Meya wa Manispaa ya Ubungo, Ndg. Boniface Jacob akamatwa na Polisi kwa mahojiano

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Ndg. Boniface Jacob akamatwa na Polisi kwa mahojiano

Hivi kutakiwa kwa mahojiano kumbe nako ni kukamatwa? [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG]
 
Huo ni wivu wa kisiasa tu. Wanataka ccm tu nfo wasifiwe na si aliyeko nje ya ccm.
 
Meya kihelehele huyu, tuna mameya karibu sita katika jiji hili lakini huyu meya kazi kuuza sura tu kwenye media, sijui hana kazi, mara kamshitaki Makonda, mara kaandamana bomoabomoa. ndio alitaka umeya wa jiji la Dar huyu, ovyooo!
Sawa na yule wa Arusha kashapiga m300 za kwenye msiba wa mzee ndesa saivi wapo kimya. familia ya ndesa inalilia rambirambi.
Hivi huyu anapenda kiki na kuuza sura mitandaoni kama Bashite? 😀😀😀 Kuandika kwenye haujui🙄🙄🙄 kihelehele❌ kiherehere✔✔
 
Kama ni Salamu za pole ndiyo kosa Basi ndiyo akome kusalimia wazungu koko.

Tuna uchungu wa makinikia yetu then, yeye anawaonea huruma wazungu koko!!?

Acha akamatwe tu hakuna namna tena.
 
Mkoa wa Dar umekosa uongozi umekuwa kama genge la wahuni tu.
Mkuu wa mkoa hajitambui ....amekuwa mbabe kwa mambo ya kipuuzi tu.
Hiki Chuo cha NEC kinachowanyanyasa wanafunzi bila sababu ya msingi kama tulivyoona kwenye taarifa za habari yeye RC Makonda hana habari ya kinachoendelea yupo yupo yu.....ni kipi kero kwa wananchi kwa kadri ya uelewa mdogo wa Makonda?
JK hakukosea kuwapa wateule wake semina elekezi kuliko kuwateua tu na kuwaacha wafanye wanachokielewa wenyewe.
 
= yanawaimarisha
= kuimarisha

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Ninyi ndio wale wanaosemwa "wanachuja mbu na kumeza ngamia". kwamba unaweza kuacha mada kuu na kuingia kwenye typos. Kwa mfano Rais Magufuli anaposema "Tunataka Watanzania wapate LAHA" unaweza kumkosoa kweli, kwamba siyo LAHA bali ni RAHA, kama unavyokosoa typos, lakini katika GT tungependa zaidi kuangalia siyo tu typos, bali vitu vingine vya juu zaidi, kama SEMANTICS. hivi si wengi sana ambao wanashughulika navyo, wengi hupendelea kwenye "low levels" kama hapo ambapo inaonekana wewe hupendelea sana. ni wazo tu, sisemi umekosea, hapana, siku nyingine badilisha mtindo kidogo
 
It is dangerous to be right in the wrong government
 
Shetani bado anaendelea kutenda kazi zake, ila msichoke wala kukatishwa tamaa na husda za shetani. Bado kitambo kdg huyu shetani atashindwa vibaya sana. Tuzidi kulia na muumba wetu ili akomeshe hizi kazi za shetani.
 
View attachment 526952
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekamatwa na Polisi kwa ajili ya mahojiano kituo cha polisi Mbezi, sababu haijajulikana.

========

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hata hivyo sababu za kuchukuliwa kwake bado hazijawekwa wazi.

Tukio limetokea leo Jumatatu saa sita mchana katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Kibamba.

Askari wapatao wanne wakiwa katika gari aina ya Land Cruise walifika katika eneo hilo kisha kuzuia msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa tayari kuanza ziara ya kutembelea manispaa hiyo.

Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.

Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.

"Tunakuomba uongozane na sisi hadi kituoni tuna maongezi na wewe yasiyozidi dakika 10 tukiridhika tunakuachia uendelee na shughuli zako,"

Baada ya kumweleza hayo, ofisa huyo alikwenda moja kwa moja katika gari la Sumaye na kumweleza kuwa wanamuhitaji meya kwa dakika 10 kisha watamuachia.


Chanzo: Mwananchi
Acha Likamatwe na Lifungwe kabisa. Tumechoka nalo. Mijitu mingine shida tupu.
 
Yale yale ambayo Mr.Mayalla kayaandika katika mada yake,kisheria inatakiwa polisi wanapokukamata wakueleze haki zako zote,and why they are arresting u,including kukuonya kuwa utakachokitamka wakati ule wanaweza kutumika kama ushahidi dhidi yako,una haki ya kuita mwanasheria wako,una haki ya kukaa kimya,na hii inatokea sana hasa kama unafahamika ya kukuomba mwenyewe uende kituoni,huku ni kudhalilishana,ukiukwaji mkubwa wa kisheria,again tatizo lipo pale pale ya kuwa na katiba ya kikandamizaji,inaelekea kila kiongozi Tanzania ana uwezo wa kumtia ndani anyone,mambo aliyoyafanya RC Makonda nchi nyingine leo angekuwa na kesi kibao za madai,huwezi kuwatuhumu watu na ukawatangaza bila ya kuwa na evidence,huku ni kuuwa vipaji na brand za watu.
 
vip wale waliotajwa katika ripoti ya acacia wameshakamatwa kwa mahojiano au ndo tusahau tena?
Hapana tunaanza na Meya wa Chadema kwanza. Mkuu hao waliotajwa kwenye report zote mbili za profesors kuhusu makanikia na kuiingizia serikali yetu hasara kwa kukubali kusaini mikataba mibovu na Mhe.Rais kutoa agizo kuwa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria "effectively" effectively bado haijatimia, ila hawa wa Chadema ngoja tuwashughulikie haraka haraka si unajua siku hizi issue za wapinzani ndiyo zinazotuweka mjini? watu wa media watauza magazeti, wengine watapanda vyeo na kupandishwa madaraja, wengine tutaonekana ni watendaji wakutukuka.Na pia hao ndiyo wameisababishia serikali hasara kubwa sana kwa "kukutana" Hao waliotajwa tunasubiria ifike effectively kama ilivyosemwa, bado itafika watakamatwa mnawasi wasi gani wana JF? Kwanza wezi wakubwa ni "wadhungu" wamekuja na wameshakiri kosa. Tunasubiri watulipe trilioni zetu 386 tuwasamehe.
 
Back
Top Bottom