Meya wa Jiji la Dar kuzindua kinachoitwa 'Chawa wa Mama'

Meya wa Jiji la Dar kuzindua kinachoitwa 'Chawa wa Mama'

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba , tarehe 14/01/2023 kwenye ukumbi wa Karimjee , Jijini DSM , kutafanyika Uzinduzi Kabambe wa kile kinachoitwa CHAWA WA MAMA .

Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari inaonyesha kwamba shughuli hiyo itasimamiwa na Mstahiki Meya Kumbilamoto , na Kwamba Wasanii kadhaa watatumbuiza , akiwemo Zuchu kutoka Wasafi .

Bali hakuna vigezo vyovyote vilivyotajwa kwa mtu kutambulika kuwa Chawa , lakini tunadhani Kusifia sifia kila kitu yaweza kuwa kigezo kikuu

Kwangu hili jambo ni jipya kabisa , na kwa kweli sijawahi kuona jambo kama hili likizinduliwa popote Duniani , Je sisi tuko mbele zaidi au tuko nyuma ?
 
FB3F7D82-4395-4423-9A73-CAF687CA32BE.jpeg

🤣🤣🤣tulipofikia
 
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba , tarehe 14/01/2023 kwenye ukumbi wa Karimjee , Jijini DSM , kutafanyika Uzinduzi Kabambe wa kile kinachoitwa CHAWA WA MAMA...
Tuko nyuma sana.

Hili neno bora wangelitafutia kirefu chake, lakini kama ni chawa huyu ninayemjua kama mdudu anayeishi kwa watu wachafu, ni ujinga hasaa.

Wanafanya makusudi ili kuwakera wasiompenda wakidhani wako sahihi, kumbe wanajishusha!
 
Back
Top Bottom