RUTAGAMBWA
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 516
- 256
Polis ingetumia nguvu hizo kibiti nadhani mauaji yangeshaisha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wa wilaya anataka waombe kibali kutoka kwa manispaa cha kwenda kufanya ziara kwenye miradi hii ndio tanzania mpyavip wale waliotajwa katika ripoti ya acacia wameshakamatwa kwa mahojiano au ndo tusahau tena?
Anajua wapi kibibi huyu anajua kutetea tu ujinga kwa kudhani yeye ni mwerevu, juzi alikua analia baada ya kuona Ana mgairwa kuteuliwa kua mkuu wa mkoa yeye kabaki solembatuambie wewe kama unajua
Meya kihelehele huyu, tuna mameya karibu sita katika jiji hili lakini huyu meya kazi kuuza sura tu kwenye media, sijui hana kazi, mara kamshitaki Makonda, mara kaandamana bomoabomoa. ndio alitaka umeya wa jiji la Dar huyu, ovyooo!
Sawa na yule wa Arusha kashapiga m300 za kwenye msiba wa mzee ndesa saivi wapo kimya. familia ya ndesa inalilia rambirambi.
Hivi hawa CCM ni nani aliyewaroga? Nilimsikia mkuu wa wilaya ya ubungo akimtuhumu Meya Jacob eti "anajiita Meya". Ikiwa mkuu wa wilaya hamtambui Jacob kama ni meya unategemea nini? Hii nchi imerogwa na CCM.View attachment 526952
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekamatwa na Polisi kwa ajili ya mahojiano kituo cha polisi Mbezi, sababu haijajulikana.
========
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hata hivyo sababu za kuchukuliwa kwake bado hazijawekwa wazi.
Tukio limetokea leo Jumatatu saa sita mchana katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Kibamba.
Askari wapatao wanne wakiwa katika gari aina ya Land Cruise walifika katika eneo hilo kisha kuzuia msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa tayari kuanza ziara ya kutembelea manispaa hiyo.
Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.
Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.
"Tunakuomba uongozane na sisi hadi kituoni tuna maongezi na wewe yasiyozidi dakika 10 tukiridhika tunakuachia uendelee na shughuli zako,"
Baada ya kumweleza hayo, ofisa huyo alikwenda moja kwa moja katika gari la Sumaye na kumweleza kuwa wanamuhitaji meya kwa dakika 10 kisha watamuachia.
Chanzo: Mwananchi
Hivi hawa CCM ni nani aliyewaroga? Nilimsikia mkuu wa wilaya ya ubungo akimtuhumu Meya Jacob eti "anajiita Meya". Ikiwa mkuu wa wilaya hamtambui Jacob kama ni meya unategemea nini? Hii nchi imerogwa na CCM.
Ndio maana hatujasikia wazee wa makinikia wakikamatwa kwa kuwa hakuna sababu ya kuwakamata.Unajuwa kakamatwa kwa sababu gani?
Mtabaki kulalama kutwa kucha.Ndio maana hatujasikia wazee wa makinikia wakikamatwa kwa kuwa hakuna sababu ya kuwakamata.
View attachment 526952