Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita achukuliwa na Polisi akiwa kwenye kikao

Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita achukuliwa na Polisi akiwa kwenye kikao

Chakaza,
Wapinzani wanaogopa kumwaga mboga,ila nahisi huyu jamaa aliweka uzbe wa watu kupiga vyao ukizingatia Ni mwaka wa uchaguzi lazma apishe Kwanza baadae Sana arudishwe
 
Madaraka ya kutumia nguvu yanapunguza ustaraabu wa watanzania waliouzoea.Kuvunja katiba na sheria tuepukane navyo vina athari nyingi
 
Wapinzani wanaogopa kumwaga mboga,ila nahisi huyu jamaa aliweka uzbe wa watu kupiga vyao ukizingatia Ni mwaka wa uchaguzi lazma apishe Kwanza baadae Sana arudishwe
Tatizo kubwa ni hela za uchaguzi 2020
 
Kwa hiyo huyu anashiriki kuwa gandamiza wana Dar es Salaam?
tapatalk_1579260277618.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka 9th December 2019 mlisema mmefungua mlango wa maridhiano na hao jamaa.

Waliohoji huo upopo wa kusherekea Uhuru mkiwa na pingu mkawajia juu na kejeli kibao.

Kiko wapi sasa,Meya anatolewa ofisini kama kibaka tu na hakuna hata anaye react si chama si waliompigia kura wala si hao mnaowashobokea.

No fear huku mnafokea nyuma ya keyboards tu.

Kama hujui uendako,njia yoyote itakufikisha!

Mtaweza kweli kuidai hata hiyo tume huru before November? Kwa hashtags mitandaoni?
 
Acha kuongea kama hooligan, sometimes tuwe serious kwenye mambo ya msingi.
Unalolijua liweke wazi ili tuwasulubu, tumechoka na mambo ya kitoto ndani ya jiji letu. Kama Mkuu wa mkoa analeta mkanganyiko basi waseme tuu tujue hata kama hawezi ondolewa na aliyemuweka ni vema tujue na tuweke kumbukumbu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Shida ya huyu meya ni nini hasa? Naona kuna malumbano ambayo kusema ukweli sielewi msingi wake ninini
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Chadema kanda ya Pwani, ni kwamba Mstahiki Mayor amechukuliwa na watu wanaosadikika kuwa ni watu wa usalama. More news to follow

======

View attachment 1325384
Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita (CHADEMA) akiongoza kikao cha Kamati ya Fedha na Uongozi, leo tarehe 16 Januari 2020, katika ukumbi wa Karimjee.

Baadaye kikao kilivurugika hadi kuitwa Polisi, baada ya mashauriano ya muda mrefu, waliondoka na Meya kwenda kituo cha Polisi Kati.

Dar es Salaam. Kikao cha Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kimeitishwa leo na huenda kukatokea mwendelezo wa mvutano wa kugombea umeya wa jiji la Dar es Salaam.

Meya aliyeng’olewa, Isaya Mwita, ambaye anang’ang’ania kuwa yeye bado anashikilia kiti hicho atakuwa na nafasi ya kupima upepo wa nafasi yake wakati atakapojaribu kuongoza kikao hicho.

Kwani tayari Naibu Meya wa jiji hilo, Abdallah Mtinika ameiambia Mwananchi kuwa yeye ndiye atakayeongoza kikao hicho baada ya Mwita kuondolewa nafasi yake.

Hata hivyo, Mwita, ambaye ni diwani kupitia Chadema kwa upande wake amesisitiza leo atakwenda kuongoza mchakato huo.

Kwa mujibu wa barua ya wito ambayo Mwananchi imeiona, kikao hicho kitafanyika katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 8.00 mchana.

Miongoni mwa ajenda za kikao ni pamoja na kusoma na kuthibitisha muhtasari wa kikao cha kamati ya fedha na uongozi kilichofanyika Desemba 23 mwaka jana na taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi huo.

Pia kikao hicho kinatazamiwa kupitia taarifa ya wito iliyotolewa na Mkurugenzi wa jiji, Sipora Liana.

Kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mwenyekiti wa kikao hicho ni meya lakini hadi sasa bado kuna sintofahamu na utata wa nani atakayeongoza mkutano huo leo.

