewa jana, Juni 24, 2026, Songoro Mnyonge alitoa maelekezo ya kusitisha gulio unaofanyika katika eneo la Biafra, akieleza kuwa unachangia msongamano usio wa lazima kandokando ya barabara.
Itakumbukwa gulio hilo limekuwa likifanyika kila Jumamosi, ambapo wafanyabiashara kutokana maeneo mbalimbali ufika kuuza bidhaa zao, hata hivyo baada ya eneo ambalo walikuwa wakitumia awali kuwekewa ofisi za kuuza magari walilazimika kusogea zaidi eneo la pembezoni mwa barabara.
Pia soma
~ Bado siamini CCM imetoa eneo la Biafra kwa mfanyabiashara wa showroom wakati lilikuwa tija zaidi kijamii
~ Nani ameruhusu uwanja wa Biafra-Kinondoni uliokuwa unatumika kwa shughuli za umma umegwe kwa mfanyabiashara?