Sintofahamu hiyo inatokana na utata uliojitokeza katika mkutano mkuu maalum wa baraza hilo uliofanyika Januari 9 mwaka huu ambao wajumbe 16 wa CCM walipiga kura ya kutokuwa na imani na Mwita kutokana tuhuma zinazomkabili.
Miongoni mwa tuhuma anazokabiliawa nazo Mwita ni kutotumia Sh5.8 bilioni za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Udart).

Fedha hizo ni asilimia 51 ya hisa zilizotolewa na kampuni ya Simon Group kama sehemu ya ununuzi wa asilimia 51 ya hisa za Uda.

Wakati tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya gari la ofisi ambalo liligongwa wakati likiwa na dereva wake.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti Mwita amekana kuhusika na tuhuma hizo akidai si za kweli na kwamba zina lengo la kumwondoa katika nafasi hiyo aliyohudumu kwa miaka minne.

Hata hivyo, wafuatiliaji wa siasa za jiji la Dar es Salaam wanadai huenda suala la fedha za Udart likajadiliwa kwenye kikao hicho.

Madiwani walioongoza harakati za kumng’oa walimtupia lawama Mwita kwa kuzuia kutumika kwa fedha hizo.

Jana Mwananchi lilimtafuta Naibu Meya wa jiji hilo, Mtinika kutaka kujua nani atakayeongoza kikao hicho ambaye alijibu, “Mimi ndiye nitakayeongoza na si mwingine nawakaribisha watu wote,” alisema Mtinika ambaye ni Diwani wa Kibondemaji Mbagala.

Wakati Mtinika akieleza hayo, Mwita ambaye ni Diwani wa Vijibweni licha ya kutopewa barua ya wito wa kikao hicho yeye amedai bado ni meya na kwamba leo ataongoza kikao hicho kama mwenyekti akidai yeye ndiye mtu sahihi ya kukiongoza.

“Inawezekana wamepeleka barua ya wito ofisini, maana leo (jana) sijaenda, nipo nyumbani. Kesho (leo) nitakwenda kuongoza kikao hicho kwa sababu ndiye mwenyekiti,” alisema Mwita, ambaye amedai kwa sasa ameamua kufanyia shughuli za umeya nje ya ofisi kutokana na kuhofia usalama wake.

“Nimeamua nitawatumikia wakazi wa Dar es Salaam nje ya ofisi, pale Karimjee. Ndani siwezi kuingia hadi mambo yatakavyokuwa shwari,” alisema Mwita.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, Patrick Assenga alisema amepewa barua ya wito, huku akisema endapo mwenyekiti wa mchakato huo hatokuwa Mwita hakuna kitakachofanyika.

“Ninachojua mwenyekiti wa kikao ni Mwita si mtu mwingine. Tunakwenda tukijua mwenyekiti wetu ni Mwita vinginevyo hatutaelewa,” alisema Assenga, ambaye ni diwani wa Tabata.

Chanzo: Mwananchi
Yote haya yanatokea na yataendelea kutokea zaidi ya haya kwa sababu watanzania wanayaridhia. Tanzania itaendelea kuongozwa kijinga na kijambazi na kishamba mpaka pale watanzania watakapoamka na kuamua kuweka mustakbali wa taifa lao mbele ya matumbo yao!
 
Shida ya huyu meya ni nini hasa? Naona kuna malumbano ambayo kusema ukweli sielewi msingi wake ninini

..Meya anadai akidi haikufikiwa ktk kikao cha madiwani kilichoazimia kumuondoa.
 
Shida ya huyu meya ni nini hasa? Naona kuna malumbano ambayo kusema ukweli sielewi msingi wake ninini
Shida siyo ya Meya , shida iko ccm kwa kulazimisha kumuondoa Meya halali kinyume cha Katiba , hii ni kwa sababu amekataa kujiuza na hivyo kuzuia mpango wa ccm wa kuiba fedha za jiji ili kugharamia rushwa ya uchaguzi mkuu 2020
 
Shida siyo ya Meya , shida iko ccm kwa kulazimisha kumuondoa Meya halali kinyume cha Katiba , hii ni kwa sababu amekataa kujiuza na hivyo kuzuia mpango wa ccm wa kuiba fedha za jiji ili kugharamia rushwa ya uchaguzi mkuu 2020
Ni Kama ulikuwa kichwani mwangu ndg,👊
 
Back
Top Bottom